Kasie's Crush... He Crush on Me....

Kasie's Crush... He Crush on Me....

Ni kweli ila... mnazijua wenyewe looh.
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
aa7cee1142143f39cd354ed49eba32c5.jpg
 
Hello ladies and gentlemen,

Allow me to take this opportunity and give you a brief of what happens to Kasie yesterday evening.

Hili tukio limenifikirisha na kunifanya niwatazame wanaume kwa upya, kwa jinsi ninavowafahamu wanaume ya jana ilinishangaza kidogo. Labda waje watiririke hapa kueleza nini hasa huwajia akilini.

Kasie ni kibibi cha kukaribia kustaafu hivo hata mikunjo kwenye sura imeshajitokeza kwa wingi, ngozi ya mwili haijanyooka kama ya kischana au mtoto bali imeanza kusinyaa na misuli ya nyama za mwili imeanza kulegea. Tangu mwaka huu uanze ni wanja wa chini ya macho tuu ndo ambao bado unakubali, lipstick poa na mashedo yote ya uso yalishakataa.

Sasa jana nilitumwa kikazi ofisi ya Pretoria hivo nikaenda na Gautren sikutaka kuendesha ili nipumzike hivo nilitumia usafiri huo wa umma.
Saa ya kwenda nilienda vizuri saa ya kurudi ndo nikakutana na hii kasumba.

Wakati narudi ilikuwa saa moja na dakika kadhaa usiku nikakata ticket na kuingia kwenye seat yangu ya dirishani. Kabla treni halijaondoka akaja kijana mmoja hivi akakaa siti ye mbele yangu hivo tukawa tunatizamana. Nasema ni kijana kwasababu muonekano wake ni kati ya umri wa miaka 28 - 34 hivi. Mie nilikuwa busy na simu yangu naperuzi JF yule kijana alianza kunitizama kila nikimuangalia ananitizama mmhhh nikasema hapa iko namna. Akaanza kunyoosha miguu yake ikawa inagusana na yangu kama vile ananistua kitu ..... mie nikaona ule mseti wote ulivokuwa nikasema ngoja nijikaushe kama sisikii kitu nione mwisho wake utakuwaje.

Nilipofikia Sandton mie nikateremka huyo kuelekea madaladala yalipo na nilifanya makusudi hivo ili nione atanifata? Hehehehehhee wajua yule kijana alinifata sasa mie niko mbele yeye nyuma wala hakunisemesha kitu, ile nafika kwenye daladala nimeingia kumbe siti yangu ndo ikawa ya mwisho akaja akamuuliza dereva hivo daladala inaenda wapi? Akajibiwa imeshajaa hahahahahhaa daah hadi nikamuonea huruma.

Akabaki pale chini na akaonekana hata haelewi aende wapi... nikajisemea huyu yawezekana alikuwa haendi huku Sandton ila kushuka huku kunifatilia tuu daah.
Basi kituo cha daladala kilichofuata mie nikashuka nikachukua taxi hadi nyumbani. Nikipoingia kwwnye taxi nikaendelea kukukwaza yule kijana na kufikiria......

Hivi wanaume wanapokutana na mwanamke ambaye on the first place au kwa muonekano wa kwanza sio mzuri au havutii kw maana ya sura na shape kama Kasie nilivo na uzee huu... sasa kinachomfanya aanze kutongoza tena kwa kunigusa gusa miguu yangu kwa miguu yake.... ni kuwa anajifunza kutongoza? Ana stress kiasi kwamba mwanamke yeyote ajaye mbele yake atamtongoza? Ni tabia tuu ya mtu husika kutongoza mwanamke yeyote? Au alishakuja na sulika za hali ya juu hivo anavaa mwanamke yeyote a jaribu kutongoza akikubali apige kazi?

Ni kipi haswa... mbona waschana wazuri wapo?

Pole wee kijana kiukweli hata ungeniongelesha nisingekubali.... basi tuu ukorofi wa kas6ie.

Alhamis njema nyote.

