KATANGA: Je, ni tamaa ya hazina dhidi ya Uzalendo?

Mkuu ahsante kwa kunialika, kwanza Heri ya Eid Mubarak

Nimepitia mada hakika iko vzr km kawaida yako Mkuu kwa mada na hoja za akili

Naona maoni ya wengi waliochangia hawapo mbali na uhalisia wa kile walichosema
Mkuu Happy Eid,

Shukrani kwa kutia timu. Hiyo bold hapo unaweza kuiweka Sawa.

Je mkuu kuna faida gani ya kumfukuza mwizi alafu ukaingia kuiba ww?
 
Pdf zinagoma ku upload ila google document zifuatazo.

1. Conflict of Interests or Interests in
Conflict? Diamonds & War in the DRC by Ingrid Samset.

2. The great African war - P. Rentyjens

3.Africa's world war By Gerard prunier
Unaweza kukisoma bure humu
Africa's world war : Congo, the Rwandan genocide, and the making of a continental catastrophe : Prunier, Gérard, author : Free Download, Borrow, and Streaming : Internet Archive

Article 1. War turns commercial

2. Congo’s hidden war

Pia ripoti juu ya Katanga
Nchi zote zinazoizunguka DRC zinanufaika na raslimali za DRC kwa mgongo wa waasi hasa hasa mashariki mwa Congo Rwanda na Uganda kuna wakati zinapigana zenyewe kwa zenyewe ndani ya nchi ya DRC ili ziwe na udhibiti wa raslimali zinazopatikana.

DRC yenye amani haitakuwepo kama Rais Museven na Kagame wataendelea kuwa madarakani katika nchi zao, ukiangalia kwa makini unagundua kwamba makundi ya waasi nchini Congo hayaibuki kutokana na political differences zao wenyewe badala yake yamekuwa yakichangiwa kwa kiwango kikubwa sana na external forces.

Kuhusu hoja ya ushiriki wa Zimbabwe na Angola katika vita hiyo inachangiwa sana na kuisaidia Congo isiwe chini ya udhibiti wa Rwanda lakini wakati huo huo mataifa hayo yalizingatia Geopolitical interests zao katika Congo, kumbuka iwapo Waasi wa Rwanda wangeweza kufanikiwa kudhibiti jimbo la Katanga wangekuwa wamefanikiwa kwenye mambo makuu mawili.
1 kuwa na udhibiti mkubwa wa DRC maana kuanzia kivu mpaka Katanga.
2 kuwa na udhibiti wa kitovu cha raslimali ambazo ziko jimbo la Katanga.
mambo hayo kwa ujumla yangewawezesha kuwa na udhibiti wa DRC kisiasa na kiuchumi hivyo wangeweza kupata nguvu ya ziada na kuiondoa madarakani serikali ya DRC. hali hiyo isingekuwa threat kwa DRC pekee bali ingekuwa threat kwa mataifa yote hayo mawili kumbuka Angola alikuwa akipambana na waasi kule Cabinda.

jambo jingine lililochangia ushirika wa nchi hizo ni unufaika na raslimali za DRC ni rahisi zaidi kuvuna raslimali za nchi husika inapokuwa vitani kuliko ikiwa katika hali ya amani hivyo ndiyo maana Zimbabwe na Angola ziliipokea fursa hiyo kwa mikono miwili.

alaah sijaambatanisha vielelezo vya ushahidi kwa sababu ya uharaka tu.
 
Mkuu ina maana siku yakitokea mabadiliko ya uongozi ngazi ya Urais kwa hizi nchi mbili (Rwanda na Uganda) huenda eneo la DRC Mashariki likatulia?
 
Japo kwa sasa kumekuwa na detente katika eneo la mashariki mwa DRC.

Huenda wanavuna kwa uhuru na makundi ya ndani ya Congo yameceasefire.
 
Eneo la maziwa makuu kuna uwezekano mkubwa sana kama uongozi mpya hautakuwa na maslahi na congo.
Lakini mkuu tatizo kubwa ni nchi jirani tu au hata siasa za ndani ya DRC?

Maana makundi kama Mai Mai walioko huko mashariki au wale Kamwene Nsapu kule Kasai utasema ni nchi jirani au siasa za ndani zinachangia?

Huoni kama kuna muda tunazibebesha hizi nchi jirani lawama wasizohusika nazo?
 
DRC ina mfumo dhaifu sana wa siasa za ndani na ina mfumo dhaifu sana wa kijeshi hivyo any foreign intrusion itapata support kubwa kutoka ndani pia.

Jambo la pili siasa za Congo nchi jirani hasa za mashariki mwa congo zinainfluence kubwa sana za nani aingie madarakani na nani asiingie ukiangalia karibu marais wote wa Congo wa wameingia kwa mapinduzi ambayo kwa namna moja au nyingine yalikuwa na mkono wa mataifa ya nje.

