Kati ya hawa wote ni Rais Kaunda tu ambae bado yuko hai

Msingi na msimamo wa rais nyerere wakati ule kuhusu kuunganisha afrika moja ulilenga "kuboresha na kuunganisha jumuiya ndogo ndogo za kikanda(regional integrations) kabla ya kuunda kwa nchi moja ya afrika"

Nyerere alitaka tusirukie moja kwa moja kwa kuanzisha nchi moja ya afrika badala yake tuanze kwa kuunda regional integration kwanza mfano ecowas, EAC, SADC nk.

Msimamo huu ulipingwa sana na Dr Nkrumah mwaka 1963 yeye alitaka twende moja kwa moja kuanzishwa kwa united state of Africa(Taifa moja la africa)

Nkrumah walivutana sana kwa hoja na Nyerere kuhusu misimamo yao hii.
Out of the topic, hivi umesgaona Katina ya Conversion People’s Party chama cha Nkurumah?
TANU waliibdba ilivyo ni copy and paste.
 
Baada ya kutoka madarakani Chiluba alimfunga Kaunda, Nyerere alikwenda kumsalimia gerezani na ali lobby atolewe.
Tarehe 30 Dec 1997 Nyerere alifunga safari hadi lusaka gerezani kwa swahiba wake mzee kaunda na hii ilitokana na kupata habari kuwa swahiba wake huyu alikataa kula kwa masiku kadhaa.

Ndio mwalimu apofunga safari hadi gerezani kwenda kumbeleza mzee kaunda ale chakula na kuiambia serikali ya chiluba imtoe Dr kaunda.

Kwa mapenzi na urafiki wao mzee kaunda hakuweza kukataa ombi la rafiki yake huyu(Nyerere) na kukubali kula, walikunywa pamoja juice ya machungwa gerezani na kumaliza mgomo wa kula.

Baada ya ziara hii ya mwalimu siku ile ya 30/12/1997 na kuipa msukumo wa hali ya juu serikali ya chiluba kumwachia mzee kaunda, ilimbidi chiluba aite baraza la mawaziri usiku wake na kutangaza kumwachia huru mzee kaunda usiku wa mkesha wa mwaka mpya 1998.
 
Mwenye story ya kaunda na nyerere kwenye party ulaya anambie hapa huwa nasikia nusu nusu.
 
Tarehe 30 Dec 1997 Nyerere alifunga safari hadi lusaka gerezani kwa swahiba wake mzee kaunda na hii ilitokana na kupata habari kuwa swahiba wake huyu alikataa kula kwa masiku kadhaa.

Ndio mwalimu apofunga safari hadi gerezani kwenda kumbeleza mzee kaunda ale chakula na kuiambia serikali ya chiluba imtoe Dr kaunda.

Kwa mapenzi na urafiki wao mzee kaunda hakuweza kukataa ombi la rafiki yake huyu(Nyerere) na kukubali kula, walikunywa pamoja juice ya machungwa gerezani na kumaliza mgomo wa kula.

Baada ya ziara hii ya mwalimu siku ile ya 30/12/1997 na kuipa msukumo wa hali ya juu serikali ya chiluba kumwachia mzee kaunda, ilimbidi chiluba aite baraza la mawaziri usiku wake na kutangaza kumwachia huru mzee kaunda usiku wa mkesha wa mwaka mpya 1998.
Aliwekwa ndani kwa kosa gani?
na kwa Nini alitoka madarakan??
 
View attachment 1028590

Mstari wa nyuma kuanzia kushoto nimemtambua Obote, Nyerere, na Kaunda

Mstari wa mbele kutoka kushoto Bokhasa, Haile Selassie , Kenyatta na Mobutu

Wengine ninaomba msaada.

Ninafahamu hapo yupo Augustino Neto wa Angola,
Conclusion yako nimeipenda...unawafahamu sita lakini una uhakika kabaki mmoja tu!!!
 
Aliwekwa ndani kwa kosa gani?
na kwa Nini alitoka madarakan??
Aliwekwa ndani na serikali ya chiluba kwa kuhusishwa na jaribio la kupindua serilali ya marehemu chiluba.

Alitoka madarakani baada ya kushindwa na chiluba kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka1991.
 
