Kati ya MBOWE na ZITTO, nani yuko sahihi?

Kati ya MBOWE na ZITTO, nani yuko sahihi?

Jiwejeusi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Posts
754
Reaction score
133
Ndugu zangu wajf, baada ya marumbano na minyukano baina ya MBOWE na ZITTO. Sasa naomba mwongozo wenu wanajf kwa kuuliza maswali yafuatayo:-
(a) Nini chanzo cha mgogoro wao!
(b) Mgogoro wao ni kwa maslahi ya nani?
(c) Kwa nini wanarumbana ktk kila kitu?
(d) Nini maslahi ya chama na wanachama ktk mgogoro huo?
(e) Je nani yuko sahihi?
Naomba kuwakilisha.
 
ili chama kiendelee kuwa na uhai mbowe ajiuzuru
 
CCM acheni kuwagombanosha viongozi wa CDM, naona mmekamia kweli kuimaloza CDM kupitia JF mwaka huu.
 
Acha uchonganishi,mbona hamtulii kila siku Chadema mara Zitto mara Mbowe
 
Zitto yeye ni CCM B, hata hivyo hawatakiwi kugombana. Ila Zitto akijitoa aende CCM wampe uwaziri itakuwa safi sana.
 
Ungeuliza ni hoja ipi iko sahihi.Pia hoja zinajadiliwa halafu conclusion inakuwa ni ya jumla.Sijui unamaanisha nini
 
Acha uchonganishi,mbona hamtulii kila siku Chadema mara Zitto mara Mbowe

Jibu hoja mwana, mimi ni chadema damu, ila sifurahishwi na malumbano baina hao wawili. Kama wanacdm ni lazima tutafute suluhisho na ikibidi kuwafukuze wote wawili kutoka chama chetu.
 
Tafuta sehemu nyingine tofauti pa kupeleka hiyo ligi yako kwani huko unakopigia ramli wote wako bize Nyanda za Juu Kusini kikazi.
 
Ndugu zangu wajf, baada ya marumbano na minyukano baina ya MBOWE na ZITTO. Sasa naomba mwongozo wenu wanajf kwa kuuliza maswali yafuatayo:-
(a) Nini chanzo cha mgogoro wao!
(b) Mgogoro wao ni kwa maslahi ya nani?
(c) Kwa nini wanarumbana ktk kila kitu?
(d) Nini maslahi ya chama na wanachama ktk mgogoro huo?
(e) Je nani yuko sahihi?
Naomba kuwakilisha.

Kila mtu anajua mumetumwa hapa jamvini kuweka thread inayohusu Zitto na MBowe kama wanamtafaruku kuiaminisha public kwamba kuna mtafaruki nadhani mumechelewa kidogo mungewahi kabla ya uchaguzi
 
Jibu hoja mwana, mimi ni chadema damu, ila sifurahishwi na malumbano baina hao wawili. Kama wanacdm ni lazima tutafute suluhisho na ikibidi kuwafukuze wote wawili kutoka chama chetu.

Tafuta thread humu ndani ya jamvi wenyewe wamekuja hapa wakasema hakuna malumbano kati yao wewe unakuja hapa unaspin kwa manufaa ya chama chako CCM tunakuambia ni very wrong strategy
 
Wakuu hesshma mbele,

Nawomba KUSITA kidogo kujadili thread kama hizi ambazo wala hata neno moja halijaandikua kamav ile kuwakilisha 'nini malumba ya wahusika waliotajwa', wapi ha wapi na juu ya kitu gani ili ndio tukajadili.

Hakuna evidensi yoyote, chanzo kinachonukuliwa basi vurugu tu kwamba CCM kimesema nacho kipate uwakilishi jukwani.

Ungeuliza ni hoja ipi iko sahihi.Pia hoja zinajadiliwa halafu conclusion inakuwa ni ya jumla.Sijui unamaanisha nini
 
Mtandao ambao mbowe anaujenga na wenzake unaoonyesha busara ndogo za mbowe na umesababisha vitendo vya sirisiri ndani ya chadema dhidi ya watu fulani, hii haijengi umoja ndani ya chama.

Busara ndogo za mbowe zinaonekana pale anapofikiria vitendo na maneno ya godbless lema yatakuwa siku zote kwa masilahi ya chadema kwasababu tu ni mmachame mwenzie.

Tukumbuke ni lema huyo huyo ndiye aliyekuja chuo kukuu cha dodoma na kutuhonga ( kutupa rushwa) ili tuandamane kupinga shibuda kuonyesha mtazamo tofauti ndani ya bunge, bahati nzuri wanafunzi wenzetu ambao hawakupata hela walikuwa wakali dhidi ya hili.

