Kati ya Vitz na Passo ipi ina heshima?

Kati ya Vitz na Passo ipi ina heshima?

Kuna siku nilikuwa nimepata lift toka dsm kwenda ikwiriri ndani ya nissan double cabin kalitufukuza ka passo kakatupita hatukukaona tena, sijui yule dereva alikuwa anatafuta kifo!!
 
Mmh wakati mi natamani japo kumiliki hiyo passo wengine wanaponda,,kweli maisha yako tofauti sana
 
Hivyo vyote vilienda na mafuriko.sijaviona siku nyingi.bado vipo??ngoja nimuulize house girl wangu nilimnunulia cha kwenda nacho sokoni kununulia bamia na ngogwe.nitarudi baada ya muda

Hata hilo ulilo nalo wewe kuna wenzio wanabebea mbwa kwenda kuchoma chanjo. Unapo dharau vya wenzio ujue kuna wengine pia wanadharau cha kwako, unapo ona una cha gharama jua kuna wenzio wana vya gharama zaid ya ko, unapo rina na kiatu kizuri cha kutembelea wenzio wanaringa na baiskel nzuri ya kutembelea, wewe unapo ringa na baiskel wenzio wenzio wanringa na pikipi unapo ringa na pikipiki wenzio wanaringa na gari, unapo ringa na gari wenzio wanaringa na ndege , jitambue ,jitathimin, kisha anza kujidharaukwa maneno yako ya kipuuzi.
USHAURI KWA MTOA MADA
Kama unahitaji kitu chochote kwa matumizi yako jitathmin kwanza kipato chako na uwezo wako wa kukihudumia bila kujali ni cha hadh gani. Ukisikiliza maneno ya watu ubaweza kujikuta unafirisika kwa kushindana na maneno yao ,fanya kinacho kidhi mahitaji yako ,wengine huwa ni wapondaji wazuri sana lakini wao hawana kitu.
Ishi maisha yanayo endana na kipato chako kama ni gari hata ukinunua HAMMER bado wenye BUGATI na hata ukinunua BUGATI wenye CHOPA watakudharau hivyo kikufaacho wewe kwa kipato chako ndicho chako. Achana na maneno ya walimwengu.
 
Kati ya Vitz na Passo ipi ina
heshima?
Jibu: huku kwetu heshima anakuwa nayo Dereva/mwendeshaji. Gari ni mashine tu ya kusafiria.

Huku kwetu kuna mbwa kibao wanaendesha magari na pikipiki, lakini bado heshima yao ni MBWA TU.

hahahahahaha:thumbup:
 
Yote ni magari mazuri tuu inategemea na matumizi ya mtu mfano mimi siwezi kutumia gari kama Nissan Navara kuendea kazini kila siku kutokana na shuguli zangu..tatizo wabongo wengi ni ushamba,kasumba za kimaskini (poverty mentality) na kukosa upeo ndio kinachowasumbua.
 
Heshima! Huwa nashangaa viongozi wa kiafrika wanatumia gari za kifahari na misafara mikubwa kuliko viongozi wa mataifa yaliyoendelea. Heshima kwenye gari halafu kila siku kiguru na njia kuomba omba.
 
Dharau hizo!! Za wanawake kwani zina matiti???

Tangu nilipoandika kuwa vitz na passo zoteni gari za wanawake. Watoto wa kiume wanamiliki gari hizo wananishambulia sn.Sijui nijifiche wapi
 
Ukiwa na PASSO tena ya cc650 unajiepusha na kero za makonda wa daladala na midume inayovaa singilendi bila kusafisha makwapa asubuhisubuhi na majibu ya kero ya waliotoka kukorofishana na wandani wao alfajiri wakati huohuo chombo kinanusa wese kama bajaji.
 
Back
Top Bottom