Ni kweli Nyerere kuamua siasa za ujamaa kuliwakera wazungu. Lakini kwanini sisi vijana tusisimame na kupinga kauli ya wazungu?
Ni sawa mama ulichoongea kwa sisi vijana kuwapinga wazungu. Hapo kuna ufafanuzi mrefu sana. 1. Kwanza unaanzia kwa nchi zetu tu wenyewe kutofautiana sera kisiasa. Utakuta mfano Tz tunamkumbatia labda mchina. Na labda Zimbabwe wanamkumbatia marekani,kwa hiyo inakuwa vigumu kuungana pamoja na kuwa na sauti moja,ksbb tu wenyewe tu tayari tumeshagawanyika huyu yuko huko na huyu huko. Na wazungu wajanja sana hawataki tuungane ndio maana wanatumia nguvu kubwa kutugawa,hasa kwa kutumia mgongo wa misaada. Bila uzee kuja kwa kasi wale wazee wetu,Nyerere,Nkuruma,walikuwa na uwezo mkubwa wa kukubarika,hawa wangewalisha siasa hizo akina Mghabe,Sankara RIP,. Sasa hivi vijana wa siku hizi hata akiwa kwenye uongozi anaangalia tumbo lake tu na ndugu zake,ndipo tulipofikia,kwa hiyo dada nikikujibu swali lako ni kwamba huwezi kumwambia kijana wa siku hizi mkaungane kupigania maslahi ya vijana wenzetu wanaoteseka labda somalia. Anaangalia tumbo lake tu. Na huko mbele tunakoelekea tutapigana sana wenyewe kwa wenyewe kwa maslahi ya wazungu. Nyerere "UJIULIZE UTAIFANYIA NINI NCHI,SIO NCHI YAKO ITAKUFANYIA NINI”. Na ndiko tulikofikia kila kijana anapoajiliwa mahala jambo la kwanza hii ofisi itanisaidia vipi niwe na hiki na kile? Inaumiza sana
 
The Africans, by David Lamb!
Wote hao wameziacha nchi zao katka lindi la ufukara! Walikuwa wanafanya nini? Picha hii imenifikirisha sana! Nimelinganisha nchi yetu na vinchi vidogo kama Switzerland, Dennark, Sweden etc. Sisi au hawa waleta "uhuru" walifail wapi, sasabu za kufail ni zipi?
Hawa wote walikuwa wanahimiza nadharia za kisiasa za KiFabians, yaani ujamaa na ukomunist, ambazo kiuhalisia ni njia za kuwafanya wananchi kuwa masikini na walioko madarakani kuwa peponi. Ujamaa naturally sio ya kibinadamu. Inner circle ya lengo, ni kuweza kwatawala watu wanavyotaka. Tunashukuru wamekufa, maana hata wao wameua sana watu waliowapinga, ili tu theory zao zisimame..
 
Dhana ya ujamaa ilianzia Eastern Europe kwa wakina Max na Lenin. Ni baada ya kuona pengo kati ya matajiri na masikini ni kubwa sana. Fahamu tu kuwa moja ya biashara zilizotajirisha sana wazungu ilikua biashara ya utumwawna na baadae kilimo cha biashara.

Wazo la ujamaa ilikua kugawana utajiri na wote kuishi sawa. Western Europe walilipinga sana wazo hilo. Baada ya mali kukusanywa kwaajili ya wote, viongozi W aliingia tamaa ya kujimilikisha.
 
asante sana! Kama sasa hivi China na Urusi walivyo bado na nadhalia za Fabians! Na kweli China wameweka kutawala milele. Hivyo hivyo Urusi, Putin ni defacto life ruler
 
Dhana ya ujamaa ilianzia Eastern Europe kwa wakina Max na Lenin. Ni baada ya kuona pengo kati ya matajiri na masikini ni kubwa sana. Fahamu tu kuwa moja ya biashara zilizotajirisha sana wazungu ilikua biashara ya utumwawna na baadae kilimo cha biashara.

Wazo la ujamaa ilikua kugawana utajiri na wote kuishi sawa. Western Europe walilipinga sana wazo hilo. Baada ya mali kukusanywa kwaajili ya wote, viongozi W aliingia tamaa ya kujimilikisha.
Manifesto ya ki soshalist haikuanzia kwa kina Max na Lenin, hao walifundishwa na Fabian SOCIETY.
Tafuta kitabu kinaitwa
"The creature from Jeckly's Island" kimeeleza mengi.
 
The Africans, by David Lamb!
Wote hao wameziacha nchi zao katka lindi la ufukara! Walikuwa wanafanya nini? Picha hii imenifikirisha sana! Nimelinganisha nchi yetu na vinchi vidogo kama Switzerland, Dennark, Sweden etc. Sisi au hawa waleta "uhuru" walifail wapi, sasabu za kufail ni zipi?

sababu ni kuwa immediate from colonialism era
 
Vision ya Nyerere ilikuwa kuingunisha Afrika kama muungano wa North America. Aliona umoja ndiyo utakaoleta maendeleo.

Alitumia resources nyingi katika ukombozi wa bara la Afrika. Siasa za ujamaa hazikuleta tija pia vita ya Kagera iliturudisha nyuma sana.

Jamaa kachangia kwa asilimia kubwa sisi kuwa maskini.

Alishindwa kuleta maendeleo Tanzania ya Africa nzima angeweza vipi
 
Kiukweli sijaona kama Nyerere Afrika,ni vile uzee unakuja kwa kasi na kunyang'anya uongozi kabla hajaweka sawa fikra zake. Eti Mandera ndio nembo ya Afrika? Wizi mtupu. Hakuna kama Nyerere Afrika nzima. Ni vile tu wazungu walikuwa hawamtaki Nyerere,na wamejitahidi kufifisha historia njema yako iliyotukuka. Badala yake wamemkweza Mandela kwa kitendo chake kimoja tu kukubariana nao. Lakini Nyerere kaifanyia makubwa sana Afrika nzima kuliko kiongozi yoyote Afrika

Sent using Jamii Forums mobile app

emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
 
Back
Top Bottom