Kassim Majaliwa: Serikali imedhamiria kutekeleza dhana ya uchumi jumuishi kwa vitendo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
941
KASSIM MAJALIWA: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUTEKELEZA DHANA YA UCHUMI JUMUISHI KWA VITENDO

WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kutekeleza dhana ya uchumi jumuishi kwa vitendo kwa kuweka vipaumbele vitakavyowawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 4, 2021) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, jijini Dodoma. Amesema kuwa vipaumbele katika mipango ya Serikali vimekuwa katika utekelezaji wa shughuli za kiuchumi zinazowajumuisha moja kwa moja wananchi.

Waziri Mkuu ametaja baadhi ya vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na uimarishaji wa huduma za afya, hifadhi ya jamii, maji, umeme na utekelezaji wa mpango wa elimumsingi bila ada “Mtanzania mwenye afya, aliyeelimika na miundombinu wezeshi ni chachu kwa ukuaji uchumi wa nchi yetu.”

Amesema uwezeshaji wa uchumi jumuishi ni msingi wa kuhakikisha kunakuwa na ustawi endelevu kwa watu wote, ambapo Serikali imeandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 ambayo pamoja na mambo mengine imeainisha mazingira wezeshi yatakayowezesha nchi kunufaika kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 pia imelenga kuhakikisha kunakuwa na viwango vya juu vya maisha, amani na umoja, utawala bora na uchumi ulioimarika wenye ushindani katika jamii.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali imeandaa sera mbalimbali ambazo zimelenga kuhakikisha kunakuwa na maendeleo endelevu na uchumi jumuishi. “Kati ya Sera hizo ni Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 ambayo ni Sera kiongozi kwenye masuala ya kuwezesha wananchi kiuchumi, sera hiyo imeweka mikakati inayolenga kuhakikisha kwamba Watanzania wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi”

IMG-20211005-WA0041.jpg

IMG-20211005-WA0042.jpg

IMG-20211005-WA0043.jpg
 
Hizi ni ngonjera za kawaida za wanasiasa.

Uchumi jumuishi ni pamoja na kujumuisha matabaka yote yaliyotamkwa ktk katiba, ambapo kwa sasa ni Tabaka moja tu ndilo liloshika nafasi nyeti za maamuzi ikiwemo vikosi vya ulinzi na usalama.

Pm kama kweli maneno hata yanatoka chini ya moyo wake tutarajie matabaka yaliyoachwa nyuma yajumuishwe ktk idara za maamuzi. Wakiwemo watz wenye asili ya Asia.
 
Hizi ni ngonjera za kawaida za wanasiasa.

Uchumi jumuishi ni pamoja na kujumuisha matabaka yote yaliyotamkwa ktk katiba...
Kwenye bishara 80% ya mafanikio yanamtegemea mfanya biashara(mjasiriamali) lakini asilimia 20% ndiyo inanguvu ya kuua bishara hii kwakinyakyusa tunaita 'the entrepreneur and his environment' that include.

Social demographic variables,political and physical factors ' hii nimeandika kwenye kitabu changu cha ujasirimali, hapa vinavyo husika ni mabadiliko ya tabia nchi.

Siasa, magonjwa ya mlipuka kama uviko-19, nitaongeza uhasama wa kisiasa(political repression and hatred) and abuse of entrusted power (matumizi mabaya ya madaraka)
 
Ccm walishaishiwa maarifa siku nyingi,hakuna jipya hapo.
Kwenye uchumi jumuishi tunavitu vingi vya kurekebisha ,cha kwanza serekali kulipa madeni ya ndani kwa wakati,kutengeneza Sera shirikishi zinazo tumia muundo madhubuti,watunga Sera wawezeshwe kupitisha Sera na sheria mbazo zina tija,kutotumia Sera mpya kwa sheria za zamani ,maamuzi yanayo fuata sheria na haki
 
Kwa wewe unataka makabachori nayo yaingizwe kwenye majeshi? Halafu hayo maneno ya kuhalalisha haramu eti wasia wenye asili ya Tanzania wapi ulisikia watanzania wenye asili ya asia?
Thrn tukubali hakuna kitu kinachoitwa uchumi jumuishi. Zaidi kuna ngonjera za wanasiasa.

Lkn kama tunahitaji ujumuishi tutahitaji uwakilishi wa karibu matabaka yote yaliytajwa nfani ya katiba kuwa hayatobaguliwa.
 
Kwenye bishara 80% ya mafanikio yanamtegemea mfanya biashara(mjasiriamali) lakini asilimia 20% ndiyo inanguvu ya kuua bishara hii kwakinyakyusa tunaita 'the entrepreneur and his environment' that include.

Social demographic variables,political and physical factors ' hii nimeandika kwenye kitabu changu cha ujasirimali, hapa vinavyo husika ni mabadiliko ya tabia nchi.

Siasa, magonjwa ya mlipuka kama uviko-19, nitaongeza uhasama wa kisiasa(political repression and hatred) and abuse of entrusted power (matumizi mabaya ya madaraka)
Umesema wanaouwa biashara ni 20%. Kama unamaanisha 20% ya watz umewapa uwingi ambao hawana. Ni only 0.001% ndio wana power ya kuuwa biashara.

