deejaywillzz
JF-Expert Member
- Mar 11, 2014
- 637
- 224
Wote wana fursa za kujiajiri, inaegemea tu na capital uliyokuwa nayo.Habari,
Aisee niende kwenye swali,
Ivi kati ya Programmer na IT yupi mwenye fursa nyingi za kujiajiri na kuajiriwa, na endapo wataajiriwa yupi ambae atapokea kiasi kikubwa cha mshahara kupita mwenzake???
cc. Chief-Mkwawa mchambawima1 MK254 snipa Isac M Barbarosa Na wengineo
PoleMtu anapouliza swali sikuzote sio tu kwa niaba yake, ni kwa niaba ya wote
na usidhani labda alikuwa hajui labda,
Hata ivyo nadhani ukipitia comment utaona lundo la watu waliokuwa wanahitaji msaada ila walikuwa wanahofia kuuliza.
Sio kwamba najua vyote NO,
''Ruksa kunitoa ushamba kwa kitu nisichokijua, nitakuwa mshamba kwa dakika kisha I am professional'' -Fid Q
Heshima yako bro!kuliko kuingia kwenye Biashara kwa lengo la kupata fedha, bora ukatafute mtu akuajiri. Utaishia kuwa frustrated na pengine kujifia mapema. Kwa lugha rahisi ni kuwa kama motive yako ni kusoma ili upate fedha, CompSc na related branches are not for you!
cjui nikujibu vp maana programmer yupo ndani ya IT...Habari,
Aisee niende kwenye swali,
Ivi kati ya Programmer na IT yupi mwenye fursa nyingi za kujiajiri na kuajiriwa, na endapo wataajiriwa yupi ambae atapokea kiasi kikubwa cha mshahara kupita mwenzake???
cc. Chief-Mkwawa mchambawima1 MK254 snipa Isac M Barbarosa Na wengineo
They get paid because they solve problems. So chase problems and offer solutions and you get money. Chase money and you'll never catch them.Heshima yako bro!
So watu wanasoma CS ili wapate nini kama si pesa?? Najua kuna passion and all that but at the end what do you want to achieve? Money?
endapo wataajiriwa yupi ambae atapokea kiasi kikubwa cha mshahara kupita mwenzake???
Pitia taratiiiibu post zake, utamuelewa vema tu Mkuu!Ina maana kama sina mda ua pesa ya kwenda chuo siwezi kuwa programmer au web developer?
Nimekupata sawia mkuu!! Get required skills, find problems, solve them and ultimately they'll pay you!! Thank you!They get paid because they solve problems. So chase problems and offer solutions and you get money. Chase money and you'll never catch them.
Basic business principal that harshly applies in Engineering/IT/CS soma kipande hiki:
N i hapo Wabongo wengi wamechemsha. A lot of apps solves nothing other than showing off skills.Nimekupata sawia mkuu!! Get required skills, find problems, solve them and ultimately they'll pay you!! Thank you!
Mk254 umeongea bonge la pointi, IT ni tamu sana ukiwa na passion waeza fanya chochote na pia ina ulingo mpana wa kuchezea popote utakapoamua kucheza kuna networking ukii mastet na ukapata certification yake utandunda, ipo sytem administration and security nayo ina itamu wake, kuna ishu za graphics and design pia huku ipo kali tu na kuna programming ambapo hapa inahitaji ujitoe roho na nafsi. Pesa utaipata popote pale kwenye IT. Note usiige wala kukurupuka kusomea hii course kama haupo tayari kujitoa na kama wewe sio mfuatiliaji wa mambo hasa ya IT TECHNOLOGY.Njia moja rahisi ya kukumbana na deals kubwa hapa Afrika, ikiwemo kwetu Kenya na pia hata Bongo ni kama ukifanya kazi on sub-contractual basis. Ni vigumu kwa programmer akiwa mwenyewe kupata deals kubwa hususan za kiserakali maana lobbying ya manyang'au huwa kali sana na deals hazipokezwi kwa kufuata sifa.
Kawaida mimi huachia makampuni yashindane kupata deal halafu wenyewe wananijia nifanye implementation kwa kunipa kandarasi ya sub contract. Unawacha wanaandika winning proposal kwa tender, wanafanya lobbying balaa maana serikali na makampuni makubwa wanataka kuona proposals za kiajabu ajabu zenye kuonyesha watendaji wa kampuni wenye masters degrees na mambo makubwa ambayo hata hayahusiani na mradi wenyewe.
Sasa kampuni ikishinda, wanasaka programmer ambaye ataongoza implementation na shughuli inafanyika. Humu siwezi kutaja baadhi ya miradi ambayo nimetekeleza, lakini kwa kifupi nimehusika katika very top projects za kiserikali na mashirika binafsi.
