Kataa jamii kuwa sehemu ya maisha yako

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,808
2,000Wengi wetu tumefungwa sana na jamii kiasi kwamba kuwa sisi siyo jambo rahisi kiasi hicho. Kinachokubaliwa na jamii ndiyo sahihi hata kama kinanuka kiasi gani. Hivyo ndivyo tunavyotakiwa kuwa kwa sababu sisi ni jamii na tunatakiwa kuishi kwa matakwa ya jamii na siyo tutakavyo sisi.

Ukweli tunatakiwa tuwe nao sisi na siyo jamii. Lakini kwa bahati mbaya hatujawahi kuwa sisi, siku zote tumekuwa jamii, hivyo tunasikiliza jamii inasemaje kuhusu sisi na inatutaka tuishi vipi. Tukiwa sisi jamii itaona tumeasi au tumekuwa vichaa.

Jamii haitaki tujitambue (tujue sisi ni nani). tukijitambua tutakoma kuwa jamii na jamii haiko tayari kutupoteza maana tayari tumeshakuwa watumwa wa jamii.

Kama tukiwa sisi jamii haiwezi kututumia itakavyo. Tukifanya jambo zuri tunapendwa na kusifiwa; na tukifanya kinyume na matakwa ya jamii tunachukiwa na kubezwa. Hii hujenga choyo cha kujipenda zaidi ambacho hutaka kushibishwa kila siku.

Mtu anajitahidi kufanya kile ambacho jamii inampangia ili kushibisha choyo alichopewa na jamii husika. Atataka gari na nyumba kwa sababu jamii imemwambia ni vya maana na vinampa thamani siyo kwa sababu yeye anavitaka. Atataka asome sana ajikusanyie digrii nyingi sana, aoe mke mzuri sana, awe tajiri sana, apate umaarufu sana, yote ikiwa ni choyo alichopewa na jamii. Kila siku tunatafuta sisi ni akina nani kupitia kwa watu wengine, kwamba, wakituona, kututambua na kutusifia ndipo tunahisi kuwa sisi.

Jamii inayumba kila siku kuhusu kipi ni kipi na hivyo na sisi tunayumba kila siku kwa sababu hatuishi kama sisi bali tunaishi vile jamii itakavyo. Maamuzi yetu na mitazamo yetu inategemea tu namna itakavyopokelewa na jamii. Na ndio maana unaweza kushangaa mtu anasema, "Hivi nikiolewa na fulani au nikimuoa fulani watu watanionaje?" Yaani si kwamba yeye hampendi huyo anayetaka kumuoa au anayetaka kuolewa naye bali anaogopa namna jamii itakavyomuona na kumhukumu kwa sababu tu huyo anayetaka kumuoa au kuolewa naye amepachikwa sifa mbaya na jamii, na yeye hayuko tayari kwenda kinyume na jamii…. Ajabu eh!

Kumbuka wakati unazaliwa ulishakuwa wewe na uwewe wako bado unao. Lakini kwa sababu umepewa uwewe mwingine na jamii ndiyo maana kuchanganyikiwa na kujuta ni kwingi sana. Ni hadi hapo utakapovua uwewe uliopewa na jamii na kubaki na uwewe uliozaliwa nao (kuwa wewe halisi) , ndipo kuchanganyikiwa na kujuta kutaisha. Inawezekana!!!

Jitambue…………….

@Lara1, King'asti, snowhite, gfsonwin, AshaDii, Fixed Point, miss neddy, miss chagga, Karucee, Chocs, Neylu, Lady doctor, Lisa, Nivea, charminglady, Heaven on Earth, Munkari, MankaM, BADILI TABIA, Kongosho, The Boss, Asprin, Nyani Ngabu, Bujibuji, Nicas Mtei, Mwita Maranya, Kiranga, Zinduna, Ruttashobolwa, Kaizer, Husninyo, MwanajamiiOne, DEMBA, Preta, marejesho, Nyamayao
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,808
2,000
mara nyingi unapojaribu kuwa THE REAL YOU...lazima ukutane na vipingamizi tuu...
What is 'right' or 'wrong' is highly perceptional....
Wapiiii miss independent lara 1

Namfagilia sana lara 1 yeye ni mmoja wa watu wanaoshi vile wapendavyo na si jamii ipendavyo..
Haishangazi ndiyo maana anapingwa sana na wadau wengi sana humu JF.
 