Ni kweli kuna makundi mengine Congo yanaibuka kutokana na siasa za ndani zenyewe ila makundi threat kwa Congo yana mkono wa hayo mataifa niliyoyataja.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwamba makundi 'threat' kwa Drc ni yale yenye kuungwa mkono na haya mataifa mawili.

Ila mkuu huoni hili swala lina pande mbili yaani hata DRC inaonekana 'threat' kwa haya mataifa maana imehifadhi wapiganaji ndani ya ardhi yake wanaopinga serikali za haya mataifa mfano FDLR wanaompinga Kagame na tena inasemekana walihusika na mauaji huko Rwanda na ADF wanaompinga Museveni tena inasemekana wana itikadi kali za kidini?

Na pia kwa nini haya mataifa mawili (Rwanda na Uganda) yanayopakana na Drc mashariki yananyooshewa kidole pale vuruga zinapoongezeka huko kivu? ila nchi nyingine zenye mpaka mkubwa na Drc hazishutumiwi mfano Angola ambayo imepakana na jimbo la Kasai ambalo wakati limekumbwa na vuruga Angola haikunyooshewa kidole.
 
Aisee. Mada nzuri ila nina swali nje kidogo.
Nimeyasoma mataifa kibao hapo yakihusishwa moja kwa moja kwenye mgogoro wa Drc na mengi tu toka EAC.
Lakin kila napokutana na hiz habari,sijawah kuona mahala popote ambapo TZ (na kenya pia) wanatajwa kujihusisha na mgogoro wa cngo (weka mbali ulinzi wa amani kupitia Monusco).

Je nchi hiz,hasa Tz, ni wema sana kias kwamba hawana interest za kujihusisha nazo huko Drc? Yan hatupo popote palee au ndio mambo yetu sis na involvement yetu huko ni one of CLASSIFIED operations kias hicho hata isifahamike wala kuongelewa kama wanavo appear rwanda na uganda zaid zaid.?
 
Hahahaha ,swali zuri Mkuu
Lkn si unajua Mzee Kabila na baadhi ya timu yake walitokea wapi ?

OK ngoja wengine watusaidie vzr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ofcz mkuu.Lakin htuonekan kuwa front kwenye harakat za kumuweka pale na ndo maana kuna mahala inasemekna ni kagame alimuweka akishirikiana na wadau wengine..
Au sis tunachora michoro tu mengine tunawaachia wao?
 
Aisee. Mada nzuri ila nina swali nje kidogo.
Nimeyasoma mataifa kibao hapo yakihusishwa moja kwa moja kwenye mgogoro wa Drc na mengi tu toka EAC.
Lakin kila napokutana na hiz habari,sijawah kuona mahala popote ambapo TZ (na kenya pia) wanatajwa kujihusisha na mgogoro wa cngo (weka mbali ulinzi wa amani kupitia Monusco).

Je nchi hiz,hasa Tz, ni wema sana kias kwamba hawana interest za kujihusisha nazo huko Drc? Yan hatupo popote palee au ndio mambo yetu sis na involvement yetu huko ni one of CLASSIFIED operations kias hicho hata isifahamike wala kuongelewa kama wanavo appear rwanda na uganda zaid zaid.?
Mkuu kama alivyosema mtu chake hapo je unajua hao players wote wa mgogoro yaani kabila,kagame na museveni wametokea wapi??

Kiukweli Mwl Nyerere alikua bingwa wa foreign policy, na hata huyo Kagame na Museveni walikuwa trained na jeshi letu kule Monduli. Wakatoka hapo wakapewa support na Nyerere wakarudi Uganda na baadae kumpindua Gen Okello.

Movement hiyo hiyo ambayo ni zao la Tanzania lilielekea Rwanda na likapindua serikali ya huko, ikumbukwe ndege ilitunguliwa ikitokea Tz!!

Haya baada ya kuiteka Rwanda hao watoto wa Nyerere wakashirikiana na zao Jingine la huku Bongo, Laurent Desire Kabila kwenda kuikamata Kinshasa kupitia kikundi walichokiita AFDL.

Nakumbuka hata kiongozi wa RCD-Goma kma sikosei anaitwa Wamba Dia Wamba iliotaka kumpindua Kabila kwenye second Congo war kwa support ya majeshi ya Rwanda na UG alikua ana command akitokea hapa Dar!!

Kiufupi naweza kusema Nchi tatu zote ziliongozwa na zao la Tanzania. Hapo achilia mbali influence ya Tz huko Burundi.

Nyerere alikua master mkuu, ila sijui tulikwama wapi hapo kati.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwamba makundi 'threat' kwa Drc ni yale yenye kuungwa mkono na haya mataifa mawili.

Ila mkuu huoni hili swala lina pande mbili yaani hata DRC inaonekana 'threat' kwa haya mataifa maana imehifadhi wapiganaji ndani ya ardhi yake wanaopinga serikali za haya mataifa mfano FDLR wanaompinga Kagame na tena inasemekana walihusika na mauaji huko Rwanda na ADF wanaompinga Museveni tena inasemekana wana itikadi kali za kidini?

