victor shio
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 651
- 109
Mimi mambo yake ya uzinzi hayanihusu hata kidogo. Hayo ni mambo yake na mkewe.
Kweli mkuu wanaoingilia kuna viereere wanajidai wana wivu kuliko mkee wake.
Mimi mambo yake ya uzinzi hayanihusu hata kidogo. Hayo ni mambo yake na mkewe.
Kwa sababu ni mkataba baina ya mume, mke na jamii waliyopo.
Ndoa is public, ni mkataba unaotakiwa uwe published in public records.
There's always a public interest in any marriage .... a wedding can be private.
Ndoa siyo jambo binafsi.
Hivi kuwa FISADI lazima uiibie Tanzania au ule pesa za serikali??? Hata huyu kiongozi mzinzi ni FISADI pia kwani ameihujumu familia yake na jamii anayoingoza. TAFAKARINakumbuka Nyerere aliwahi kusema, kiongozi mzinzi hafai kuongoza nchi!
KATIKA kile kinachoonekana kama kumsafisha Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe dhidi ya kashfa ya uzinzi inayomuandama.
Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tindu Lissu amesema suala hilo ni maisha binafsi ya mtu, ambayo hayawezi kuhusishwa na wadhifa wake kwa namna yoyote.
Nashangaa sana Watanzania badala ya kushughulikia maswala ya kupanda Kwa bei ya vitu kama umeme na mengineo wamekalia kuongea mambo binafsi ya watu
Viongozi wa CHADEMA ni majanga tupu.
Kwa hiyo kumbe Mh. Mbowe ni mzinzi kwa maana nyingine, tuhuma hizi ni za kweli.
Sasa kama maswala ya Uzinzi ni private affairs. Vipi hili swala la kupewa millions pesa za Tanzania na wale wale kila mara alikuwa akipanda kwenye majukwaa alikuwa anawaita mafisadi.
Pesa za huyu kada wa CCM alizochukua nazo ni private affairs
View attachment 132573
Tunaomba tufahamu mipaka ya private affairs nchini
Kama ameweza kuijibu hoja ya uzinzi, kwa nini hakutaka kuijibu hoja ya "double agent" kwa maana kuwa, mchana ni mpiga vita mafisadi na usiku ni mpokea pesa za mafisadi
Mimi ni muumini wa CDM na mshabiki mtiifu kwa Mbowe,hata kama ndoa ni jambo la binafsi lkn kwanini akubali kuingia kwenye hizi kashfa kizembe namna hii,CDM inawindwa kila kona,kosa kidogo maadui wanalishikia bango,binafsi nawaomba viongozi wa CDM kuachana na mambo yanayozua maswali kwa jamii...........CDM malizeni hili la Zitto tusonge mbele.