Usiku huu wa leo hapa nafanya coding ya system ambapo nipo hotelini, nimekuja na wafanyi kazi 20 wa wizara fulani ambapo nipo nawapa darasa ya system fulani ambayo nimewatengenezea. Tutaishi hotelini humu siku 30 kila siku tunapitia system nikiifanyia maboresho kulingana na mapendekezo yao. Ni system nimeitengeneza ndani ya miezi sita.
So kwa kifupi, nawashauri madogo ambao wanataka kuingia kwa fani hii, wajifunze IT in general ndani na nje, halafu kisha wakomae na programming. Kazi zitawafuata tu... zipo, programmers ni wachache kwenye nchi zetu hizi. Tatizo wengi wanataka shortcuts, anajifunza programming language kwa mihemko na kujiita programmer.
Programming is a lifestyle, it's a way of life...ukianza inabidi ubadilishe maisha yako kabisa, unakua boring kwa marafiki maana huna muda wa kwenda kucheza cheza pool table kitaa.
fundi makenika...Ok kama I T ni teknolojia ya mawasiliano, unaitenga vp na programming.
Jamii forum ni sehem moja wapo tunapopata taharifa na kiwasiliana, je hapa haijatumika teknolojia ya habari? Ok na je programming haijatumika?
IT ni nani na proggramer ni nani?
Ninachojua kwny ofisi nyingi iwe za kiserikali au za kmpuni binafsi huwa wanatenga kitengo cha IT na si programming ingawa yaeeza kuwa ni ofisi ya kudeal na programming.
Mleta uzi naomba unijibu na mimi.
Kati ya fundi makanika na mtengeneza engine ya gari nani anapata deal nyingi.
Soko la programming ni kama vipi? au ni kutengeneza programu tu?Nitakujibu kwa maneno machache maana umeniita.
Binafsi nilizunguka mjini sana nikiwa muda mwingi nimefulia kipindi nafanya kazi general za IT kama vile computer and printer repairs, networking n.k.
Lakini baadaye nikaamua kukomaa na programming. Yaani sijajutia kwangu mimi kuwa coder. Inalipa na pia ina watu wachache maana wengi huanza kwa mihemko halafu wanaishia njiani. Lazima uwe na moyo wa chui, nguvu za simba na mvumilivu kama nyoka ili ufaulu kwenye taasisi ya programming.
Kubali kuwa chizi mwenye uwezo wa kufanya coding week yote huku unalala masaa machache sana.
Ukiwa na passion ya kihivyo utakua bingwa na kazi zitakufuata, wateja watakufuata, hutotaka kuajiriwa na mtu.
WatProgramming kwa Afrika bado mkuu!!.......hata kazi zinazohitaji programmer hapa Tanzania nafikiri pia ni chache sana!
Moja ya shida ya tanzania watu wanawaza soko kwanza Na hela kabla hawajaanza ku appreciate Na kuelewa nini maana ya computing.Ndo maana ni nadra sana kuona system programmers hapa kwasababu most of them(wana IT na CS)hawataki kwenda deep into the system Na ku devote time and passion kuelewa vitu.soko ni muhimu lakini tunabidi kwaanza tuanze ku appreciate computing Alf soko Ndo litafuata baadayeSoko la programming ni kama vipi? au ni kutengeneza programu tu?
nataka kuwa programm lakini nataka niome mwenyewe kama ulivyosema bila kwenda chuo sasa unanishauri nianzeje mm kama beginnerLabda hujanielewa, naomba urudie majibu yangu yote taratibu na utapata picha nzima ya nini ninachokisema. Fahamu kwamba chuo hakikufanyi uwe programmer, uwezo wa kuwa programmer ni juhudi zako mwenyewe. Ujifungie chumbani na kuyasahau ya dunia, wewe na vitendea kazi vyako hadi kieleweke.
Wapo watu wengi wenye shahada za sayansi ya kompyuta lakini kuandika software inakua shughuli, wamejaa nadharia tupu. Nilichokisema ni kwamba baada ya chuo kukuandaa kwenye mambo muhimu ya msingi, unafaa kuanza kutia bidii na kuhakikisha umekua programmer mwenyewe.
Wapo programmers wazuri ambao hawakupitia chuoni, lakini kila mmoja atakuambia ilibidi atumie nguvu nyingi sana ili kufanikiwa. Hivyo kama unao uwezo wa kupitia chuo, nenda kasome kwanza, lakini kama uwezo huo haupo, usikate tamaa, komaa, tafuta videos, download vitabu, andaa mazingira chumbani, jifungie ndani kitaa, ingia kwenye online forums za programmers, husika katika mijadala, pambana tu na kitaeleweka.