Kataa jamii kuwa sehemu ya maisha yako

Kataa jamii kuwa sehemu ya maisha yako

Asante sana Suprise, Ni heshima kubwa kusikia haya kutoka kwako.
Ndio jamii yetu, Inatupasa kuionesha upande sahihi kwa kile wanachokiamini.

Please Do have a good day.
mkuu Tized nimekupenda bure, hahaha, sasa utakua unaambiwa wot next na jamiii
 
Last edited by a moderator:
Big up mkuu Mtambuzi hapo umehit the point, mada yako inanikumbusha kipindi nimemalza kidato cha 4 ambapo nilikuwa mchepuo wa sayansi na jamii nzima iliyonizunguka hasa family walikuwa wanataka nikiende kidato cha 5 basi nisome sayansi ili nije kuwa dokta, kwakweli sitosahau ilikuwa ni vita kali hasa baada ya kusimamia uamuzi wangu wa kusoma mchepuo wa sanaa sababu ndoto zangu na moyo wangu ulikuwa huko, Namshukuru Mungu mwanzo sikueleweka na hatimaye leo hii nimeleweka baada ya wao kuona matunda yake.

"The strongest man in the world is the one who walks alone"-Henrik Isben
 
Last edited by a moderator:
Solution ni Uislam.

Hakuna mfumo bora wa maisha kama Uislam.
Mfumo mzuri wa maisha ni ule uliojichagulia na unaokupa amani ndani ya moyo wako usio vunja heshima ya mtu wala kumkwaza.

Sio uishi kwa kufuata jamii ya watu wenye imani fulani wanaofuata maandiko yaliyoandikwa na kusomeka kutoka kushoto kwenda kulia.

Hapo bado utakuwa unaturudisha kule kule kwenye maisha ya kufungwa na matakwa ya jamii kwa kigezo cha imani fulani na hadithi za vitabuni..
 
Kaka Mtambuzi wengi tupo frustrated kwa kuwa tumeishia kuipendezesha jamii tukajikuta sio vitupendezavyo sisi. Jamii inatuona tumefanikiwa sana na tukijipima tunajiona hivyo ila ndani ya kilindi cha mioyo yetu hakuna chembe ya raha na ufahari kwa kuwa tumehangaika kuifurahisha jamii tukajisahau sisi wenyewe.

Ukiwa Kijana:-
1. Ukiwa single watakuuliza....--..kwanini huna Girlfriend au Boyfriend??
2. Ukiwa na mchumba..... watahoji mmekaa sana mwaoana lini??
3. Ukioa utasikia.......--...... mbona hamzai nyie twataka wajomba na shangazi..!!
4. Mkizaa watakuja na hii.....mtoto kakua mtafutieni dada au kaka yake!
5. Ukimtafuta.....-.. utasikia mbona mnazaa haraka haraka hamuogopi maisha.?? maswali maswali hadi unazeeka?

6. Mkizeeka..watakuja na hili..daahh ebana mmezeeka lakini hamfi?
 
Karibu sana mkuu, pia asante kwa hekima zako, Ndio jamii yetu hio.

Inahitaji watu wanaoweza kufanya maamuzi na KUYASIMAMIA ili kuionesha jamii upande wa pili wa shilingi ukoje. Japo watasema na kuponda sana lakini kwa kuwa hujamkosea mtu na ni uamuzi wako binafsi.. UNASONGA MBELE.. na utashangaa baadae wakishakuelewa wanakua wa kwanza kuja kukupongeza ila ndio waliokuwa wapingaji wa kwanza kabisa.

Point kubwa naoiona.. UJASIRI, KUFANYA MAAMUZI NA KUUSIMAMIA HUO UAMUZI bila kuingilia haki ya wengine. Maana wanasemaga... katika hali yoyote, kitu BORA kabisa ni kufanya UAMUZI sahihi, cha pili bora ni kufanya uamuzi hata kama sio uamuzi sahihi. Na cha tatu ambacho ndio kibaya kupita vyote ni KUTOKUFANYA UAMUZI WOWOTE.

Mkuu Tized umenikumbusha wakati nilipofanya maamuzi ya kuamua kuacha dini ya mapokeo ambayo niliirithi kutoka kwa wazazi wangu nilitengwa na baadhi ya ndugu zangu, baba yangu (mama yangu alikwishafariki wakati huo) alinikabili kutaka kujua sababu ya kuasi dini yake, nilimuuliza maswali mawili tu akashindwa kunijibu na kunipa ruksa kuwa mpagani.

Hayo yalikuwa nai maamuzi yangu na ninafurahi kubaki hivyo na najivunia kujiita mpagani mahali popote.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tized umenikumbusha wakati nilipofanya maamuzi ya kuamua kuacha dini ya mapokeo ambayo niliirithi kutoka kwa wazazi wangu nilitengwa na baadhi ya ndugu zangu, baba yangu (mama yangu alikwishafariki wakati huo) alinikabili kutaka kujua sababu ya kuasi dini yake, nilimuuliza maswali mawili tu akashindwa kunijibu na kunipa ruksa kuwa mpagani.

Hayo yalikuwa nai maamuzi yangu na ninafurahi kubaki hivyo na najivunia kujiita mpagani mahali popote.

Kwani upagani cyo dini?
 
Last edited by a moderator:
Mfumo mzuri wa maisha ni ule uliojichagulia na unaokupa amani ndani ya moyo wako usio vunja heshima ya mtu wala kumkwaza.

Sio uishi kwa kufuata jamii ya watu wenye imani fulani wanaofuata maandiko yaliyoandikwa na kusomeka kutoka kushoto kwenda kulia.

Hapo bado utakuwa unaturudisha kule kule kwenye maisha ya kufungwa na matakwa ya jamii kwa kigezo cha imani fulani na hadithi za vitabuni..

Hayo ni maoni yako na siwezi kuyapinga, niliyoyaweka ni yangu na ukipenda yafuate usipoyapenda usiyafate.

Wewe na njia yako nami na njia yangu.
 
Solution ni Uislam.

Hakuna mfumo bora wa maisha kama Uislam.

Jisomee:

Tuishi Kiislam



Tofauti yetu na wasio kuwa Waislam si chengine kipya ila ni tabia. Uzuri wa mwenendo wa maisha yetu ndio utakaotupatia sifa mbele ya jamii isiyokuwa ya Waislam. Hima yetu ya kutosema uongo na kufuata maadili ya ajabu ndio utakuwa msingi imara wa imani yetu. Haya yote yameelezwa na Habiybul Mustwafaa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa hakuletwa yeye isipokuwa kurekebisha jamii kuwa na tabia njema.

Hakika Uislamu wetu umekamilika kwa kuwa na tabia bora za kuigwa na Waislam wenyewe kwa ushahidi wa Qur-aan na Sunnah.

Kama kweli sisi ni Waislam tunaoipenda diyn yetu ni lazima tuwe tayari kuanza kubadilika kila hatua ya maisha yetu kwa kuishi Kiislam. Zingatio letu litatupeleka hatua baada ya hatua ili kurekebisha nyumba iliyojikita kwenye masuala yasioendana kabisa na mila zetu sisi Waislam.


1. TUZUNGUMZE KIISLAM

Muislam wa kweli ni lazima awe ni mkweli, hatakiwi kuzua uongo, kufitinisha, kusengenya wala kuzungumza kwa sauti ya juu. Haya tunayapata ndani ya Qur-aan:

{{Na uteremshe sauti yako; bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote (kwa makelele yake ya bure).}} [Surat Luqmaan: 19]

Pia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuhimiza sana kushikamana katika kusema ukweli:

"Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli unapeleka katika wema, na wema unapeleka Peponi." [Muslim]


2. TULE KIISLAM

Muislam anatakiwa ale kilicho mbele yake kwa kutumia mkono wa kulia na asiwe na papara ya kusukuma tonge namna ya kima anavyokula. Aanze kula kwa kusema "BismiLlaah" na amalize kwa kusema "AlhamduliLlaah". Chakula cha Muislam ni lazima kiwe ni cha halali, hatakiwi kula ovyo ovyo kama wanavyofanya wasiokuwa Waislam. Anapokula aligawe tumbo lake kwenye thuluthi tatu. Thuluthi moja ni ya chakula, nyengine ni ya maji na mwisho ni hewa. Hii ni kwa mujibu wa dalili ya Hadityh:

"Kama ukilazimika kula hakikisha theluthi moja ya tumbo lako unaijaza chakula, theluthi moja maji na acha theluthi moja kwa ajili ya hewa (yaani iache tupu)" (At-Tirmidhiy).


3. TUSIKILIZE KIISLAM

Muziki ni haramu na haifai kwa Muislam kuutengeneza, kutengenezewa, kuimba, kuimbiwa, kuutangaza, kuupeleka muziki, kuuza, kula thamani yake, kununua na kuuza. Muziki umekuwa ni tatizo kubwa kwa Waislam kwani wengine hata usingizi hawapati bila ya kusikiliza muziki. Nyumba za Kiislam sasa zimekuwa sawa na magofu kwa kutopatikana maadili ya Kiislam. Kwani wengi wanaishi tofauti na mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni muhimu kwa Waislam wakawa wanasoma Qur-aan kila siku kwa sauti na kwa kusikilizana kwa mtindo wa dawaar (mmoja baada ya mwengine). Tuzibadilishe nyumba zetu kwa kusikiliza idhaa za Kiislam zisizokuwa na mambo ya uchafu na uzushi.

((Na soma Qur-aan kwa utaratibu na utungo)) [Al-Muzammil 73: 4]

Muislam anayesoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika na Mitume (‘Alayhi swalaatu was-salaam). Hata yule asiyejua kusoma Qur-aan ni vyema akawa na jitihada ya kujifundisha ilhali anakosea au hata kuchekwa. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((Yule ambaye kwamba anasoma Qur-aan naye ni mjuzi (hana shida aina yoyote) atakuwa pamoja na Malaika na Mitume (‘Alayhi swalaatu was-salaam) na watiifu. Na yule ambaye kwamba anarudia pamoja na kuwa na shida katika kusoma basi atakuwa na ujira mara mbili(( [al-Bukhaariy, Muslim, Tirmidhy na Ibn Maajah kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)]


4. TUVAE NA TUTEMBEE KIISLAM

Maringo ya kutembea bila ya shaka yanatokana na mtu kuvaa nguo za kifakhari ambazo hazitakiwi kuvaliwa kwa Muislam. Muislam wa kiume anatakiwa avae nguo zisizoburura. Mwanamke hatakiwi kuonekana zaidi ya viganja vya mikono na kipaji cha sura yake. Mapambo yote ni halali kwa mumewe na walio Maharimu wake. Haitakikani Muislam kutembea kwa kujivuna, kujifakharisha na maringo. Hivi sivyo Uislam unavyotufundisha kuishi. Qur-aan inasema:

{{Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala huwezi kufikia urefu wa milima}} [Surat Israa: 37]

Usiwaangalie watu kwa jeuri au kwa upande mmoja wa uso. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

{{Wala usiwatazame (usiwafanyie watu jeuri), kwa upande mmoja wa uso, wala usende katika ardhi kwa maringo, hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye.}} [Surat Luqmaan: 18]


5. TUJENGE URAFIKI WA KIISLAM

Miongoni mwa matatizo makubwa ya vijana wetu pamoja na Waislam kukosa maadili ya Kiislam ni kuwa na marafiki wasiokuwa na maadili mema. Ni vyema Muislam akawa hana rafiki hata mmoja kuliko kuwa na marafiki kumi wasioishi Kiislam. Kuishi Kiislam yatakikana juhudi na inaanza kwa kuwa na rafiki mwema atakayekukemea unapofanya kosa na kukupa maneno ya subra wakati wa huzuni.

Lazima tuchague marafiki ambao wako radhi na dini yetu na tuepukane na wale ambao hawako radhi na dini yetu. Na tukiona marafiki zetu matendo yao sio mazuri, ni lazima tuepukane nao kwa sababu tunaweza tukaiga tabia zao ambazo zinakwenda kinyume na dini yetu.
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu yamkini kufuata dini ya rafiki yake, kwa hivyo muangalie unayemfanya rafiki." (Abuu Daawuud na Tirmidhiy)

6. TULALE KIISLAM

Tumalizie kwa kuona namna anavyotakiwa Muislam kuimaliza siku yake kwa kujipumzisha Kiislam. Muislam anatakiwa atie wudhuu kabla ya kulala, wudhuu unaendana na Sunnah ya kupiga mswaki. Ni vizuri ukaswali rakaa tatu za witri (kwa wasioamka usiku).

Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akienda kulala usiku anakusanya viganja vyake kisha akivipuliza na akivisomea Suratul-Ikhlaas, na Suratul-Falaq, na Suratu-Nnaas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani na usoni na mbele (akifanya hivyo mara tatu).
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ukienda kulala soma Ayatul-Kursiy mpaka uimalize kwani Mwenyezi Mungu Ataendelea kukuhifadhi wala hakukaribii shetani mpaka asubuhi"
Unapolala ulaze ubavu kwa upande wa kulia na usome du'aa ifuatayo:

اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وا جْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت
"Ewe Mwenyezi Mungu nimeisalimisha nafsi yangu kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nimeuelekeza uso wangu kwako na nimeutegemeza mgongo wangu kwako, kwa matarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila kwako, nimekiamini kitabu chako ulichokiteremsha na Mtume wako uliyemtuma".

Bila ya shaka tutakapoishi Kiislam tutakuwa mbali na wasiokuwa Waislam. Hivyo maisha yetu yatakuwa hakika ni ya Kiislam. Kila kitu yatakikana juhudi na inaanza kwa nafsi kujifunga kukubali mafundisho ya Kiislam. Inawezekana kubadilika kwa kuishi Kiislam. Anza sasa, katu usichelewe kuishi Kiislam.



is this all you know?am sorry to say a lot of gold has been mined from the brains of men than has ever been taken from the earth.
 
I like your the statement.. Though Inatia Hasira sana.
is this all you know?am sorry to say a lot of gold has been mined from the brains of men than has ever been taken from the earth.
 
Hongera sana Mkuu kwa kusimamia uamuzi wako, Huwa naamini kila mmoja wetu anao uhuru kamili wa kuamua yale yamfaayo na ndivyo kila mtu anawajibika kwa nafsi yake mwenyewe kwa uamuzi wake. [Accountability and responsibility]

Binafsi nimevutiwa sana kujua kwa nini uliamua kuasi mkuu (I mean kwa nini uliamua kuchagua ulichochagua?) Maana lazima utakuwa na sababu zako za maana na za msingi sana either ulikoenda kulikuvutia au ulikotoka kulikukwaza. Ningependa sana kukujifunza mkuu. Natanguliza shukrani. Ikibidi PM tafadhali.

Mkuu Tized umenikumbusha wakati nilipofanya maamuzi ya kuamua kuacha dini ya mapokeo ambayo niliirithi kutoka kwa wazazi wangu nilitengwa na baadhi ya ndugu zangu, baba yangu (mama yangu alikwishafariki wakati huo) alinikabili kutaka kujua sababu ya kuasi dini yake, nilimuuliza maswali mawili tu akashindwa kunijibu na kunipa ruksa kuwa mpagani.

Hayo yalikuwa nai maamuzi yangu na ninafurahi kubaki hivyo na najivunia kujiita mpagani mahali popote.
 
Kuna wakati inatulazimu kuishi aina fulani ya maisha kutoka na jamii tutokazo, kimsingi swala hili ndilo haswa linamfanya mtu aonekane tofauti anapofanya kitu tofauti na jamii yake, swala la msingi la kujiuliza je? jamii yako maisha inayoishi yapo kwa misingi na kwa matakwa ya nani? je wewe ukiamua kuishi maishi yako ambayo ni tofauti na wao utakuwa umemkosea huyo ambae jamii yako inashi chini ya misingi yake na matakwa yake.

Kama jibu ni hapana, utakapoamua kuishi maisha yako sio mbaya ila jambo la msingi ni kwamba uishi katika misingi hii;
(1)Amani
(2)Upendo
(3)Heshima n.k
Kuna wakati ukiamua kuchangua maisha yako upendayo inakubidi utoke nje ya maagizo mbali mbali na imani zinazo kufunga.

Sasa si ndio hayo Mtambuzi kayasema wewe ni nani wa kumpangia mtu hiyo misingi?
Kubwa kwa yote either unaishi kwa kupangiwa au upendavyo ni kupata balance ya kila kitu
 
Last edited by a moderator:
is this all you know?am sorry to say a lot of gold has been mined from the brains of men than has ever been taken from the earth.

Yes, that is what I know but not "all".

What do you know?
 
Hayo ni maoni yako na siwezi kuyapinga, niliyoyaweka ni yangu na ukipenda yafuate usipoyapenda usiyafate.

Wewe na njia yako nami na njia yangu.

Wajifanya aalimu kumbe si lolote.

Haya endelea na njia yako ila usione bora kuliko za wengine.!
 
Back
Top Bottom