Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,144
- 166,077
FIFA imepanga kuunda kampuni mpya ya kibiashara iitwayo FIFA Forward Enterprise, yenye thamani ya takribani $20 Bilioni (karibu TZS Trilioni 50) kisha itauza 20% ya hisa za kampuni hiyo kwa wawekezaji binafsi ikiwemo kampuni ya uwekezaji Thrive Eternal na benki ya J.P. Morgan.
Kupitia mpango huo kila chama cha soka (kati ya vyama 211 vilivyopo) kitapokea $40 Milioni (Kama Bilioni 100) kwa kipindi cha miaka mitatu 2027–2030 kisha $8 Milioni kila mwaka (sawa na TZS 20 Bilioni).
Mpango huo umepigwa vikali na mashirikisho matatu ya soka ambayo ni Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), Shirikisho la Soka Amerika Kaskazini, Kati na Carebean (CONCACAF) na Shirikisho la Soka Amerika Kusini (CONMEBOL). UEFA imetoa msimamo mkali kupinga mpango huo ikisema "FIFA is not for sale" na kutishia kujitoa FIFA ikiwa haitabadili mpango huo.
Kati ya mashirikisho 6 ya soka duniani yanayounda FIFA, mashirikisho matatu tayari yametoa msimamo wa kupinga mpango huo. Mashirikisho mengine matatu yapo kimya yanasubiri. Mashirikisho hayo ni Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Shirikisho la Soka Asia (AFC) na Shirikisho la Soka Oceania (OFC).
Ukiangalia vizuri hapa utakumbuka ile kauli ya wahenga kwamba maskini hana kauli. Mashirikisho matatu yaliyotangaza msimamo wa kupinga mpango huo wa FIFA ni yale yanayojiweza (Ulaya na Amerika). Na mashirikisho ambayo yamekaa kimya ni ya nchi maskini (Afrika, Asia na Oceania).
Kwa wale msiojua Oceania ni vile visiwa vidogo hapo Pacific kama Fiji, Tuvalu, Kiribati, Vanuatu n.k. Ni nchi maskini sana na ndogo kieneo. Nchi moja inaweza kuwa sawa na kata ya Dumila 😂. Nchi pekee yenye afadhali huko Oceania ni New Zealand. Lakini wengine wote wapo hoi.
Sasa hao Oceania wameungana na maskini wenzao wa Afrika na Asia kupiga kimya. Ikumbukwe kwa sasa FIFA inatoa $10 (Kama TZS Bilioni 25) kwa kila mwanachama kwa miaka mitatu kwa ajili ya maendeleo ya soka. Hii ni sawa na TZS Bilioni 8 kwa mwaka.
Sasa ikiwa FIFA itafanikiwa katika mpango wake wa kuuza hisa, wanachama watapata kwa mkupuo $40 Milioni (Kama Bilioni 100) ndani ya miaka mitatu, kisha wataanza kupokea $8 Milioni kila mwaka (sawa na TZS 20 Bilioni).
Sasa nchi maskini zinaona kabisa hiyo ni fursa ya kupiga hela. Kutoka kupata TZS Bilioni 8 kwa mwaka hadi Bilioni 20 kwa mwaka sio jambo dogo. Hiyo ndiyo sababu imefanya wakae kimya.
Ama kweli ukiwa maskini wa kipato unakuwa hadi maskini wa akili. Ulaya, na Amerika wameshatoa msimamo. Sisi tunaogopa kutoa msimamo ili tusipoteze hela. What a shame?
UEFA inasema ikiwa FIFA itaunda kampuni ya kibiashara itakuwa imetoka kwenye misingi yake kwa sababu FIFA ni shirikisho lisilojiendesha kwa faida (Non-profit organization).
Pili UEFA inasema FIFA ikiendelea na mpango wake wa kuuza hisa itapoteza udhibiti wa Kombe la Dunia, kwa sababu watakaonunua hisa watakuwa na uwezo wa kuathiri michuano ya Kombe la Dunia. Pia wanasema ni kuingiza maslahi ya kibiashara kwenye maamuzi ya michezo, na hiyo itadhoofisha uhalali wa FIFA kama chombo cha kimataifa cha umma.!