kati ya hawa nani mkali?....na kwa nini?

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka watu wenye kutathmini soka la Ulaya ktk vituo mbalimbali vya Luninga hapa nchini.

na kila kukicha wanaibuka na inaaminika wataibuka wengine kadha wa kadha wenye kujua kutathmini na kuelezea soka la ulaya.

Uzuri ni kuwa kutathmini soka haijalishi kuwa ulicheza mchezo huo au la...

Kilichonipelekea kuanzisha mada hii ni hali ya ubishi niliokumbana nayo kitaa mara kadhaa, watu wamekuwa wakibishana na kila mmoja kuvutia upande wake
Wengine wakisema Dr LICKY ABDALLAH
Wengine wakimtaja SHAFII DAUDA
Na Hata wengine wakionekana kumkubali EDO KUMWEMBE.

je kwa wewe mwana JF unayefuatilia soka la ulaya kuliko la hapa una mtazamo gani?
Je ni nani anayetathmini kwa kina soka na anajua kueleza makosa, kueleza aina ya mchezo wa timu husika, anayejuwa mapungufu ya vikosi husika, mwenye DATA za ukweli, mwenye breaking newz, mwenye hadithi za kale zenye radha na msisimko?....nk nk nk nk
 
Wote Wakali tofauti ni asilimia. Hivyo kwa mtazamo wangu DR Licky Abdalala Namkubali Zaidi





TUWE MACHO 2010 TUSIRUDIE KUCHAGUA MAKAPI YALEYALE ! Waswahili walisema majuto mjukuu
 
Nashauri uombe mod akuwekee kitufe cha kupiga kura ili tubofye, kama opinion vote nyingine. Vinginevyo tutaanza kukutajia na majina ambayo hukuweka kwenye orodha yako kama vile Mgombea ubunge we Mwibara, Cyprian Musiba.

Kwangu Liky hana mpinzani. Kiwango chake na uelewa wake uko juuu sana.
 
Nashauri uombe mod akuwekee kitufe cha kupiga kura ili tubofye, kama opinion vote nyingine. Vinginevyo tutaanza kukutajia na majina ambayo hukuweka kwenye orodha yako kama vile Mgombea ubunge we Mwibara, Cyprian Musiba.

Kwangu Liky hana mpinzani. Kiwango chake na uelewa wake uko juuu sana.

Huyo Musiba hana lolote analojuwa.
Yeye akiambiwa atoe tathmini ya mechi basi anapita kulekule alikopita Dr Licky then anaanza kutaja marafiki zake ''eeh ndugu yangu Barantanda wa JF sijui anahali gani huki aliko, maana mpaka Arsenal chama lake wako nyuma''...huyo ndo Musiba.
 
Huyo Musiba hana lolote analojuwa.
Yeye akiambiwa atoe tathmini ya mechi basi anapita kulekule alikopita Dr Licky then anaanza kutaja marafiki zake ''eeh ndugu yangu Barantanda wa JF sijui anahali gani huki aliko, maana mpaka Arsenal chama lake wako nyuma''...huyo ndo Musiba.
Kweli mkuu huyo Musiba akiwa anacomment kila mara utaskia akisema 'PENETRATION PASS' hakuna anachokijuwa zaidi ya penetration pass.
Anyway Dr. Licky ni mkali.
 
Dakta Licky mwisho wa reli.....nazimia sana uchambuzi wake tokea miaka ile katikati ya tisini...94,95,96......
 
Dr Ricky mkongwe, hao wengine wamekuja juzi tu, msifananishe kabisa na hao vijana, Dr anachambua si masihara mpaka kule usukuma walipendekeza apewe Timu ya Taifa..!! SI MCHEZO ATIII...!!
RICKY BAB KUBWA.
 
wachambuzi waliowachambua wachambuzi hao wa soka wamesema kuwa...

''Dr Licky''
Ni mzuri kwa hadithi, ana rafudhi nzuri inayovutia ktk hadithi.
Anajuwa kuchambua soka kiundani, hana mapenzi, na mwenye kutegemea sana hadithi na matukio ya nyuma.
Mara nyingi huwa anasubiri mpira uishe then anatoa uchambuzi.

''Shafii Dauda''
Anapita mulemule kwa Dr.
Anatumia sana hadithi za kale, anajua kuuchambua mpira ktk kila point husika.
Anayaona mapungufu na si mkurupukaji.
Naye pia husubiri mpira uishe ili atoe tathmini.

Akiendelea vizuri atakuwa mrithi wa Dr.

''Edo Kumwembe''
Anajitahidi, lakini bado sana.
Ameachwa umbali sawa na kutoka ardhini mpaka Mbinguni na Dr Licky.
Ni mkurupukaji asiyehitaji kusubiri mpira uishe na hawezi kuuacha mpira 50/50.

Yeye mara zote hutoa final result wakati mechi inapokuwa half tym na kisha mechi inapokuwa imekwisha akiulizwa vp mbona mechi imekwenda tofauti na ulivyosema yeye hubaki anajiuma uma.

kwa hilo watu wamemsifia kwa kipaji chake cha kutokuwa na haya.
Anaweka wazi sana mapenzi yake kwa Arsenal na vilabu vya England.

Na anasahau kabisa kuwa timu ya taifa ya England wala vilabu vyake havina rekodi ktk soka la Ulaya.
 
Umewasahau Chacha Maginga na Issa Michuzi ambao wakianza kumkatisha Dr Ricky(ambaye he is so down to earth hata anawasikiliza tu) maana yake tafuta mahali remote ilipo
 
Dr. Licky ni mkali zaidi hasa anapoingiza na mambo ya historia ya mji, kiwanja au mchezaji huwa inaleta ladha sana. Na kuna mwingine Rishard Adolf yeye mara nyingi huwa katika maswala ya kiufundi zaidi. Bila kumsahau Ally Mayai Tembele.
 
Back
Top Bottom