Na pia kwa nini haya mataifa mawili (Rwanda na Uganda) yanayopakana na Drc mashariki yananyooshewa kidole pale vuruga zinapoongezeka huko kivu? ila nchi nyingine zenye mpaka mkubwa na Drc hazishutumiwi mfano Angola ambayo imepakana na jimbo la Kasai ambalo wakati limekumbwa na vuruga Angola haikunyooshewa kidole.
Mkuu labda na mimi nichangie.

Kwa maoni yangu naona external influence ya nchi jirani ndio inaharibu amani ya DRC kuliko matatizo ya ndani. Nasema hivo sababu ukiangalia makundi ya ndani mengi yameanzishwa kwa ku align na taifa fulani.

Nakumbuka walipotaka kumpindua Kabila mkubwa, ilisemekana wananchi wa kivu wamemchoka. Lakini hao Banyamulenge ambao Kagame alidai kwenda kuwasaidia nao walimpinga wakawa na jeshi lao parallel na RCD Goma. Hta hao CNDD walipewa silaha na Angola ili wakazui majeshi ya Burundi kuvuka mpaka, hao FDLR nao walipewa silaha na pesa kutoka kinshasa wapambane huko Kivu.

Kwahiyo utaona makundi hayo sio kwamba yanashadadia internal conflicts bali yanashinikizwa na mataifa ya nje. Mfano MLC mpaka walipelekwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kuokoa serikali,RCD walipelekwa kupambana na majeshi ya Chad n.k

Kuhusu Angola kutohusishwa ni sababu hawana imperialistic agenda kma ya hao majirani wa mashariki. Kagame na mwenzie wako ambitious sana kutafuta madaraka sababu wanajua wakipatikana majirani hostile basi watapoteza utawala wao. Pia sababu inaweza kuwa ardhi, eneo la Ug na Rwanda lina population density kubwa sana kuliko Angola hivyo kuivamia DRC ni njia mojawapo ya ''kuitanua'' nchi yao maana kulikua na mpango wa kuifanya kivu ijitenge na DRC!!

Sababu nyingine ni mali maana nchi zao hazina rasilimali za kutosha kulinganisha na Angola!! na ndio maana kuna kitabu wanaitwa "Soldiers without borders"!! Yaani wanasaka fursa kokote. Licha ya Ug na Rwanda kutokuwa na rasilimali ila waliwahi kuwa exporters wakubwa wa Almasi na dhahabu!!! Ila nadhani Angola walau wana rasilimali kuzidi hao wawili otherwise nao wangekuwa kila siku wanaivamia DRC kwa kigezo cha kwamba wanasaka waasi wa UNITA!! Ili tu wapore rasilimali.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwamba makundi 'threat' kwa Drc ni yale yenye kuungwa mkono na haya mataifa mawili.

Ila mkuu huoni hili swala lina pande mbili yaani hata DRC inaonekana 'threat' kwa haya mataifa maana imehifadhi wapiganaji ndani ya ardhi yake wanaopinga serikali za haya mataifa mfano FDLR wanaompinga Kagame na tena inasemekana walihusika na mauaji huko Rwanda na ADF wanaompinga Museveni tena inasemekana wana itikadi kali za kidini?

Na pia kwa nini haya mataifa mawili (Rwanda na Uganda) yanayopakana na Drc mashariki yananyooshewa kidole pale vuruga zinapoongezeka huko kivu? ila nchi nyingine zenye mpaka mkubwa na Drc hazishutumiwi mfano Angola ambayo imepakana na jimbo la Kasai ambalo wakati limekumbwa na vuruga Angola haikunyooshewa kidole.
Mkuu ni kweli kwamba misitu ya Congo ni maficho mazuri sana ya waasi wote wanaofurushwa kutoka huko mataifa ya Uganda na Rwanda lakini hili linachangiwa sana na udhaifu wa kijeshi wa Congo na siyo support ya Congo kwa waasi hao.

pili Nchi za Rwanda na Uganda ushiriki wake katika kuvuruga Congo ni kwa lengo la kupanua wigo wa kuweza kuvuna mali za Congo kupitia mgongo wa waasi rejea kisa cha Rwanda kurejesha zaidi ya Tani 80 za madini ya Cobalt yaliyokuwa yamevunwa kutoka Congo mwka 2014 kama kumbukumbu zangu ziko sawasawa.

kwanini mataifa haya mawili yamekuwa yakinyooshewa vidole sana kuliko mataifa mengine ? sababu kubwa sana ni kwamba makundi mengi ya kigaidi yamekuwa na affiliation ya moja kwa moja kutoka kwenye mataifa hayo kuliko nchi nyingine zinazoizunguka Congo hata huko jimbo la Kasai Angola hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja kuyahusisha makundi hayo na Angola.

kumbuka pia ujirani wa mataifa ya Rwanda, Congo na Uganda ni ujirani wa kuviziana,
 
Back
Top Bottom