Kati ya watawala na wale waandamanaji ni nani mwenye mapenzi na Tanzania?

Kati ya watawala na wale waandamanaji ni nani mwenye mapenzi na Tanzania?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,252
Nikinukuu maneno ya Rais, kuwa "vurugu na uvunjifu wa amani huishia kupimana nguvu na uwezo wa kujihami, ila mazungumzo huzaa mshikamano. Sasa tuchague lenye manufaa kwetu, kwani usalama wa Taifa lolote hulindwa na wote kwa nguvu zote na gharama zozote"
Niongezee kwa lugha ya sasa, kwa wivu mkubwa! Sasa kuna ya kujiuliza hapa;

Mosi: Ni nani anaipenda kweli Tanzania kati ya hawa watawala na watawaliwa? Kati ya vongozi (tabaka lililopewa/lililojipa mamlaka ya kuwakilisha wengine) na wenye nchi? Kwa wizi ule na uporaji ule na ubakaji ule wa uchaguzi ni haki kusimama mbele za watu na kuwaaminisha una wivu mkubwa na Taifa hili?

Pili: Kila mmoja anasema anaipenda Tanzania na ndio maana akachukua hatua aliyochukua. Anasema vurugu na uvunjifu wa amani huishia kupimana nguvu na uwezo wa kujihami. Unapimana nguvu na kujihami vipi dhidi ya yule ambaye naye anataka kuiona Tanzania yenye neema? Tulio nje ya mifumo na madaraka kuna kitu hatukijui vizuri kuhusiana na hayo madaraka, kiasi cha kusema, kwa gharama zozote.

Watanzania hawakufikiria kuwa ingeweza kutumika nguvu kubwa kiasi kile. Bado weye madaraka pamoja na kuona matokeo ya matumizi ya nguvu kupitiliza, hawakusita kuteremsha lawama na vitisho vya nyongeza kwa wahanga. Inasikitisha kuona wale vijana wameshika bunduki na kuanza kumimina risasi za moto kwa vijana wenza na wadogo zao. Kama vile walikuwa wanawinda tetere. Hawana tena ubinadamu.

Tatu: Hii ni ngumu kidogo kuielewa. Ni hivi, watawala wenye nia ovu huvuruga uwiano. Uwiano kwa maana kwamba kilichopo kinashirikishwa kwa wote, japo si kila mmoja anaweza kupata kipande kilicholingana. Wao hutaka kupata zaidi na kufuru. Wakishafanikiwa kuvuruga uwiano, wale wanyonge hukasirika na kusononeka. Wako watakaomwachia Mungu ila wapo ambao hawatamwachia Mungu. Hapo ndipo mikingamo huanza.

Tunarudi kwenye nukuu yetu, wanyonge wanaanza kupimana nguvu na watawala. Watawala nao wanaonyesha uwezo wao wa kujihami. Ni bora basi wangejihami kwa kutumia rasilimali toka nje ya kinacholeta mikingamo. Huyu mnyonge ndiye anamlisha huyu mtawala, na mtawala anaongeza juhudi za kumkamua huyu mnyonge kuhakikisha anapata riziki yake ya kila siku toka kwa mnyonge, wakati huo huo akimchukia huyu mnyonge.

Sasa la kushangaza ni hili, mtawala akishafanikisha kumvuruga mnyonge na kumwondolea uhalali wenye haki kabisa, kwa lugha ya kompyuta tunasema ana format device na kuanza upya akiamini kabisa kuwa yaliyopita yamepita, bila kujali yanakumbukwa au la. Mfano mzuri ni suala la uchaguzi uliopita. Pamekuwepo na (hatuwezi kusema wizi wa kura) ubakaji wa uchaguzi. Watu wameona. Intaneti imezimwa. vyombo vya habari vimetishwa. Hatukujua nini kinaendelea kipindi cha "upigaji kura na wakati wa kuhesabu". Ila watanzania wanachojua ni kuwa uchaguzi ulibakwa vibaya mno!

Sasa watawala baada ya kumaliza hilo zoezi waka format kama nilivyosema kisha wakataka kuanza upya bila kujua kumbukumbu bado zipo. sasa watawala wanashangaa ni kwa nini hawa wanyonge hawataki kuanza upya? Si tumeshamalizana na zoezi lililopita? Mnataka nini? Mbona mnaleta vurugu? Hamjui kuwa amani ya Taifa hili inalindwa kwa nguvu zote na gharama zozote? Kwa nini mnataka kupimana nguvu? Mnao uwezo wa kujihami? Anaongea hivi sio kwa kuigiza bali kwa kumaanisha kabisa, kama vile hakuna kilichotokea awali. Ndio maana nikasema awali pengine hatujui kuna siri gani katika madaraka. Si jambo la kawaida.

Nne: Katika hili tukashuhudia unafiki mkubwa mno na uliopitiliza wa wale ambao tulitegemea wawe visemeo vyetu, hasa waandishi na vyombo vya habari. Mtawala mmoja anasema, kuhusu taarifa kuwa kuna fujo , ghasia, vifo vinaripotiwa na media za nje... ni hivi, kitakachorushwa na media za ndani (Tanzania) ndio uhalisia wenyewe. Habari yoyote itakayosikika na vyombo vya nje kinyume na media za ndani, sio taarifa sahihi.

Ina maana kuwa vifo vyote vilivyotokea na havikuripotiwa hata na chombo kimoja cha ndani ni vifo feki. Basi tusemeile ni kazi ya akili unde (AI). Hakuna uhalisia. Akaenda mbali na kusema mmeona sasa kile ambacho mlikitamani. Hii shut down imeleta madhara ambayo yataathiri na mataifa mengine. Mmeyataka wenyewe.