Last edited by a moderator:

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,613
2,000
Mtambuzi habari za masiku aiseee?!
Back to mada yako, nakubaliana na wewe maana hata sasa jamii inatulazimisha tutenge bajeti yetu kubwa sana kila mwezi kwa ajili ya kutoa michango ya harusi, send-off, kitchen party nk. badala ya kuzikusanya fedha hizi na kufanyia mambo mengine ya maendeleo! (Hapa simaanishi msitoe michango ya namna hii, za kuambiwa changanya na zako!!!) Usiposhiriki kwenye mfano wa jambo nililolitaja, jamii inaweza isikuelewe, na moja kwa moja utajikuta unaishi nje ya jamii!
 

Tized

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
4,024
2,000
Kaka Mtambuzi wengi tupo frustrated kwa kuwa tumeishia kuipendezesha jamii tukajikuta sio vitupendezavyo sisi. Jamii inatuona tumefanikiwa sana na tukijipima tunajiona hivyo ila ndani ya kilindi cha mioyo yetu hakuna chembe ya raha na ufahari kwa kuwa tumehangaika kuifurahisha jamii tukajisahau sisi wenyewe.

Ukiwa Kijana

1. Ukiwa single watakuuliza, kwanini huna Girlfriend au Boyfriend?

2. Ukiwa na mchumba, watahoji mmekaa sana mwaoana lini?

3. Ukioa utasikia, mbona hamzai nyie twataka wajomba na shangazi!
4. Mkizaa watakuja na hii, mtoto kakua mtafutieni dada au kaka yake!
5. Ukimtafuta, utasikia mbona mnazaa haraka haraka hamuogopi maisha? maswali maswali hadi unazeeka?

Ukiwa na Hela

1. Ukinenepa, we unanenepa tu hivi huogopi magonjwa (presha na kisukari)

2. Ukikonda, acha ubahili, pesa zote hizo unakuwa mbahili? wengine wanasema mara alitembeaga na dada/kaka fulani mwenye ngoma ndio imekolea sasa. Hamalizi mwaka lazima aondoke huyu.

3. Ukinunua gari, unanunuaje gari wakati hujajenga? huna kiwanja? Vijana wa siku hizi bure kabisa.

4. Ukijenga huna gari, yaani na usumbufu wote huu wa madaladala huna gari? tunakushangaa sana. Nunua ata Toyo!!

5. Ukiamua kusoma Mastere etc, unasomaje Masters wewe? kwani kuna kazi umewahi kuomba wakakunyima kwa kuwa huna masters... mimi sisomi tena hata nikihongwa. Watu wengine bhana kama wamenyweshwa vitabu.

6. Ukiamua kujiajiri, ndio watakusema kila aina ya maneno na kukunyanyapaa, ukifanikiwa ndio wakwanza kuja, aisee nina kijana wangu amemaliza chuo yupo tu nyumbani naomba umsaidie ngugu yangu.

Ukifanya mazoezi

1. Kama ni mwembamba, wee kimbau mbau unapunguza nini kwenye ako kamwili ako, (wanajua mazoezi ni kupunguza mwili)

2. Ukiwa Mnene, yaani Mungu hakupi vyote. Ona sasa amekula mikuku yake sasa ndio anateseka nayo kupungua.

3. Ukiwa na mwili wa wastani, huyu ni bishoo tu, hana lolote yeye ni kupita na vikaptula tu huku.

Hii jamii sijui jema ni lipi kwenu?

Nyie akina Ntuzu, Karucee OLESAIDIMU, Mr Rocky, miss chagga, Bantu lady, Mentor, mwallu, Mndengereko, utafiti mpo?

Huko kwenu jamii ikoje uko?
 

Nanaa

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
5,905
1,225
Asante, mada yako imekuja wakati muafaka, nipo katika mgogoro wa nafsi juu ya maamuzi fulani hivi.
Ila hii mada imenipa mwanga wa hatua ya kuanzia.
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,808
2,000
Mtambuzi habari za masiku aiseee?!
Back to mada yako, nakubaliana na wewe maana hata sasa jamii inatulazimisha tutenge bajeti yetu kubwa sana kila mwezi kwa ajili ya kutoa michango ya harusi, send-off, kitchen party nk. badala ya kuzikusanya fedha hizi na kufanyia mambo mengine ya maendeleo! (Hapa simaanishi msitoa michango ya namna hii, za kuambiwa changanya na zako!!!) Usiposhiriki kwenye mfano wa jambo nililolitaja, jamii inaweza isikuelewe na moja kwa moja na pia utajikuta unaishi nje ya jamii!

