Hatma ya ndoa ya EAC na DRC mikononi mwa Kagame?

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Wakati Jamhuri ya Kidemorasia na Kongo (DRC) ilipokubaliwa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka 2022 watu wengi waliamini kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia kumaliza machafuko yaliyodumu kwa muda mrefu katika eneo la mashariki mwa DRC.

Ilidhaniwa kuwa DRC ikiwa mwanachama wa EAC, nchi nyingine wanachama zitafanya kila linalowezekana kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na kumaliza mashambulizi ya kikundi cha waasi cha M23.

Kwa kuwa kulikuwa na hisia kuwa Rwanda ndio inalisaidia kundi hilo, iliaminika kuwa DRC na Rwanda sasa zitakuwa watoto wa mama mmoja (EAC), basi wanaweza kusuluhishwa kwa haraka.

Lakini sasa imeonekana dhahiri kuwa hali imekuwa tofauti. Si tu kuwa waasi bado wanaendelea kuisumbua DRC, bali sasa kuna madai ya wazi kutoka kwa Serikali ya DRC kuwa majeshi ya Rwanda nayo yameanza kuivamia DRC moja kwa moja. Lakini Rwanda imekuwa ikukanusha tuhuma hizi.

Tshisekedi aonekana kukata tamaa na EAC
Rais Felix Tshisekedi wa DRC inaonekana amekatishwa tamaa na jinsi EAC ilivyoshindwa kumsaidia dhidi ya Kagame na Rwanda yake.

Hivi majuzi alidhihirisha chuki hiyo alipomuita Kagame kuwa ni dikteta (kuna thread humu JF - Rais wa DR Congo, Tshisekedi amlinganisha Rais Paul Kagame na Hitler). Ni nadra sana kwa kiongozi wa nchi kumwita mwenzake hivyo, tena hadharani.

Tshisekedi haikuishia hapo kuonyesha chuki yake dhidi ya Rwanda na Kagame. Katika mkutano wa kuhitimisha kampeni jijini Kinshasa akatangaza wazi wazi kuwa iwapo atashinda tena urais basi ataliomba Bunge limpe idhini ya kutangaza vita dhidi ya Rwanda. Akawataka wananchi wakae mkao wa mapigano ili idhini itakapotolewa basi waanze mapambano kuelekea Kigali.

Kama kuna watu walidhani kuwa Tshisekedi alitamka hayo kama sehemu ya kampeni alikosea sana kwani siku iliyofuata, wakati akizindua Kituo cha Uchumi jijini Kinshasa, alipewa zawadi ya jambia na kampuni kutoka Uturuki iliyojenga kituo hicho. Baada ya kulipokea jambia hilo, Tshisekedi akalitoa katika ala yake, akawaonyesha wananchi waliohudhuria hafla hiyo kisha akaenda kwenye kipaza sauti na kutangaza: “Hili ndilo jambia nitakalotumia kumchinja Kagame.”

Kwa Rais (mwanadiplomasia namba moja wa nchi) kutamka maneno kama haya hadharani inaonyesha ni jinsi gani mtu huyo amechoshwa na hilo jambo analolilalamikia.
 
Back
Top Bottom