Kasulumbai aunguruma Igunga

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
P1020060.JPG P1020070.JPG P1020062.JPG
Leo kumefanyika mkutano wa hadhara wa CDM Igunga.

Madhumuni ya mkutano huo ni kwa CDM kuwashukuru wananchi wa Igunga kwa hatua waliyofikia ya kubadirika na kukubaliana na mageuzi katika kupigania haki zao, Pia kasulumbai alisema CCM imeshindwa kuongoza kwani mfano halisi unajionyesha kwa jeshi la Polisi kwani hadi leo hawana makazi ya kudumu na wanapanga mitaani kitu ambacho ni hatari kutokana na kazi wanayoifanya.

Suala lingine na mpango wa serikali kuleta maji Igunga kutoka Ziwa Victoria amesema mpango huo ni mzuri kwa wananchi lakini serikali hii inawaandalia mazingira mazuri wawekezaji wa Madini ambao watakuja Igunga kwa ajili ya uchimbaji wa Madini ambayo kwa kiwango kikubwa watanufaika wao na sio wananchi wa Igunga.

Alitolea mfano ni Kahama kwani baada ya kuwepo wawekezaji ndo maana maji kutoka Ziwa Viktoria yamepelekwa huko. pia ametoa tamko kuwa CCM haitawweza kufanikiwa kwa propaganda chafu inazozifanya ikiwemo ya kutumia kifaa maalum cha kutuma sms kwa kutumia No. za wabunge wa CDM ili kuwatia hatiani kwamba wametuma SMS za vitisho kwa wabunge wa CCM na amesema wanasubiri suala hilo lipelekwe mahakamani na ndiyo watatoa ushahidi kuhusu suala hilo na ndipo hapo CCM watakapoumbuka.

Mwisho amewataka wananchi wa Igunga kuhakikisha wanachangia kuiondoa CCM madarakani hapo 2015 ili kuweza kukiweka chama ambacho kitawasaidia katika kuwaletea maendeleo na kulinda rasilimali zao na sio CCM inayomaliza rasilimali zetu na kunufaisha wachache.
 
Kuna mambo ya kuzungumza na mengine sio......CDM ni chama chenye ukomavu uliosababishwa na matatizo hewa ya CCM. Hakwenda kuomba huruma za wananchi kuhusu aina ya hukumu iliyotolewa.

Amekwenda kuwashukuru kwa uelewa wao na kupanga mikakati ya ushindi ujao wa kishindo.

CCM wanasali kabla ya kula chakula- Wanaomba na kubembeleza kabla ya kuchaguliwa....wachague uone (5yrs) ndo mtaonana tena.

CDM wanasali kabla na baada kula chakula- Wanaomba na kubembeleza kabla na baada ya kuchaguliwa.
 
igunga peopleeee power. Badilikeni. Hongera kamanda kasulumbai kuwapa dawa ya akili wana igunga
 
Mbona kakwepa luongelea hukumu yake?
Hilo suala halikuwa na muhimu kuliandika hapa, kuhusu kesi amesema amehukumiwa kwa sababu hukumu yenyewe ni nyepesi hakuona umuhimu wa kuipinga na amemaliza na sasa yupo kwenye mapambano na CCM wasitegemee kudhoofisha upinzani kwa kuwafungulia kesi kila wakati wajue hiyo ni kuwaongezea nguvu na kuwafanya wawe wakakamavu hiyo ni sawa na kumpiga chura teke ni kumuongezea mwendo. nafikiri AVANT umenipata
 
kwa mtaji huu ccm lazima iteketee maana nguvu ya serikali walionayo sasa wanachanganyikiwa jinsi chadema walivyo makini r.i.p ccm
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom