Ugali gani? Kuna aina nyingi za ugali: wa sembe, wa 'dona', wa mtama, wa mihogo, wa ulezi nk.
Inabidi uende shule ujifunze masomo ya sayansi ya afya au Biology. Ujue kutofautisha nutrients zinazopatikana katika aina mbalimbali za ugali.
Ugali hauleti high blood pressure wala cancer moja kwa moja. Tatizo sio ugali, bali ni aina ya chakula kinacholiwa pamoja na ugali, au mtindo wa maisha kwa ujumla. Kwa mfano, mtu anayekula ugali mwingi kisha anakula nyama ya mafuta kila siku, hana mazoezi, na anakunywa soda au pombe — huyo yuko katika hatari zaidi ya kupatwa na magonjwa hayo, sio kwa sababu ya ugali bali kwa sababu ya mtindo wa maisha.
Ugali unatengenezwa kwa wanga kutoka nafaka kama mahindi, mtama au muhogo. Wanga ni chanzo muhimu cha nishati mwilini. Kinachotakiwa ni kiasi sahihi na mlo kamili unaojumuisha mboga, protini na matunda. Kupiga marufuku ugali ni kueneza hofu isiyo na msingi.
Biblia inatuonya katika 1 Timotheo 4:3-5 tujihadhari na watu wanaokataza wengine kula vyakula fulani:
"Wao huwakataza watu wasioe na kuwaagiza wajiepushe na vyakula fulani, ambavyo Mungu aliviumba ili vipokewe kwa shukrani na wale wanaoamini na kuijua kweli."
(1 Timotheo 4:3-5)
Soma pia, Mithali 25:16
"Ukipata asali, kula kiasi tu cha kukutosha, ukila zaidi, utatapika.."
Hapo tunafundishwa kula kwa kiasi, sio kupiga marufuku.