Katibu wa bunge bwana Kashillillah aliita waandishi wa habari kuelezea minyukano iliyojitokeza katika mkutano wa 3 wa bunge hili la 10, aliuleza umma kwamba kilichosababisha ni ugeni wa wabunge na sio udhaifu wa Spika. Alienda mbali zaidi kutolea mfano wa mbunge wa Arusha Mh. Godbless Lema kwamba kitendo chake cha kusema 'funga mlango tupigane' kinatokana na uchanga wake bungeni na kwamba hana wala hajasoma kanuni za bunge. Maoni yangu ni kwamba katibu hajamtendea haki Mhe. Lema kwa sababu
1. Ni wabunge wengi ambao walijibizana maneno wakiwemo wakongwe na mawaziri (tulisikia wengine wakisema 'atoke nje');
2. Si kweli kwamba mhe. Lema hana kanuni za bunge;
3. Kila bunge jipya huja na wabunge wapya lakini haya hajajitokeza huko nyuma;
Mtazamo wangu ni kwamba yaliyojitokeza ni mwanzo tu wa kuonesha dhahiri kwamba spika wa sasa hakuwa amewiva vya kutosha kuvaa viatu vya Sitta. Aidha kitendo cha ufafanuzi huu kutolewa na katibu wa bunge ni ushahidi mwingine kwamba Spika kashindwa. Naomba kuwasilisha.
Bwana Zulu ndiye PRO wa bunge letu. Sijamsikia akijibu hoja yoyote kwa wanahabari tangu bunge hili lianze.
Kama Kashilila aliwajibibka kutoa ufafanuzi kwa mambo yanayotokea bungeni, kwa nini amechelewa sana. Watu wamejadili hadi wamesahau yeye ndo anaibuka na kutudanganya tena. Je, ni mzembe?
Kwenye kikao cha February, kuna mdada mbunge mmoja alikuwa anagombea uwakilishi wa vyuo vya elimu ya juu. Ofisi ya Kashilila ilikiuka kanuni na kumfanyia mizengwe huyu dada. Katika hotuba yake bungeni dada huyu alijitoa na kuitupia lawama ofisi ya Kashilila. Ilirushwa live na TBC na Star tv.
Kashilila hajajibu tuhuma za huyu dada hadi leo. Kama kuna ushahidi huu kwamba Kashilila AMA hazifahamu kanuni na au amezipindisha, je Kashilila ni mgeni bungeni? Je, hana elimu ya kutosha?
Yaani ina maanisha kuwa Wabunge waogope kusema eti kwa sabau wanaogopa Karani wa Bunge atachukuliaje maneno wanayosema. Sijawahi ona bangi mbichi kuliko hii!!! Kazi ya Kashishila ni kupanga ratiba ya vikao na kuhakikisha Mjengo una-function. Yeye siyo Mbunge na wala siyo Spika.
Yeah, I believe this woman (In bold red) could make the best Speaker than the current - Anna Makinda who unlike her predecessor Samuel Sitta has proved to be totally incompetent. The same is the case with her Deputy; Kashililla who fits more in the shoes of the propaganda platform of the worn out, exhausted and dilapidated CCM.Ni hivi majuzi tumesoma kwenye baadhi ya magazeti kuwa Mwanasheria mkuu aliitwa kwenye vikao vya CCM kule Dodoma wakati inafanya madaliko katika safu ya uongozi. Na watu walihoji inakuwaje mwanasheria wa Serikali anashiriki kwenye vikao vya chama cha siasa?
Sasa Leo Katibu wa Bunge anaita waandishi wa habari na kuanza kuelezea 'upya' wa wabunge pamoja na madai kwamba baadhi yao hawazijui kanuni! Naomba kama kuna mtu mwenye job description ya katibu wa Bunge atuwekee hapa jamvini ili tujue katibu ana mamlaka gani na anawajibika kwa lipi?
Hizi kanuni za bunge zimekuwa zikiongelewa sana na Mama Makinda na sasa Katibu wa bunge kama some sort of holy gray! Na kuna uwezekano kabisa kuwa walipania kuzipindisha lakini kwa bahati mbaya hawa wabunge 'wapya' ambao wengi wao ni wanasheria wamewazidi 'maarifa' plus wameonesha kuwa kanuni za bunge ni taratibu na lazima zimesomwe pamoja na sheria mama ya nchi yaani katiba.
Mis-calculation ya kuweka Spika, naibu spika na katibu wa bunge ambao wote si wanasheria ndio mwanzo wa sokomoko bungeni. Kashilila aache kuhubiri porojo maana watanzania tumeona zomea zome na mipasho bungeni tofauti kabisa na kipindi kingine chochote hasa kipindi cha Spika Sitta. Kama taifa ni aibu kuona tuliyoona na nadhani ingekuwa busara kwa watu kama wakina Kashilila kuwa na different attitude wanapokaa kwenye viti vya uongozi badala ya kuja na excuses. Mbona kikao alichoongoza Mh. Jenista Mhagama kilikuwa na nidhamu nzuri? Fair play.
Kwanza nadhani aliyetamka maneno 'funga milango tupigane' sio Lema, ni mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe Haule. Sielewi kwanini lema anahusishwa na ile kauli
Angemsamehe Lema bure kwani Lema ni form four, aliyepata division four points 29, sasa unategemea nini?