Katazo la mtoto kucheza kamari

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
Michezo yote ya kubahatisha (kamari) ikiwemo betting, slot machines inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya Michezo ya Kubahatisha namba 4 ya mwaka 2003 sura ya 41 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Lakini, ifahamike kwamba mtoto haruhusiwi kucheza kamari ya aina yoyote.

Mtu yeyote atakaye ruhusu mtoto chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia, kukaa au kuzururazurura karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha (kamari) anahesabiwa kufanya kosa.

Mtu huyo anastahiri adhabu ya kulipa faini ya kiasi kisichopungua shilingi milioni moja (1mil.) na kisichozidi milioni tano (5mil.) au kifungo kisichozidi miezi 12 (mwaka 1) au vyote kwa pamoja faini na kifungo.

Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 70 cha Sheria ya Michezo ya Kubahatisha kama ilivyotajwa hapo juu.

Pia kifungu cha 47 cha sheria hiyo tajwa hapo juu kinamzuia mwendesha kamari kuuza au kutoa ticket au nafasi ya kushiriki mchezo wa bahati nasibu kwa mtoto chini ya miaka 18.
Kufanya hivyo ni kosa na adhabu yake ni shilingi laki tatu au kifungo cha miezi mitatu au vyote kwa pamoja.


Hivyo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla tukemee vitendo hivyo kwa watoto kwani;
-kamari inaathiri saikolojia ya mtoto kutaka kupata mafaniko kirahisi.

👉Pia inaathiri ushiriki mzuri wa mtoto shuleni na

👉kuchochea zaidi vitendo vya kiarifu kwa watoto kama vile wizi, ukabaji, ugomvi na wengine kufikia hata kuuana kwasababu ya kamari.

Hata wewe mtu mzima usitegemee kamari kama ndio nyenzo kuu ya uchumi. Mafanikio hayaji kwa kubahatisha.

It's me
A Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis
0713736006
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom