Katiba ihusishe dini!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba ihusishe dini!!!!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Kadogoo, Feb 7, 2011.

 1. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tanzania wanaishi watu wenye dini mbalimbali na zaidi Waislamu na Wakristo! kumekuwa na malalamiko mengi ya chini kwa chini kuwa Dini haipewi nafasi ktk maamuzi mengi muhimu ya nchi yetu!
  Pia kuna malalamiko ya baadhi ya dini fulani kubaguliwa ndani ya nchi yao! na zaidi wimbo wa Serikali kuwa Dola haina dini ila watu ndio wenye dini!

  Wakati umefika kuandika katiba yetu mpya kwa kutambua rasmi dini zetu na kuacha kurudiarudia kauli ya kuchanganya dini na siasa! kauli hii imepitwa na wakati! Dini na viongozi wa dini wapewe nafasi stahiki ktk katiba yetu na iwe ruksa kuanzisha chama chenye mrengo wa dini! hata huko Ulaya mbona kuna vyama vyenye mrengo wa dini ya Kikristo? na vingine viko madarakani? kwanini hapa kwetu iwe haramu?
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Serikali yetu haina dini, ya wa huko ulaya tuwaachie wa huko huko ulaya je na wapagani hawana haki katiba iwawakilishe kwa serikali kutokuwa na dini. Haya mambo hayafai ukitaka kujua hayafai cheki historia ya Yugoslavia

  By the way Zubeda kila nikikuuliza swali hutaki kunijibu umeacha swali kule kwenye jukwaa la siasa kuhusu kukataliwa kwa RC naomba turudi kule ukanieleweshe..
   
 3. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapa tunazungumzia Katiba! habari za nilikuuliza swali ktk post za Siasa ningojee huko usichanganye mambo ili kuvuruga mada hii ya Kuingiza dini ktk Katiba!
  Mimi sijasema uislamu na ukristo pekee ndio katiba itambue, hujanielewa! ila Katiba yetu itambue dini zote hata kama ziko za Mashetani mradi ni wa TZ na wanafuata sheria! sasa unaposema Serikali haina dini na wala tusiwaige Ulaya bila ufafanuzi nashindwa kukuelewa Mkuu!

  Kama ya Ulaya tuwaachie wao basi hakuna haja ya kuwaigiza kwa demokrasia zao na tubaki na mfumo wetu wa kiimla wa tangu zamani!
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Du we mkali kwelikweli... (lakini naomba twende kule baada ya kujibu hapa ile na kule unijibu)
  Hatufanyi mambo kwa kuiga sababu wengine wanafanya, tunachukua vitu nchi nyingine ambavyo vina faida kwetu..na kwa kukupa mfano wa kwamba hili jambo halifai nikakwambia angalia yaliyotokea Yugoslavia..

  Nchi yetu inatambua mtu kutokana na character yake na sio imani kabila wala kitu kingine chochote..., kwahiyo kama unaona tufanye hivyo kwanini tusiweke hata kabila liingie kwenye katiba, kwamba kila kabila liwe na chama chake cha siasa?

  Hivi tumekosa kweli mambo ya maana ya kufanya hadi tuanze kufatilia vitu ambavyo havina tija na vinaweza kuigawa nchi?
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Crap as usual! Tanzania is a secular state
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Haina tija kwa taifa...kabla haijaingizwa kwenye katiba kushaanza vijineno sasa itakuaje likiwa written...nadhani nchi yetu tuna lulu ya watu wenye busara(sijasema wazee) hivyo hatuwezi kukubaliana na pendekezo jepesi namna hii!
   
 7. M

  Mtwike Senior Member

  #7
  Feb 7, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  No, Tanzania is an atheist State!
   
 8. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama TZ ni Secular State mbona Rais na Wabunge hula kiapo kwa kutumia vitabu vya dni? na kwanini Spika wa Bunge husoma dua kabla ya kuanza kikao chao bungeni? mbona siku ya Jumapili hakuna kazi ili watu waende kanisani sio? hii ndio tafsiri yako Mchungaji ya Secular state?
  Hivi kuna mtu anaweza kutufafanulia nini maana ya Secular State? ni nchi zipi muhimu hufuata siasa hii?
   
 9. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Dada tusipotoshe issue tukipata raisi mpagani sio lazima kiapo kiwe kwa kutumia kitabu cha dini, tutatafuta njia ya yeye kula kiapo kwa imani zake, kusoma dua kabla ya kikao cha bunge ni kuomba mwongozo kutokana na imani za watu (tukiendelea hivi utauliza kwanini watu wanasalimiana Salaam Aleikhum), Jumapili hakuna kazi kwenye mashirika mengi ndio taratibu walizojiwekea, hata jumamosi wengine hakuna kazi au wanafanya nusu siku..., (sababu ni weekend) wengine tunapiga kazi siku zote, siku ya kupumzika ni hata J3 depends on my commitments na mfuko wangu unaniambia nini...
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  suala la dini kwenye uandishi wa katiba liwekwe pembeni kabisa,sabb hata issue ya kutambua hizo dini itakua ugonvi mwingine i mean katiba ikitambua upagan,wafuasi wa dini hizi mbili zenye maguvu watapinga.lazima tujue tanzania ni nchi ya watu wenye dini mbalimbali ukristo,uislam,uhindu,singasinga,budha nao wapo,wapagan wanaoishi,kusaidiana na kuheshimiana bila kujali tofauti ya dini zao............dini kwenye katiba noooooooooooooooo.........
   