Bila ya shaka lema alifanya kitendo hiki bila ya kuwa na upeo wa kujuwa kwamba kinaweza kuchafua jina la chadema na kuharibu umoja ndani na nje ya chama.

Chuo kikuu cha dodoma kina watu wakabila mbalimbali, asifikirie wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma wanaamini mtu ambaye anaweza kutetea masilahi yao ni yule ambaye kazi yake nikusema ndio bwana mkubwa kwa mbowe.

Mimi binafsi naweka imani yangu kwa mwanasiasa mwenye mawazo huru na ambaye hawezi kuburuzwa na mtu au kundi lolote. Najiuliza je hawa watu washawahi kusikia kuhusu joe lieberman wa democratic party aliyeenda kuhutubia katika mkutano wa kuzindua kampeni za republican party na kumpinga mgombea wa chama chake(obama wa democratic party).

Labda mbowe kuna kitu anatakiwa kujifunza kutoka kwa obama au democratic party; obama anaelewa pale kura za chama chake hazitoshi ndani ya bunge mtu ambaye anaweza kumtumia kupata kura za wabunge wa republican ni joe lieberman(shibuda), kwasababu ameonekana mawazo yake yako huru.

Kama kuna mtu yoyote ndani ya chadema ambaye anaweza kushawishi wabunge wa ccm wapige kura za ndio kwajambo ambalo chadema wanataka, basi mtu huyo ni shibuda.


Watu wa shinyanga wametumia uhuru wao vizuri kuchagua mtu ambaye wanamtaka, lakini kuna watu wachache (mbowe na lema) wanataka kuwachagulia watu wa shinyanga kiongozi ambaye kazi yake itakuwa ni kujipendekeza kwa mbowe.

Watu wa shinyanga wanajuwa shibuda anavyojitolea hasa ukizingatia chadema sio chama chenye uwezo kifedha. Tumemuona akitumia muda na hela binafsi kutatua matatizo ya watu wa maswa, iwe siasa (uchaguzi) au uchumi; hapa nazungumzia juhudi binafsi sio za chadema.


Umefika wakati wa kukubali ukweli kwamba mbowe hana sifa wala busara za kujenga chadema imara, bora achaguliwe mtu mwingine (dr. Slaa).

Tukumbuke ukiwa ndani ya chadema sio maana yake wewe sio fisadi, sio maana yake wewe ni msafi. Ukichunguza historia ya mbowe au lema unaweza ukakuta hawana tofauti na rostam azizi.

Lazima tuwe makini nani tunampa madaraka ya kutuongoza. Tusiwape watu ambao wanatafuta nafasi za kufanya ufisadi. Mmesikia kuhusu ufisadi wa magari mitumba chadema.
 
We peter mkali una problem. Rudi darasani ukasome!
 
Watu tutambue uongozi shupavu wa kamanda Mbowe. Amekuwa ni kiongozi mwenye msimamo uliopelekea kukijenga chama kilicho imara na madhubuti.

Kikwazo kikubwa kwa usalama wa taifa, CCM na serikali ktk kukibomoa CDM ni Mbowe, wametumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumshawishi arudi CCM ili wampe hata uwaziri ila mbowe alisimama imara kutetea msimamo wake hii imepelekea CCM kumchukia sana kamanda Mbowe, na wako tayari kufanya lolote ili tu kummaliza wakiamini kwamba wataweza kuisambaratisha CDM.

Leo hii Zitto atueleze utajiri mkubwa alio nao ameupata wapi? Mwaka 2005 alipoenda kugombea ubunge alisaidiwa gari pajero naikumbuka ili kufanikisha ushindi wake, leo hii Zitto anaendesha Hammer na magari mengine ya kifahari.

Mbowe ametumia mali zake ktk kukijenga chama, fuso za music, gari aliyokuwa akitumia Dr Slaa, na magari mengine mengi ndani ya CDM yote ni mali ya Mbowe na siyo CDM.

Anapotaka kukiuzia chama magari ambayo chama chenyewe kimeyachakaza kwa nini aonekane mbaya? Wanajamii mtambue ya kuwa Zitto anatumiwa na kwa hilo hatofanikiwa hata kidogo.

Kanyaga twende makamanda wa ukweli ndani ya CDM.
 