Habari za siku tele mkuu HorsePower
Nakubaliana na wewe kwamba jamii imekuwa sehemu ya maisha yetu, imefika mahali mtu anataka kufanya jambo ambalo binafsi anajua litampa furaha au litamletea faida, lakini anawaza jamii itamuonaje, yaani kila kitu kwetu ni jamii jamii jamii, hatufanyi kwa utashi wetu bali tunafanya kwa utashi wa jamii.
Mimi hapa kibaruani kwangu wanajua kabisa zaidi ya misiba na matatizo ya ugonjwa sichangii chochote kinachohusisha sherehe ya kupangwa......
Wamesema wee, lakini nimeweka pamba masikioni na huwa wanaambiana kabisa kwamba mimi sichangiagi sherehe.

Nashukuru jambo hilo nimemudu.
 
Last edited by a moderator:

Nyamayao

JF-Expert Member
Jan 22, 2009
6,969
1,225
mara nyingi unapojaribu kuwa THE REAL YOU...lazima ukutane na vipingamizi tuu...
What is 'right' or 'wrong' is highly perceptional....
Wapiiii miss independent lara 1

Hiyo ndio shida, ndio mana wengine tunaonekanaga wakorofi sana, vipangamizi kibao, lakini naonaga bora niende sawa na wachache kuliko kwenda sawa na robo tatu ya jamii huku nakijua nafanya unafiki kuridhisha jamii.
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,808
2,000
Kaka Mtambuzi wengi tupo frustrated kwa kuwa tumeishia kuipendezesha jamii tukajikuta sio vitupendezavyo sisi. Jamii inatuona tumefanikiwa sana na tukijipima tunajiona hivyo ila ndani ya kilindi cha mioyo yetu hakuna chembe ya raha na ufahari kwa kuwa tumehangaika kuifurahisha jamii tukajisahau sisi wenyewe.

Ukiwa Kijana:-
1. Ukiwa single watakuuliza....--..kwanini huna Girlfriend au Boyfriend??
2. Ukiwa na mchumba..... watahoji mmekaa sana mwaoana lini??
3. Ukioa utasikia.......--...... mbona hamzai nyie twataka wajomba na shangazi..!!
4. Mkizaa watakuja na hii.....mtoto kakua mtafutieni dada au kaka yake!
5. Ukimtafuta.....-.. utasikia mbona mnazaa haraka haraka hamuogopi maisha.?? maswali maswali hadi unazeeka?

Tized umenifurshisha sana na hiyo analysis yako, kweli binadamu hatuna jema aisee.............
 

JJ10

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
282
0
Mtambuzi' you have touched the deapest part of my heart!!! Nilikutana na hayo mambo pindi niliamua kuacha kazi''' pia yalinitokea pindi nataka kuoa!! Kazi kwelikweli it needs self Consciousness and commitment otherwise jamii itakuwa inakuendesha kwakila jambo..
 

badiebey

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
5,877
1,500
Namfagilia sana lara 1 yeye ni mmoja wa watu wanaoshi vile wapendavyo na si jamii ipendavyo..
Haishangazi ndiyo maana anapingwa sana na wadau wengi sana humu JF.

umeona ehhh....so many a times we have regrets kwa sababu ya kukosa uthubutu wa kuishi na kufika pale tunapotaka,kama mwanamke ndo kabisaaa waonekana mcharuko....ya nini ukae ku-dream low kisa jamii itakuonaje,wakati deep in ur heart u want the really big things,good life nk?...in the end mtu ishi upendavyo maneno ya watu huwa hayaishi hata uwe mwema kama yesu
 
Last edited by a moderator:

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Solution ni Uislam.

Hakuna mfumo bora wa maisha kama Uislam.

Jisomee:

Tuishi Kiislam


Naaswir Haamid


Tofauti yetu na wasio kuwa Waislam si chengine kipya ila ni tabia. Uzuri wa mwenendo wa maisha yetu ndio utakaotupatia sifa mbele ya jamii isiyokuwa ya Waislam. Hima yetu ya kutosema uongo na kufuata maadili ya ajabu ndio utakuwa msingi imara wa imani yetu. Haya yote yameelezwa na Habiybul Mustwafaa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa hakuletwa yeye isipokuwa kurekebisha jamii kuwa na tabia njema.

Hakika Uislamu wetu umekamilika kwa kuwa na tabia bora za kuigwa na Waislam wenyewe kwa ushahidi wa Qur-aan na Sunnah.

Kama kweli sisi ni Waislam tunaoipenda diyn yetu ni lazima tuwe tayari kuanza kubadilika kila hatua ya maisha yetu kwa kuishi Kiislam. Zingatio letu litatupeleka hatua baada ya hatua ili kurekebisha nyumba iliyojikita kwenye masuala yasioendana kabisa na mila zetu sisi Waislam.


