Kataa jamii kuwa sehemu ya maisha yako

Kataa jamii kuwa sehemu ya maisha yako

Mtambuzi,
Kuna vitu viwingi vina shabihiana.
Kwanza ni fikra sahihi, kisha mtu sahihi na kingine ni jamii sahihi.
Katika maisha yangu yote nimesha wahi kuona vitu sahihi vichache mno.
Kwanza ni mtu sahihi, pili ni fikra sahihi.
Sijawahi kuona kamwe jamii sahii, kwa kuwa jamii ni mlundikano wa watu wenye maono na maoni mkanganyiko, usahihi wa fikra na maono (vision) uko within someones heart. Mtambuzi you will always be my Mentor
Hapa ngoja niwaorodhesha ma mentali wangu wengine, ASHA dii, mwaJ, Mwita Maranya, Vin Diesel, na wengine wengi, mko wengi sana siwezi wataja wote hapa

Mnh! Bujibuji, am I your mentor? If so I honoured!
 
Last edited by a moderator:
Kaka Mtambuzi wengi tupo frustrated kwa kuwa tumeishia kuipendezesha jamii tukajikuta sio vitupendezavyo sisi. Jamii inatuona tumefanikiwa sana na tukijipima tunajiona hivyo ila ndani ya kilindi cha mioyo yetu hakuna chembe ya raha na ufahari kwa kuwa tumehangaika kuifurahisha jamii tukajisahau sisi wenyewe.

Ukiwa Kijana

1. Ukiwa single watakuuliza, kwanini huna Girlfriend au Boyfriend?

2. Ukiwa na mchumba, watahoji mmekaa sana mwaoana lini?

3. Ukioa utasikia, mbona hamzai nyie twataka wajomba na shangazi!
4. Mkizaa watakuja na hii, mtoto kakua mtafutieni dada au kaka yake!
5. Ukimtafuta, utasikia mbona mnazaa haraka haraka hamuogopi maisha? maswali maswali hadi unazeeka?

Ukiwa na Hela

1. Ukinenepa, we unanenepa tu hivi huogopi magonjwa (presha na kisukari)

2. Ukikonda, acha ubahili, pesa zote hizo unakuwa mbahili? wengine wanasema mara alitembeaga na dada/kaka fulani mwenye ngoma ndio imekolea sasa. Hamalizi mwaka lazima aondoke huyu.

3. Ukinunua gari, unanunuaje gari wakati hujajenga? huna kiwanja? Vijana wa siku hizi bure kabisa.

4. Ukijenga huna gari, yaani na usumbufu wote huu wa madaladala huna gari? tunakushangaa sana. Nunua ata Toyo!!

5. Ukiamua kusoma Mastere etc, unasomaje Masters wewe? kwani kuna kazi umewahi kuomba wakakunyima kwa kuwa huna masters... mimi sisomi tena hata nikihongwa. Watu wengine bhana kama wamenyweshwa vitabu.

6. Ukiamua kujiajiri, ndio watakusema kila aina ya maneno na kukunyanyapaa, ukifanikiwa ndio wakwanza kuja, aisee nina kijana wangu amemaliza chuo yupo tu nyumbani naomba umsaidie ngugu yangu.

Ukifanya mazoezi

1. Kama ni mwembamba, wee kimbau mbau unapunguza nini kwenye ako kamwili ako, (wanajua mazoezi ni kupunguza mwili)

2. Ukiwa Mnene, yaani Mungu hakupi vyote. Ona sasa amekula mikuku yake sasa ndio anateseka nayo kupungua.

3. Ukiwa na mwili wa wastani, huyu ni bishoo tu, hana lolote yeye ni kupita na vikaptula tu huku.

Hii jamii sijui jema ni lipi kwenu?

Nyie akina Ntuzu, Karucee OLESAIDIMU, Mr Rocky, miss chagga, Bantu lady, Mentor, mwallu, Mndengereko, utafiti mpo?

Huko kwenu jamii ikoje uko?
mkuuu umemaliza yoteee,huku mtaani ni shida aiseee,hata ufanye nini watasema tuu tena kwa maneno ya kukeraaa
 
Umemuulelewa Mtambuzi!!

Huwa najivunia uwepo wake, Nimesoma nimeelewa, kichwa kimedadavua niliyosoma na kimeyakubali.

Hitimisho ni kuyafanyia kazi yale niliyosomana kuyaelewa alafu nisubiri matokeo.

Hii ndio moja ya sifa muhimu na faida kuu za elimu.
Ahsante sana ndugu Mtambuzi.
 
[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
Hiyo ndio shida, ndio mana wengine tunaonekanaga wakorofi sana, vipangamizi kibao, lakini naonaga bora niende sawa na wachache kuliko kwenda sawa na robo tatu ya jamii huku nakijua nafanya unafiki kuridhisha jamii.
Sasa Nyama yetu mbona hutupi na sisi?
 
[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85]
Yaani sisi tulioishia darasa la pili mnatukomoa kweli yaani mpaka tunashika adabu saaana,sasa hayo ma(emoji85) ndio makitu gani jamani? au ndio unanitukana kihaya? mimi Mkurya bhana acha hizo.
 
Nimegusika kwa kweli na hii mada yaani siwezi kuishi navotaka kwenda napotaka na wakati napotaka bila kutaarifu wakwe zangu kwa kuogopa kusemwa
 
Back
Top Bottom