Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Mimi naona mtakuwa hamjamtendea haki jk,the incumbent-bado hajamaliza muda,tusubiri amalize then ndo tuwafanyie comparisson,coz ndan ya kipindi kilichobaki,anaweza badilisha upepo kabisa,au akaboronga kabsa,so lets wait- la sivyo tutakuwa tunafanya comaparison vitu ambavyo havipo sawa
 
acha chuki.. tafadhali pingana na hoja zangu hapa chini mstari kwa mstari.
1. kabla ya mkapa kuingia madarakani, maliasili zilikuwa hazijaanza kuvunwa. yeye ndie mvunaji wa kwanza na muandishi wa mikataba mibovu inayotugharimu hadi leo.
ninapoongelea maliasili namaanisha wanyama pori, misitu, madini,samaki na ardhi kwa ujumla.
2.ROSTAM AZIZ, EDWARD LOWASSA.ANDREW CHENGE,DAUDI BALALI, NAZIR KARAMAGI, JEETU PATEL, SOMAIYA E.T.C nadhani unajua walikutengenezwa na nani na ni nani anayewaondoa katika system hivi sasa.
3.nadhani unakumbuka viwanda viligawanywa kwa wahindi katika utawala gani.
4. na mashirika ya umma yalikufa na kugawanywa katika uongozi wa nani? kumbuka TANESCO na IPTL, TTCL na CELTEL, ATCje?
vipi kuhusu shirika la reli???? vipi kuhusu TIPER??? KAMA UNA ZAIDI YA UMRI WA MIAKA 15 HAYA YOTE UTAKUWA UNAYAJUA KUWA KAYACHAKACHUA NANI..........
5. vipi kuhusu uhuru wa kujieleza na kutoa maoni??? hivi enzi ya ben mkapa ungeweza kuandika uharo unaouandika hivi leo kwenye mitandao chochezi????
6.Mkapa alikuwa anaamini kuwa watanzania wote wasio viongozi ni mbumbumbu na hawastahili hata kusikilizwa na je KIKWETE Unamuonaje
7.Kikwete kajenga kilomita nyingi zaidi za barabara kuliko mkapa( nenda tanroads kwa uhakiki)
8.kasuluhisha mgogoro wa visiwa vya comoro single handed bila kutaka msaada wala ushauri wa wakoloni
9.kasuluhisha mgogoro wa kenya kila mtu anajua
10.kawafikisha mahakamani viongozi wa ngazi za juu kabisa serikalini watuhumiwa wa wizi na ubadhirifu wamali ya umma(tuhuma kuthibitishwa na mahakama11. ANACHUKIWA NA WAPENDA UBAGUZI(Wanasisa uchwara na waroho wa madaraka, viongozi wa dini mafisad wenye ajenda mbaya kwa taifa)


For sure weee bwana mdogo ulikuwa bonge la kilaza na inawezekana still U are a bonge la kilaza........my friend try to emancipate yourself from CCMm mental slavery, otherwise...... pole sana

Kimsingi umekubaliana na mimi yote hayo ( Nkapa + Kiwete) ni manyang'auu, hakuna mwenye afadhalii
 
Utafanishaje kiongozi anayeongoza kwa facts na kiongozi anayeongoza kwa propaganda!!! Mkapa na jk ni sawa na mlima kilimanjaro na kichuguu cha mchwa, respectively.
 
Hawakutawala kipindi kimoja kwa hiyo mazingira hayakuwa sawa kuweza kuwapima. Mfano wakati wa Mkapa serikali ilipata mapato mengi sana kwa kuuza mashirika ya umma, wakati wa Kikweti hakukuwa na mashirika ya kuuza. Milango ya makampuni ya madini ilifunguliwa kipindi cha Mkapa, wakati kipindi cha Kikwete ni makampuni yale yale yanajipanua tuu. Kikwete alipokea nchi kipindi cha matatizo ya umeme wakati kipindi cha Mkapa mbali na MV Bukoba mabwawa ya kuzalisha umeme hayakuwa na upungufu mkubwa. Mwisho wote wanatoka chama kimoja na wanasimamia sera zile zile Ujamaa na Kujitegemea,
 
Jamani acheni kumdhalilisha Mkapa, muacheni apumzike, huwezi ukamfananisha Mkapa na kamtu kama kikwete.
 