1. TUZUNGUMZE KIISLAM

Muislam wa kweli ni lazima awe ni mkweli, hatakiwi kuzua uongo, kufitinisha, kusengenya wala kuzungumza kwa sauti ya juu. Haya tunayapata ndani ya Qur-aan:

{{Na uteremshe sauti yako; bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote (kwa makelele yake ya bure).}} [Surat Luqmaan: 19]

Pia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuhimiza sana kushikamana katika kusema ukweli:

"Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli unapeleka katika wema, na wema unapeleka Peponi." [Muslim]


2. TULE KIISLAM

Muislam anatakiwa ale kilicho mbele yake kwa kutumia mkono wa kulia na asiwe na papara ya kusukuma tonge namna ya kima anavyokula. Aanze kula kwa kusema "BismiLlaah" na amalize kwa kusema "AlhamduliLlaah". Chakula cha Muislam ni lazima kiwe ni cha halali, hatakiwi kula ovyo ovyo kama wanavyofanya wasiokuwa Waislam. Anapokula aligawe tumbo lake kwenye thuluthi tatu. Thuluthi moja ni ya chakula, nyengine ni ya maji na mwisho ni hewa. Hii ni kwa mujibu wa dalili ya Hadityh:

"Kama ukilazimika kula hakikisha theluthi moja ya tumbo lako unaijaza chakula, theluthi moja maji na acha theluthi moja kwa ajili ya hewa (yaani iache tupu)" (At-Tirmidhiy).


3. TUSIKILIZE KIISLAM

Muziki ni haramu na haifai kwa Muislam kuutengeneza, kutengenezewa, kuimba, kuimbiwa, kuutangaza, kuupeleka muziki, kuuza, kula thamani yake, kununua na kuuza. Muziki umekuwa ni tatizo kubwa kwa Waislam kwani wengine hata usingizi hawapati bila ya kusikiliza muziki. Nyumba za Kiislam sasa zimekuwa sawa na magofu kwa kutopatikana maadili ya Kiislam. Kwani wengi wanaishi tofauti na mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni muhimu kwa Waislam wakawa wanasoma Qur-aan kila siku kwa sauti na kwa kusikilizana kwa mtindo wa dawaar (mmoja baada ya mwengine). Tuzibadilishe nyumba zetu kwa kusikiliza idhaa za Kiislam zisizokuwa na mambo ya uchafu na uzushi.

((Na soma Qur-aan kwa utaratibu na utungo)) [Al-Muzammil 73: 4]

Muislam anayesoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika na Mitume (‘Alayhi swalaatu was-salaam). Hata yule asiyejua kusoma Qur-aan ni vyema akawa na jitihada ya kujifundisha ilhali anakosea au hata kuchekwa. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((Yule ambaye kwamba anasoma Qur-aan naye ni mjuzi (hana shida aina yoyote) atakuwa pamoja na Malaika na Mitume (‘Alayhi swalaatu was-salaam) na watiifu. Na yule ambaye kwamba anarudia pamoja na kuwa na shida katika kusoma basi atakuwa na ujira mara mbili(( [al-Bukhaariy, Muslim, Tirmidhy na Ibn Maajah kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)]


4. TUVAE NA TUTEMBEE KIISLAM

Maringo ya kutembea bila ya shaka yanatokana na mtu kuvaa nguo za kifakhari ambazo hazitakiwi kuvaliwa kwa Muislam. Muislam wa kiume anatakiwa avae nguo zisizoburura. Mwanamke hatakiwi kuonekana zaidi ya viganja vya mikono na kipaji cha sura yake. Mapambo yote ni halali kwa mumewe na walio Maharimu wake. Haitakikani Muislam kutembea kwa kujivuna, kujifakharisha na maringo. Hivi sivyo Uislam unavyotufundisha kuishi. Qur-aan inasema:

{{Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala huwezi kufikia urefu wa milima}} [Surat Israa: 37]

Usiwaangalie watu kwa jeuri au kwa upande mmoja wa uso. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

{{Wala usiwatazame (usiwafanyie watu jeuri), kwa upande mmoja wa uso, wala usende katika ardhi kwa maringo, hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye.}} [Surat Luqmaan: 18]


5. TUJENGE URAFIKI WA KIISLAM

Miongoni mwa matatizo makubwa ya vijana wetu pamoja na Waislam kukosa maadili ya Kiislam ni kuwa na marafiki wasiokuwa na maadili mema. Ni vyema Muislam akawa hana rafiki hata mmoja kuliko kuwa na marafiki kumi wasioishi Kiislam. Kuishi Kiislam yatakikana juhudi na inaanza kwa kuwa na rafiki mwema atakayekukemea unapofanya kosa na kukupa maneno ya subra wakati wa huzuni.

