Salamu wana JF. Pamoja na kuwa mimi ni mara yangu ya kwanza ktk kutoa maoni kwenye mtandao wako, ninayo machache ya kuchangia kimawazo. Leo napenda kuchangia sakatala CDM, La kulumbana Mbowe na zito kwenye kikao. Nimefuatilia habari hizi kwa karibu, lakini hazijanifurahisha. watanzania wengi sasa tuna taka kuona chama badala ina kwepo itakayo ingoa CCM madarakani, ambayo kuwayo CHADEMA ndiyo inategemewa kufanya hivyo.
Suala la ununuzi wa magari mitumba inawahusu kamati kuu ya CDM, endapo wote walikubaliana kwa kikao halali. Hata hivyo Tsh. 480 mil. ni nyingi na magari ya mitumba. Lakini hata Zito na Mbowe kulumbana, wote wana makosa kwani wao ni viongozi. ZITO alikuwa wapi wakati budget ya kununua magari imepitishwa na wakati yeye ni ni N/katibu mkuu? Naye Mbowe haoni ni kutumia vibaya hela ya chama? Hawa wote wana tamaa ya uongozi na uchu wa madaraka, hawafai kuendelea kuongoza chama hicho kizuri kinacho kubalika kwa watanzania walio wengi.
Wengine wanachama wenye uwezo wagombee akina Mbowe na Zito sasa wasogee pembeni mpaka hapo watakapojirekebisha.
By Nada, The Prof.