 11. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Zubeda kama jina lako linavyojieleza ni muumini wa dini fulani, tena watu wa dini hiyo hawana hoja yoyote isipokuwa dini tu. Ndio maana hata kielimu wako chini kisa dini, kazi zao kubwa ni udereve wa daladala kisa hawana elimu, shule zao aghalabu ni za mwisho kisa msisitizo ni dini. wao na DINI DINI NA WAO KILA KITU DINI DINI DINI DINI. Crap hebu jaribu kutazama maendeleo ya nchi acha kukalia dini dini tu.... Boredom
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa kukusaidia tu! Watu wana dini zao na wanaruhisiwa kuzifuata ila serikali kama serikali haina dini na haiongozi kufuata dini fulani. Tanzania is a secular state
   
 13. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mbona unatolea mfano Ulaya na siyo Uarabuni kama Iran, iraqi, Pakistan, Afganistan, Kuwait na hata Africa kama Somalia, Egypt, Eritrea, Morocco, Algeria nk?

  Sioni sababu ya kuingiza dini kwenye Katiba kwani tutakuwa tumewatenga wasio na Dini nao ni wengi tu.
   
 14. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Zubena, na wasiwasi na eulewa wako, unaweza kuniambia Spika huwa ana soma dua ya DINI ipi? Wabunge wanadini zao ila SERIKALI HAINA DINI! Na wala wabunge hawalazimishwi kuapa kwa kushika Kitabu cha Dini. Kingunge alipokuwa akiapishwa enzi zile ALINYOOSHA MKONO MTUPU bila kitabu chochote cha dini na ilikibalika!

  Suala la kupumzika Jumapili ni taratibu za nchi, binadamu anapofanya kazi lazima apumzike, inapokuwa Jumapili ama Jumamosi ni siku ya mapumziko, hawa ambiwi siku hiyo LAZIMA WAKASALI! Wewe unataka wafanyakazi wapumzike lini?
   
 15. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wazo lako zuri sana na linaheshimika, ila kumbuka sio watanzania wote ni waislamu na wakristo... wapo wapagani na dini nyingine nyingi tu.... sasa na wenyewe itabidi watambuliwe na serikali na kuruhusiwa kuanzisha vyama vyao... Sijui kama hiyo itakuwa nchi zaidi ya kichaka!!!:twitch:
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wapi Tanzania ni secular state? Pia ni vipi basi sheria zake haziko secular? What define a secular state?
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ndio hoja dhaifu kuliko ninavyodhani. Wewe ndio na wasiwasi na uelewa wako mnapodai serikali haina dini halafu mkawa mnalazimisha watanzania wawe wakristo sijui hoja yako inasimamia wapi? Mfano nakupa sheria zinatulazimisha tuwe wakristo? Jumapili inatambulika kiserikali kuwa ni siku ya mapumziko wakati sio wote tunaopumzika na kwenda kusali jumapili, pili mishahara yetu inaenda according to the calendar ya kikristo wakati wengine kalenda yetu ya kiislamu ipo (Hijri calendar), Sheria ya ndoa inatambua kuwa mke mmoja ndie anayetambuliwa kiserikali wakati waislamu sie tuna wake zaidi ya mmoja, sasa hizi sheria huoni kwamba zinatulazimisha tuwe wakristo!!!!

  Wewe unadai kuwa jumapili ipo duniani kote ni uongo kuna nchi mapumziko yao sio Jumapili. Niambie Uarabuni mapumziko yao lini??? Malaysia je? Indonesia ? Turkey? Sasa usilizungumze jambo usilolijua. Siku za mapumziko ziwe Ijumaa na Jumamosi au Ijumaa na Jumapili ili kuweza kuaccomodate the needs of all. Utaona hilo swala ni gumu kulitatua. Cha msingi kusiwepo na siku ya mapumziko ila watu wawe na siku zao mapumziko ili kama wewe jumapili unasali uende ukapumzike, vilevile kama wewe jumamosi pia, na ijumaa pia na taifa liendelee kuzalisha kama kawaida.
   
 18. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280

  "Nikawaambia mashehe nchi yetu haina dini" astakhafyulilah!!! astakhafyulilah!!! "Lakini watanzania wana dini" mashehe wakanielewa!! Nawewe elewa.
   
 19. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu acha choko choko, hiyo inawezekana kwa wazungu lakini hapa africa kwa sisi wenye ngozi nyeusi tutachinjana na tutaisha. isitoshe DINI ZOTE hazina asili ya Africa lakini waafrica ndio tunaoongoza kwa kubaguana kidini, asilimia zaidi ya 90 ya watu wa Zanzibar ni waislamu, je umeona kuna kiongozi mkristo pale?
  Nchi ya Nigeria kila siku utasikia mapigano ya waumini wa Kikristo na kiislamu lakini hilo halipo kwa waanzilishi. Hayo ni mawazo ya mwendawazimu bila shaka wewe ni nazi wa dini ya kiislamu
   
 20. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
   
Loading...