Zed
JF-Expert Member
- Mar 28, 2009
- 435
- 257
Katiba itakayo andikwa inaandikwa kulinda maslahi ya watanzania. Je vyama vya kidini au kikabila ni kwa maslahi ya watanzania? Sehemu ya katiba kuhusiana na dini ni kumhakikishia mtanzania uhuru wa kuabudu au hata kutoabudu ili mradi havurugi au kuingilia uhuru wengine na ustawi taifa. Sasa kama katiba itaweka article ya kuwa Tanzania ni secular state basi vyama vyenye sera za kidini vitakua vinakwenda kinyume na article hii. Ila kama itaweka dini rasmi ya au za taifa hili basi wazo lako la vyama vya kidini linaweza kuwa sawia. Kwa kuangalia demographic composition ya Taifa letu, endepo kutakuwa na article inayosema kila raia wa taifa hili ni sawa, basi kutakua na dini rasmi zipatazo 1500 au zaidi, kwani Tanzania si waislam na wakristo tu, bali nchi hii ina dini za asilia zinazozidi 1800, nyingine ni za kimakabila na nyingine ni za koo tu na nyingine za raia wenye asili ya mataifa mengine Hindu, Bahia, Sikhs n.k ! Kwa maslahi ya watanzania ninadhani Tanzania ibakie kama ilivyo sasa secular state ila iwahakikishie watanzania uhuru wao binafsi wa kuabudu au kutoabudu kulingana na ustawi wao na taifa.