Wakuu naomba tuchambue kati ya Mkapa na JK ni nani aliyeweza kuleta heshma kubwa kwa nchi kimataifa,
na ninani aliyekuwa au anaheshimika zaidi kimataifa.
Mfano Mkapa aliweza kuiunga mkono Iraq wakati wa vita kwa kukataa hadharani kuiunga mkono US na kusema hatajali madhara yanayo weza kutokea kwa maamuzi hayo, ukizingatia US walikuwa wanatoa misaada mingi TZ.
Pia aliweza kuteuliwa kuwa M/kiti mwenza wa Utandawazi Duniani na Pia baada ya kustaafu, amekuwa akifanya shughuli mbalimbali za kimataifa.
JK kwa upande wake ameweza kumwalika Rais mstaafu wa US bw.Bush hapa nchini,pia akiwa M/kiti wa AU aliweza kusuluhisha mgogoro uliosababishwa na uchaguzi nchini Kenya.
Je kwa kutumia mifano mingi kadri inavyowezekana ni nani ambaye amejipatia yeye mwenyewe sifa za kimataifa na taifa kwa ujumla?
NB: Kati ya mambo yanayochangia taifa kuwa imara kimataifa ni pamoja na siasa safi,mahusiano ya kimataifa*diplomasia*,elimu ya watu wako,rasilimali ikiwamo na raslimali watu etc.
JK Zaidi, ameweza kujitambulisha sehemu nyingi hivyo TZ kufahamika, pia aliweza kumleta Bush na Rice hapa, hata Obama alipokuwa Ghana alimsifia sana JK .
 
5 vs 10? cant compare bt can say zis
dur Mkapa era, despite of the so called uwazi na ukweli verbally anounced, was contrary ! alikuwa dikteta , mwizi na Jambazi aliyelea majambazi na kuuza rasilimali zote na mashirika ya Umma kwa bei chee ,huku akikamua 10pcs na wasaidizi wake! ktk kuuza kuna cash fulani 3pc ya mrabaha ikaongeza pato la taifa,hii ndio ambayo wapaza sauti kuwa amekuza uchumi wanaisemea kumbe ni 3pc vs 97pc inayochukuliwa na wawekezaji! Akhsante jk pamoja na kuwa bado kuisafisha CCM umeonyesha uzalendo kwa mambo mengi, alaaniwe Pengo ambaye hakusema chochote wakati nchi inauzwa na Mkapa, leo analo la kusema kwa kuwa ujambazi umepungua sana, sadaka atapata wapi?
 
"Any one is innocent untill proved guilty".

Kwa sheria zetu mtu ni safi hadi apatikane na hatia.Wale wanaumlaum jk kwa kusema akina mramba ni safi hawajui sheria.Si kazi ya jk kutoa hukumu,yeye kashawafikisha mahakamani sasa kama akina Agustino hawafanyi kazi zao kuwahukumu mnataka jk afanye nini? Jaji Agistino anapaswa kujiuzulu kwa kushindwa kazi

Uuuuuwih...! Jaji Agustino aliwekwa hapo na JK kama alivyowekwa Jaji Makame NEC. Unategemea Agustino atawafunga mafisadi bila JK kukubali? Ni uchakachuaji tu kama alioufanya Makame!
 
ni aibu kumfananisha kikwete na ben. yaani akili ya ben ni pana kama mwili wake.
 
Hatuwezi kuwafananisha kwani mmoja ni muislamu na mwingine ni mkristu.
 
"Any one is innocent untill proved guilty".

Kwa sheria zetu mtu ni safi hadi apatikane na hatia.Wale wanaumlaum jk kwa kusema akina mramba ni safi hawajui sheria.Si kazi ya jk kutoa hukumu,yeye kashawafikisha mahakamani sasa kama akina Agustino hawafanyi kazi zao kuwahukumu mnataka jk afanye nini? Jaji Agistino anapaswa kujiuzulu kwa kushindwa kazi

Hapa Tanzania ni kinyume, kwanza you are guilty until you are proved to be innocent. Ben aliprove kuwa innocent mpaka alipobadilika kuwa guilty.
 
Mkiitwa matahira mnachukia. Mnalinganisha watu ambao wamewafanya muwe masikini.
 
JayKei zaidi bwana mkapa kaiba sana awamu ya mwisho maana wachagga mafisadi walimkalia kooni (Anna na Pesambili)

kwa kweli JK naona kajitahidi kidogo kuliko Mkapa Kwani Mkapa alikuwa Dikteta wakati JK anatuacha tujimwage kwa uhuru.
Hahahaha!!!!
 
Sio siri Mkapa alikuwa na matatizo yake ila alikuwa Rais mwenye maamuzi na msimamo. Hakuwa indecisive kama huyu tuliye nae. Natoa tu mfano mmoja. Kuna wakati Valambia aliishtaki serikali kuhusu rada na mahakama kuu ikaamrisha serikali ilipe shilingi bilioni 50 plus interest. Mkapa alikataa akasema mkataba ulikuwa wa hila na mkawaambia waziri wa fedha, gavana na mwanasheria mkuu kuwa kama pesa ikilipwa nao wajiuzulu. Ilibidi wapeleke sheria bungeni kuzuia mtu kushika mali za serikali. Pesa haikulipwa hadi leo na Valambia mwenyewe na mwanasheri wake Maira wameshafariki. Huyu ndie rais anayejua kuwa maslahi ya mafisadi hayawezi kuwa juu ya maslahi ya nchi. Kwanini Kikwete asifanye hivyo? Narudia, hii hela ikilipwa serikali itaanguka.
 
Hapa hapa Mkapa alikuwa anatupiwa madongo, leo watu wanatuambia alikuwa mzuri? ... subiri wanaojiita makamanda dhidi ya ufisadi waanze kuchangia, ...
 
Back
Top Bottom