Ni kikundi cha wahuni hawazidi watu 6000.
 
Hizi ni ngonjera za kawaida za wanasiasa.

Uchumi jumuishi ni pamoja na kujumuisha matabaka yote yaliyotamkwa ktk katiba, ambapo kwa sasa ni Tabaka moja tu ndilo liloshika nafasi nyeti za maamuzi ikiwemo vikosi vya ulinzi na usalama.

Pm kama kweli maneno hata yanatoka chini ya moyo wake tutarajie matabaka yaliyoachwa nyuma yajumuishwe ktk idara za maamuzi. Wakiwemo watz wenye asili ya Asia.
Kumbe tabaka unalolizungumzia wewe ni Wenye asili ya Asia, ndio tabaka pekee lililoachwa nyuma?.

Kwa hiyo hapa unawazungumzia Wahindi au hata Wachina, Waindonesia, Phillipines n.k?.

Na je wao ni sehemu ngapi ya Watanzania milioni 60?. na kujumuishwa kwao ni mpaka waalikwe na serikali?....na vipi basi kuwaona wakishirikia hata kwenye timu zetu za soka ligi kuu, vibarua wa ujenzi, Machinga, Mama lishe n.k?.
 
Umesema wanaouwa biashara ni 20%. Kama unamaanisha 20% ya watz umewapa uwingi ambao hawana. Ni only 0.001% ndio wana power ya kuuwa biashara.

Ni kikundi cha wahuni hawazidi watu 6000.
Hujanielewa kabisaa duuu! pole sana,nimesema hivi asilimia 80% ya mafaniko ya biashara yoyote ile yanamtegemea mfanya biashara "will depend on personal qualities' lakini asilimia 20% ndiyo inanguvu kua biashara na nimekutajia visababishi, inatakiwa ujue pia kwamba biashara ni watu hela zao zinaweza kusababisha upate mafanikio ama vinginevyo ,hivyo basi mfanyabiashara inatakiwa ajipange kuweza kukabiliana nayo, kwenye hiyo aslimia 20 serikali (siasa), pia ina mkono wake,karibu tuelimshane zaidi maana hili ndilo eneo langu japo muda mwingi nautumia kwenye utengenezaji vifaa vya electronics, ambavyo vinanichangamusha akili
 
Haaminiki tokea siku kasema mwendazake yuko na afya njema. Ni muongo
Mimi tatizo langu zaidi ni kuwa anaongea utafikiri ni mradi tu anaongea.
Mengi ya anayoongea do not make sense.
Sasa hivi the burning issue ni the machinga problem nation wide.
Akiwa kiranja mkuu hatujamsikia akiweka malengo yoyote ya kutazamiwa na wananchi.

Katika komgamano hilo sijaona kuwa kaongelea any tangible steps kuwezesha wananchi kibiashara na kiuchumi, its the normal and usual rhetoric.
 
Kumbe tabaka unalolizungumzia wewe ni Wenye asili ya Asia, ndio tabaka pekee lililoachwa nyuma?.

Kwa hiyo hapa unawazungumzia Wahindi au hata Wachina, Waindonesia, Phillipines n.k?.

Na je wao ni sehemu ngapi ya Watanzania milioni 60?. na kujumuishwa kwao ni mpaka waalikwe na serikali?....na vipi basi kuwaona wakishirikia hata kwenye timu zetu za soka ligi kuu, vibarua wa ujenzi, Machinga, Mama lishe n.k?.
Watz wenye asili ya Asia ni sample kati ya matabaka yasiyojumuishwa. Nielewe sijazungumzia matabaka yaliyo achwa nyuma, Bali matakabaka yaliyobaguliwa. Serikali inaposema inataka kuunda uchumi jumuishi manake hapo inakiri kuwa mfumo wa uchumi wa sawa si jumuishi. Ndio maana Leo asilimia kubwa ya wasimamizi wa korosho ni wasukuma. Wenye korosho zao wamewekwa kando. Hawajajumuishwa.

Uchumi jumuishi utakuwa umeonekana kwa vitendo iwapo matabaka yote yaliyotajwa ndani ya katiba yanajunuishwa kwanza ktk teuzi za nafasi za kufanya maamuzi. Tofauti na sasa ni Tanaka moja tu ndilo linalofanya maamuzi kwa watz 60mil. Wahindi watz wakiwa wamesahaulika. Waarabubwatz wamesahalika.

Kujua maana ya uchumi jumuishi ingalie serikali ya sasa ya znz. Wahindi wamo, waarabu wamo, upinzani wamo, wakristo wamo. Matabaka yote yamejumuishwa sawa na popular yao.

Huku bara kabla ya kujua ni asilimia ngapi wa watz, au wanamchango gn kwa uchumi wa nchi. Kuna matabaka yamebaguliwa kabisa ktk teuzi. Huu huitwa uchumi wa kibaguzi
 
Back
Top Bottom