Tuhuma zako kwa Mbowe hakika ni nyingi, ila nataka kukujuza mambo kadhaa kwamba nyumba unayoitetea sasa (cdm) haikujengwa mara moja ilichukua muda mrefu kuijenga na kuinakshi mpaka wewe na wengine wengi wa aina yako mkaiona na kuipenda.

Mjenzi mkuu ni Mbowe na Slaa na huko nyuma hakukuwa na hili tunaloliona leo la Mbowe kukosa busara, haya yote tunayoyaona leo ni matunda ya mafanikio na ndio maana sasa mnatamani kufaidi au kudidimiza mafanikio hayo ila kikwazo ni Mbowe.

Viongozi wa mwanzo (akiwamo Mbowe) walijenga chama kwa fedha zao na rasilimali zao leo wanaonekana hawana busara.
 
Huu mkakati wa kuipiga vita cdm ni mzuri, ila kwa bahati mbaya mmechelewa
 
Watu tutambue uongozi shupavu wa kamanda Mbowe.Amekuwa ni kiongozi mwenye msimamo uliopelekea kukijenga chama kilicho imara na madhubuti. Kikwazo kikubwa kwa usalama wa taifa, CCM na serikali ktk kukibomoa cdm ni Mbowe, wametumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumshawishi arudi CCM ili wampe hata uwaziri ila mbowe alisimama imara kutetea msimamo wake hii imepelekea ccm kumchukia sana kamanda mbowe na wako tayari kufanya lolote ili tu kummaliza wakiamini kwamba wataweza kuisambaratisha cdm.Leo hii Zitto atueleze utajiri mkubwa alio nao ameupata wapi? Mwaka 2005 alipoenda kugombea ubunge alisaidiwa gari pajero naikumbuka ili kufanikisha ushindi wake, leo hii Zitto anaendesha Hammer na magari mengine ya kifahari. Mbowe ametumia mali zake ktk kukijenga chama, fuso za music, gari aliyokuwa akitumia dr slaa, nan magari mengine mengi ndani ya cdm yote ni mali ya mbowe na cyo cdm, anapotaka kukiuzia chama magari ambayo chama chenyewe kimeyachakaza kwa nini aonekane mbaya?Wanajamii mtambue ya kuwa Zitto anatumiwa na kwa hilo hatofanikiwa hata kidogo. Kanyaga twende makamanda wa ukweli ndani ya cdm.

... wewe Kwayu kwenu si pale Nshara, jirani na Mbowe? Kwani lazima uvutie kwako? Hakuna ubishi kwamba Mbowe amefanyia nini CDM. Yapo mazuri mengi zaidi ya uloandika hapa. Yapo mengine ambayo si jukumu langu kuyaandika hapa. Kama ni kweli au majungu hayana nafasi kwani:
Mosi: CDM ni Chama, yaani wanachama wake na sera zake
Pili: Safari ya Ukombozi bado ndefu. The war is still on although some battles have been won. Huko tuendako kunahitaji mtu SAFI zaidi yake.
Tatu: Piga ua, ukwe (in-law wa Mzee Mtei) wake changanya na U-billicanas wake bado ni aspects ambazo kwa nji hii ni tatizo. Vijembe kama, ... mchezesha disko... sio kejeli ndogo kwenye uwanja wa siasa za maji taka. Hapa bado sijaweka ile minong'ono ya msokoto flani ..( jah man!). najua iko siku jamaa flani waweza mlipua vibaya mpaka afanane na kituko cha aina yake. Usione watu kimya.
.
Busara na hekima zingetosheleza kutothubutu kuiuzia CDM magari yale.... wengi hawatelewa kwa maana ya kwamba somo halitopanda. Kiongozi yeye anatakiwa alijue hilo. He should swallow that bitter salt pill instead.
.
.
et al.
 
Hoja ya kumtengua SHIBUDA kuwa mwenyeketi wa SHY hiyo watu wa SHY tumeikataa. SHIBUDA ataendelea kuwa mwenyekiti wetu. Hapo MBOWE kachemsha, tutamchagua tena ktk uchaguzi huru unaofikrika.
 
Mambo ya msokoto ni ya binafsi.Mbona hata mimi natumia kwa sana tu, huko Mara, shinyanga na Mwanza tunatumia kama mboga wewe unashangaa.Tena tunasokota na kutumia baada ya hapo ugali mkuuuuubwa mambo mswano, maana jembe likikamatwa hapo shughuli.Msokoto ni kawaida tu acha jamaa atumie, mbona bungeni wako wengi tu watumiaji???? na maamuzi ya hao jamaa si ya kupinda pinda kama ya Mizengo Pinda.Yaah JAA PEPO
 
Back
Top Bottom