Kasinde.
HaaAh et ukorofi wa KASIE .

HUONI ULIVYO MZURI,MREMBO JAPO UMRI UMEKUTUPA?


Hakika WEWE ndo waleeee,waliotungiwa msemo wa AGE JUST A NUMBERS.[emoji7] .



Hapa tuu JF,kwa mwandiko na maneno yako,TUPO WENGI TUNAKUP........[emoji7] [emoji106] .

"love me n I will live in your heart,hate me n I will be remembered in yo mind" Priceless Soul(Kasies' Hz)
 
Hahaaa. Dada yangu wa Kinyamwezi katika ubora wako mwenyewe.

Siku zote kuna vitu huwa vikitokea vinakuwa ni kama kikohozi yaani mtu anaweza jizuia ila mwisho wa siku inashindikana. Na ndio ilivyokuwa kwa huyo Kaka sasa.
Mapenz kama kikohoz ukifcha,itabumbulika.
 
Ni kweli usemacho Sam.... kiufupi yule kijana alinitamani na si kama alinipenda on the first place. Maana hapo do nashangaa si rahisi umpendae mtu ilhali hana mvuto wa macho....

Mie ni mzee nahua kuna wazee wanazeeka na uzuri wao ila Kasie sio.... kunyanzi zimeanza kama kinyago cha mmakonde. .. manyama uzembe kibao na ngozi haina nuru yaani mvuto sifuri ndo maana najiuliza kipi haswa kilimvutia.... au ndo alitamani chupa ilale?
MM napenda hvyohvyo aiseee.Umenigusa hadi mwili umesisimuka my KASIE
 
Ni kosa kubwa sana Kasie kujidharau, usinielewe vibaya, ni kweli unazeeka lakini haimaanishi ule uzuri wako unapotea, usiruhusu mawazo na hisia zako zikakunyanyapaa. Umesahau unavyojiona wewe nafsini mwako ndivyo unawafanya na watu wengine wakuone hivyo?

Sam, sio kuwa maji dharau bali nausema uhalisia kuwa nimezeeka hivo ule mvuto wangu nikiwa mschana haupo tena. Nashindwa muelewa mwanaume anayenitongoza. ..... what's is he into.... am a mere normal woman out there....
 
Ni kwa vile tu wewe unapenda kufunguka na kufurahia maisha, kila mtu angeeeleza mikasa yake hapa, mngeshangaa wanaume tunavyohitaji maombi na huruma. Kuna vitu unafanya akili na roho vinakwambia kabisa hii sio sawa...lakini hapohapo unaendelea kujisokomeza...acheni tu tuitwe wanaume.

Kwakweli poleni na hongereni hapohapo.
 
HaaAh et ukorofi wa KASIE .

HUONI ULIVYO MZURI,MREMBO JAPO UMRI UMEKUTUPA?


Hakika WEWE ndo waleeee,waliotungiwa msemo wa AGE JUST A NUMBERS.[emoji7] .



Hapa tuu JF,kwa mwandiko na maneno yako,TUPO WENGI TUNAKUP........[emoji7] [emoji106] .

"love me n I will live in your heart,hate me n I will be remembered in yo mind" Priceless Soul(Kasies' Hz)

Hahahahhaa looh asante kwa kunipenda, love you back all.
 
Oohh sasa ntafanyaje maana sijui ntamuona wapi tena.....
Bila shaka una alternatives za kumpata yule,sasa ukimwona utatakiwa umwanze wewe
(Karma-whats goes around,come around)

HIS LOVE=YOUR NEED.
-FIND HIM.
 
Sam, sio kuwa maji dharau bali nausema uhalisia kuwa nimezeeka hivo ule mvuto wangu nikiwa mschana haupo tena. Nashindwa muelewa mwanaume anayenitongoza. ..... what's is he into.... am a mere normal woman out there....
Wengi hao ni mamario tu achana nao! Anyway siku hizi vijana wanapenda nyie nasi kama kawa tunalea wajukuu miaka 12 na nusu
 
Back
Top Bottom