Kazi ya MONUSCO ni kulinda Amani au kuisadia Congo dhidi ya M23?

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,614
15,942
Nashindwa kuelewa tunaambiwa vikosi vya umoja wa mataifa MONUSCO pamoja na SADC kazi yao ni kulinda amani huko mashariki ya DRC lakini kazi wanayoifanya ni kusaidia vikosi vya serikali ya Congo kupambana na M23.

Je kuna uhalali kuendelea kuwepo kwa vikosi hivyo vya kimataifa katika ardhi ya Congo?

Nadhani wakati umefika sasa Umoja wa mataifa na SADC kuondoa majeshi yao kwakua jukumu walilopewa wameshindwa kulifanya kinachoendelea huko kwa sasa ni uhuni mtupu au wao ndio wezi wa madini ya Congo?
 
20240220_153356.jpg
 
Nashindwa kuelewa tunaambiwa vikosi vya umoja wa mataifa MONUSCO pamoja na SADC kazi yao ni kulinda amani huko mashariki ya DRC lakini kazi wanayoifanya...
ingekuwa kazi yao sio kupigana wasingeenda na bunduki, wangeenda na virungu vya kimasai tu. na kama wao wanashambuliwa, mfano juzi ile askari wa south 2 waliuawa, na silaha wanazo, kwanini wasizitumie?
 
Nashindwa kuelewa tunaambiwa vikosi vya umoja wa mataifa MONUSCO pamoja na SADC kazi yao ni kulinda amani huko mashariki ya DRC lakini kazi wanayoifanya ni kusaidia vikosi vya serikali ya Congo kupambana na M23...
Monusco kuna peacekeeping na force intervation brigade(FBI) ambayo Tanzania, South africa na Malawi ilikuwa kwenye hiyo FIB 2013 unahusika moja kwa moja na kumshambulia adui.

Huko Congo mission zilizopo ni za peace forcing sudan ndio kuna peacekeeping.
 
ingekuwa kazi yao sio kupigana wasingeenda na bunduki,wangeenda na virungu vya kimasai tu. na kama wao wanashambuliwa, mfano juzi ile askari wa south 2 waliuawa, na silaha wanazo, kwanini wasizitumie?
Nenda kasome majukumu yao halafu urudi tena hapa mkuu. Raia wanateseka kwa upumbavu tu
 
Monusco kuna peacekeeping na force intervation brigade(FBI) ambayo Tanzania, South africa na Malawi ilikuwa kwenye hiyo FIB 2013 unahusika moja kwa moja na kumshambulia adui.
Huko Congo mission zilizopo ni za peace forcing sudan ndio kuna peacekeeping.
Huu ni uongo mission iliyopo Eastern DRC ni peace keeping. Hiyo FIB ilifanyika 2013
 
Nashindwa kuelewa tunaambiwa vikosi vya umoja wa mataifa MONUSCO pamoja na SADC kazi yao ni kulinda amani huko mashariki ya DRC lakini kazi wanayoifanya ni kusaidia vikosi vya serikali ya Congo kupambana na M23 . Je kuna uhalali kuendelea kuwepo kwa vikosi hivyo vya kimataifa katika ardhi ya Congo? Nadhani wakati umefika sasa Umoja wa mataifa na SADC kuondoa majeshi yao kwakua jukumu walilopewa wameshindwa kulifanya kinachoendelea huko kwa sasa ni uhuni mtupu au wao ndio wezi wa madini ya Congo?
Kuna vikosi vya peacekeeping na vya kushambulia.
M23 wanafanya uharibifu tizama habari kila kona Congo raia hawawapendi m23 imefikia hatua m23 wanawaponza raia wa kawaida wa kitutsi waishio Congo.
Mwaka jana nimetizama habari kuna kijiji maeneo ya Kivu kuna mama wa kitutsi alielezea kuwa alikua akiishi vizuri tu na majirani ila toka m23 waanze vurugu majirani wakaanza kuwatenga na kuwafanyia unyama.
MTUTSI HUYO ALIKIRI AKISEMA M23 WAACHE VURUGU ZINAWAATHIRI WATUTSI WAISHIO DR CONGO.
Wewe ni nani useme vice versa mkuu!?
WAACHE WACHAPIKE
 
Mandate ya safari hii sio kulinda amani ni offensive kulinda raia wa Kongo wote wawe wanyamulenge or whatever

Wanaoumia Eastern Kongo sio wanyamulenge pekee ambao ni raia halali kabisa wa Kongo na wakongomani makabila ya Kongo wote wanaumia na hii vita sio kuwa M23 wakishambulia mji wowote Wanao suffer ni wakongo tu hata wanyamulenge wa Kongo wanakimbia nyumba zao kupigwa mabomu na uchumi kuharibiwa ukiwemo wa wanyamulenge sababu wateja wao wakongo wa biashara za jumla au rejareja

Mandate ya Sasa ya majeshi ya SADC sio peace keeping ni offensive shambulia yeyote anatesumbua wakongo na wanyamulenge wa Kongo kutoishi Kwa amani

Mfano mji wa Goma au eneo la Kivu likishambuliwa wanaoumua ni wote wakongo na wanyamulenge sababu mabomu na makombora hayajui pale anaishi mkongo au mnyamulenge

SADC ni offensive force sio peace force lengo ni kushambulia kikamilifu Kila yeyote anashambulia raia wa Kongo na Mali zao wakiwemo wakongomani na Banyamulenge kuwa wanaishi Kwa amani sababu Banyamulenge nao ni raia halali wa Kongo

Bomu au kombora likitua Kivu au Goma linaua raia wasio na hatia wakongo na Banyamulenge halibagui

SADC hawafanyi kazi ya peace keeping ni offensive adui akirusha risasi wanarusha makombora ya kufa mtu kulinda wakongo wasio na hatia na raia Banyamulenge waishio Hilo eneo

Jeshi la SADC sio peace mission ni Offensive army

Peace Mission ilikuwa majeshi ya Monusco yaliyoondoka baada ya kushindwa kuleta amani Eastern Congo Kwa wakongo na Raia wazaliwa wakongo Banyamulenge raia halali wa Kongo
 
Back
Top Bottom