Watu tutambue uongozi shupavu wa kamanda Mbowe. Amekuwa ni kiongozi mwenye msimamo uliopelekea kukijenga chama kilicho imara na madhubuti.
Kikwazo kikubwa kwa usalama wa taifa, CCM na serikali ktk kukibomoa CDM ni Mbowe, wametumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumshawishi arudi CCM ili wampe hata uwaziri ila mbowe alisimama imara kutetea msimamo wake hii imepelekea CCM kumchukia sana kamanda Mbowe, na wako tayari kufanya lolote ili tu kummaliza wakiamini kwamba wataweza kuisambaratisha CDM.
Leo hii Zitto atueleze utajiri mkubwa alio nao ameupata wapi? Mwaka 2005 alipoenda kugombea ubunge alisaidiwa gari pajero naikumbuka ili kufanikisha ushindi wake, leo hii Zitto anaendesha Hammer na magari mengine ya kifahari.
Mbowe ametumia mali zake ktk kukijenga chama, fuso za music, gari aliyokuwa akitumia Dr Slaa, na magari mengine mengi ndani ya CDM yote ni mali ya Mbowe na siyo CDM.
Anapotaka kukiuzia chama magari ambayo chama chenyewe kimeyachakaza kwa nini aonekane mbaya? Wanajamii mtambue ya kuwa Zitto anatumiwa na kwa hilo hatofanikiwa hata kidogo.
Kanyaga twende makamanda wa ukweli ndani ya CDM.