Hakuna mwanasiasa toka chama tawala alisimama na kusema lolote hadharani kuhusiana na vifo vilivyotokea. Wasanii karibu wote walikalia jambo hili kimya wakiendelea kusubiri miongozo toka juu. Dhambi ya unafiki italiangamiza Taifa hili. Hakika Polepole na Gwajima wakifa tutawakuta peponi. Yule Gwajima mama wa ustawi wa jamii alikuwa kimya siku ya uapisho akichezea tu simu. Shigongo, uko tayari kushiriki dhuluma hii? Na wengine wengi.

Nini kifanyike:
Bado sauti ya Polepole inaleta mwangwi kichwani mwangu. Utawala huu umefitinika. Hauna kibali. Damu iliyomwagika ni nyingi mno. Bado vyombo vya dola (hasa polisi) vinaendelea kutisha watu. Hawakomi, hawajifunzi. Wanataka tuamini kuwa kazi ya upolisi ni kazi ya laana. Kazi ya kitumwa. yani unatumwa tu bila kushirikisha ufahamu wako. Kati ya hawa polisi wengi wapo wachache wenye uelewa sana. Nawajua na wengine ni rafiki zangu, na wamenisaidia kwenye madhila kadha wa kadha.

Katika maridhiano yajayo, ni lazima jeshi la polisi LITAZAMWE UPYA. Muundo wake pamoja na udahili wake. Kazi ya upolisi isiwe ni kwa wale walioshindwa maisha kwenye tasnia zingine. Iwe ni kazi yenye kuhitaji elimu na akili na ufaulu mzuri ili wajitambue na kuacha kutumika namna hii.

Raisi akiendelea kutuhumu raia wake kuwa ni wahalifu na mamluki bado tatizo litaendelea kuwa kubwa. Aachane na hotuba za kuandikiwa na aongee kama mtu huru kwa kile alicho nacho moyoni. Bado ana nafasi ya kuponya Taifa hili. Wakati anaapishwa na kuanza kazi, raia walikuwa na imani naye kubwa mno na iliyopitiliza. Kadiri siku zilivyosonga watu waliona tofauti.

Sasa utaenda kuhutubia Bunge watu wakiwa na mtizamo hasi mno juu yako. Inawezekana taratibu raia wakaanza kuipata faraja kama ile waliyodhania mwaka 2022. Walisema mama anaupiga mwingi ila ikawa kinyume. Sasa wana siri zao mioyoni. Sio siri nzuri. Ikawe kinyume. Ukidhani 4R zimeenda na kazi iendelee utakuwa umekosea sana. 4R ndio zinaanza kazi Rasmi baada ya hafla ile ya uapisho. Kaulimbiu nyingine zozote utakazokuja nazo au kupewa kwa awamu hii nikwambie tu kuwa utaharibu. Kazitafakari tena 4R

Pengine hazikufanya kazi kwa kuwa hazikuwa na kazi. sasa zina kazi ya kufanya. Rebuild, Reconciliation, Reform na Resilience.
 
Kwa kuwa kwetu sisi wakatoliki mwezi huu ni mahususi wa kuwaombea marehemu, nami niungane na waumini wenzangu kuwatakia rehema nyingi.
Raha ya milele uwape ee Bwana, na mwanga wa milele uwaangazie. Wapumzike kwa amani, Amina 🙏🇹🇿
 
Naendelea na mada yangu.

Kilichotokea kwenye 4R za awali zilizokuwepo kama nilivyosema awali hazikuakisi yaliyokuwa yakihubiriwa kwa kuwa hazikuwa na kazi ya kufanya. Zile 4R zilikuwa kama ifuatavyo;

  • Reinstate: Hapa mifumo ya awali iliyokuwepo ilianza kurudi taratibu na ndio maana tukaona kuchanua sana kwa yule mtu. Sio kwa kumbato lile
  • Refusal: Hapa tunaona mifumo ilianza kuweka kando matakwa mengi tu ambayo ni kama vile yalikaribia kukaa sawa. Tukashuhudia nguvu ya upinzani ikianza kuwekwa kando na hatimaye yakatokea yalitotokea
  • Relapse: Tukashuhudia kurudi kule kwenye shida za awali. Tulidhani tunaenda Kanani kumbe tunarudi Misri. Ni kama mraibu aliyeshindwa kuendelea na tiba. Matokeo yake ni kurudi kwenye uraibu kwa kishindo. Wasiojulikana ilikuwa ni kiashiria tosha
  • Restrict: Kisha tukashuhudia m’binyo wa kipekee kuanzia kwenye siasa, dini, sheria hadi total shut down ya October.
Sasa zile 4R zingine ndio zitakuja kuyeyusha hizi ambazo zilileta dosari nyingi sana. Tuna Imani na Tanania. Tuna Imani na utaifa wetu.

Out of the ruins
out of the wreckage
can’t make the same mistake this time
we are the children
the last generation
we are the ones they left behind
And I wonder when
We gonna change it
Living under the fear
Till nothing else remains


We don’t need another hero
We don’t need to know the way home
All we want is life beyond the Thunderdome



Looking for something we can rely on
There’s got to something
Better out there
Love and compassion;
Their day is coming
All else are castles built in the air
And I wonder when we are ever
Gonna change it…

We don’t need another hero…

Tribute from Tina Turner
 
Back
Top Bottom