Lazima tuchague marafiki ambao wako radhi na dini yetu na tuepukane na wale ambao hawako radhi na dini yetu. Na tukiona marafiki zetu matendo yao sio mazuri, ni lazima tuepukane nao kwa sababu tunaweza tukaiga tabia zao ambazo zinakwenda kinyume na dini yetu.
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu yamkini kufuata dini ya rafiki yake, kwa hivyo muangalie unayemfanya rafiki." (Abuu Daawuud na Tirmidhiy)

6. TULALE KIISLAM

Tumalizie kwa kuona namna anavyotakiwa Muislam kuimaliza siku yake kwa kujipumzisha Kiislam. Muislam anatakiwa atie wudhuu kabla ya kulala, wudhuu unaendana na Sunnah ya kupiga mswaki. Ni vizuri ukaswali rakaa tatu za witri (kwa wasioamka usiku).

Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akienda kulala usiku anakusanya viganja vyake kisha akivipuliza na akivisomea Suratul-Ikhlaas, na Suratul-Falaq, na Suratu-Nnaas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani na usoni na mbele (akifanya hivyo mara tatu).
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ukienda kulala soma Ayatul-Kursiy mpaka uimalize kwani Mwenyezi Mungu Ataendelea kukuhifadhi wala hakukaribii shetani mpaka asubuhi"
Unapolala ulaze ubavu kwa upande wa kulia na usome du'aa ifuatayo:

اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وا جْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت
"Ewe Mwenyezi Mungu nimeisalimisha nafsi yangu kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nimeuelekeza uso wangu kwako na nimeutegemeza mgongo wangu kwako, kwa matarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila kwako, nimekiamini kitabu chako ulichokiteremsha na Mtume wako uliyemtuma".

Bila ya shaka tutakapoishi Kiislam tutakuwa mbali na wasiokuwa Waislam. Hivyo maisha yetu yatakuwa hakika ni ya Kiislam. Kila kitu yatakikana juhudi na inaanza kwa nafsi kujifunga kukubali mafundisho ya Kiislam. Inawezekana kubadilika kwa kuishi Kiislam. Anza sasa, katu usichelewe kuishi Kiislam.


 

Phlagiey

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
3,452
2,000
Kuna wakati inatulazimu kuishi aina fulani ya maisha kutoka na jamii tutokazo, kimsingi swala hili ndilo haswa linamfanya mtu aonekane tofauti anapofanya kitu tofauti na jamii yake, swala la msingi la kujiuliza je? jamii yako maisha inayoishi yapo kwa misingi na kwa matakwa ya nani? je wewe ukiamua kuishi maishi yako ambayo ni tofauti na wao utakuwa umemkosea huyo ambae jamii yako inashi chini ya misingi yake na matakwa yake.

Kama jibu ni hapana, utakapoamua kuishi maisha yako sio mbaya ila jambo la msingi ni kwamba uishi katika misingi hii;
(1)Amani
(2)Upendo
(3)Heshima n.k
Kuna wakati ukiamua kuchangua maisha yako upendayo inakubidi utoke nje ya maagizo mbali mbali na imani zinazo kufunga.
 

Tized

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
4,024
2,000
Karibu sana mkuu, pia asante kwa hekima zako, Ndio jamii yetu hio.

Inahitaji watu wanaoweza kufanya maamuzi na KUYASIMAMIA ili kuionesha jamii upande wa pili wa shilingi ukoje. Japo watasema na kuponda sana lakini kwa kuwa hujamkosea mtu na ni uamuzi wako binafsi.. UNASONGA MBELE.. na utashangaa baadae wakishakuelewa wanakua wa kwanza kuja kukupongeza ila ndio waliokuwa wapingaji wa kwanza kabisa.

Point kubwa naoiona.. UJASIRI, KUFANYA MAAMUZI NA KUUSIMAMIA HUO UAMUZI bila kuingilia haki ya wengine. Maana wanasemaga... katika hali yoyote, kitu BORA kabisa ni kufanya UAMUZI sahihi, cha pili bora ni kufanya uamuzi hata kama sio uamuzi sahihi. Na cha tatu ambacho ndio kibaya kupita vyote ni KUTOKUFANYA UAMUZI WOWOTE.


Tized umenifurshisha sana na hiyo analysis yako, kweli binadamu hatuna jema aisee.............
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom