zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,005
- 28,627
Habari za mchana wana JF, hivi Karibuni nimekuwa nafuatilia kwa ukaribu historia ya siasa za maziwa makuu ila nikagundua kitu fulani kilichonishangaza kidogo nikaona nilete mjadala kwa great thinkers tujadili pamoja.
Utangulizi
Kama tunavyofahamu DRC ni nchi iliyojaaliwa kuwa na maliasili ya kila aina kuanzia Gesi mpaka madini, ardhi nzuri, mvua za kutosha na mito/maziwa ya kutosha. Lakini changamoto kubwa imekua migogoro isiyoisha ama isiyo na nia ya kumalizwa sababu ya maslahi fulani wanayovuna kwenye utajiri wa nchi hii.
Hapo nyuma kidogo nimewahi kuleta uzi kuhusu 2nd congo war na jinsi majeshi ya Kitutsi yaani Banyamulenge, Rwanda,UG na Burundi walivyoiteka mashariki ya Congo na kujaribu kumpindua Rais Laurent Desire Kabila August 1998 kupitia operation kitona huko Kinshasa ambayo awali ilifeli kutokana na kuingia vitani kwa majeshi na ufadhili wa Zimbabwe na Angola pale kinshasa.
Nilipata maoni mengi sana kuonyesha Rwanda ilikua inatumika na wazungu, ama Rwanda iliingia kupora mali za DRC na maoni ya upande huo lakini tukisoma zaidi leo tutaangalia upande wa pili wa shilingi. Je majeshi yaliyoingia upande wa Kabilw yaliongozwa na tamaa ya hazina ama uzalendo?
KATANGA
Hili ni jimbo lililopo kusini mwa DRC na kiufupi tu ndio eneo lenye utajiri mkubwa sana wa madini DRC na liliwahi kuchangia 80% ya bajeti ya serikali ya DRC kila mwaka. Inazalisha madini kma dhahabu,almasi,shaba,fedha,cobalt,platinum,nickel n.k. Wakati vita inaanza mwaka 1998, DRC ilikua inazalisha Almasi yenye thamani ya Tsh 1.2 Trillion kwa mwaka achilia mbali zilizokuwa zinatoroshwa kifisadi mipakani.
Katanga ina 34% ya hazina ya madini ya Cobalt duniani ambayo hutengenezea battery za simu &Laptop, Engine za ndege, mashine za kuchakata gesi n.k. pia 10% ya hazina ya shaba duniani ipo Katanga. Kwa utajiri huu makampuni mengi ya madini yalikua pale Lubumbashi kusafirisha madini dunia nzima, kiufupi walipaita ''Kitovu cha madini ya DRC''.
Baada ya kidogo kupata picha kuhusu eneo hili sasa turudi kwenye kisa cha 2nd Congo war ama ''Vita kuu ya dunia ya Africa'' sababu ilihusisha nchi 13 kwenye mapigano ambapo upande mmoja walikuwepo Burundi,UG na Rwanda dhidi ya DRC, Sudan,Chad,Angola,Zimbabwe, Namibia,Libya,CAR,Ethiopia, Eritrea n.k
Kwa summary tu majeshi ya Rwanda na washirika wao yalipovamia DRC ili kumtoa Kabila waliyemuweka madarakani takribani mwaka mmoja tu uliopita, yaliteka haraka majimbo yote ya mashariki na kaskazini kuanzia Kivu zote mbili, Province Oriental na Manyema hivyo walikua wanaelekea kuteka Jimbo la Katanga ili kupata nguvu ya kiuchumi ya kuwawezesha kuendesha vita, kuparalyse nguvu ya kabila, na kuwapa njia fupi zaidi ya kufika Kinshasa.
Kabla ya kufika lubumbashi ambapo ni makao makuu ya Katanga, mapigano makali yalizuka kwenye mji muhimu wa Kindu ambapo ndio geti la kuelekea kusini mwa DRC palipo na jimbo la Katanga. Baada ya mtanange mzito kwa siku kadhaa Majeshi ya washirika wa Rwanda yalifanikiwa kuuteka mji huu October 1998, hivyo safari rasmi ya kuteka Hazina ya congo ilikua imeanza rasmi.