Kashfa ya Uzinzi: Lissu amsafisha Mbowe

Status
Not open for further replies.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125

Ojuku Abraham na Jelard Lucas

KATIKA kile kinachoonekana kama kumsafisha Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe dhidi ya kashfa ya uzinzi inayomuandama.

Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tindu Lissu amesema suala hilo ni maisha binafsi ya mtu, ambayo hayawezi kuhusishwa na wadhifa wake kwa namna yoyote.

Akizungumza katika mahojiano maalum ndani ya chumba cha habari cha Global Publishers Ltd, Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam juzi, Lissu alisema kwa kadiri anavyofahamu, suala hilo ni binafsi linalopaswa kuachwa chumbani, kwa sababu kama litahusishwa na nafasi yake, ni sawa na kukubali kuwa mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini si lolote wala chochote.

“Maisha ya kimapenzi ya mzee Mandela yalikuwa ya ukakasi, kwa maana hiyo unataka tuseme kuwa kwa sababu hiyo, mzee huyu hakuwa kiongozi bora, unataka tuseme Bill Clinton wa Marekani hakuwa kiongozi bora kwa sababu tu alipata kashfa katika moja ya makorido ya Ikulu ya White House? Mimi nadhani haya mambo kama yapo au hayapo, hayahusiani na uwezo wa mtu kiuongozi, ni mambo ya chumbani yanayopaswa kuachwa huko,” alisema Lissu.

Lissu alikuwa akirejea baadhi ya sababu zilizosababisha mgogoro kati ya chama chake na Naibu Katibu Mkuu wao aliyetimuliwa, Zitto Kabwe, anayedaiwa kushiriki kuandaa waraka wenye nia ovu, ambao pamoja na mambo mengine, ulitaka kufanyika kwa mabadiliko ya viongozi wa juu, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, kwa kudaiwa kuwa na elimu ndogo pamoja na kukosa uaminifu katika ndoa yake.

Aidha, hivi karibuni wakati wa kikao kilichomalizika cha Bunge mjini Dodoma, Freeman Mbowe alidaiwa kuvuruga ziara ya mbunge mmoja mwanamke (wa viti maalum) wa chama chake aliyekuwa katika ziara ya kibunge nje ya nchi, na badala yake kumtaka kuungana sehemu alipokuwepo.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki, licha ya kukiri kuwepo kwa mgogoro unaokitikisa chama chao, lakini alisema hatimaye Chadema itashinda na kubakia imara na akasisitiza kuwa mwavuli wa mahakama alionao Zito ukiondoka, watamtimua.

Chanzo: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/lissu-amsafisha-mbowe
 
Attachments

  • lissu.jpg
    lissu.jpg
    31.3 KB · Views: 2,477
  • mbowe.jpg
    mbowe.jpg
    18.7 KB · Views: 2,690
Nashangaa sana Watanzania badala ya kushughulikia maswala ya kupanda Kwa bei ya vitu kama umeme na mengineo wamekalia kuongea mambo binafsi ya watu ama kweli ndio maana nchi haiend mbale kila uchao inarudi nyuma tu mara utasikia ati hakuna kazi siku mbili Kwa ajili ya sikukuu ya Mapinduzi tena ya Zanzibar ambayo ni nchi na isitoshe Tanganyika waliwapa sappoti siku ya kilele lakini cha ajabu serikali ya Tanganyika ati nayo imetangaza kupumzika Kwa siku mbili lol aibu gani hiyo kupoteza mamilion ya shilingi Kwa mamabo ya Zanzibar.Ulaya kuna vongozi ambao ni maGAY lakini wanachapa kazi vibaya sana Kwa maendeleo ya nchi zao na wananchi wala hawahoji mambo yao ati mbona kiongozi Yule ni GAY na hiyo yote Kwa kuwa ni mambo yake binfsi yeye atabeba msalaba Wake mwenyewe so wajameni tuache kuingilia mambo binafsi tujikite Kwa mambo yenye tija na Taifa letu
 
Viongozi wa CHADEMA ni majanga tupu.

Kwa hiyo kumbe Mh. Mbowe ni mzinzi kwa maana nyingine, tuhuma hizi ni za kweli.

Sasa kama maswala ya Uzinzi ni private affairs. Vipi hili swala la kupewa millions pesa za Tanzania na wale wale kila mara alikuwa akipanda kwenye majukwaa alikuwa anawaita mafisadi.

Pesa za huyu kada wa CCM alizochukua nazo ni private affairs

View attachment 132573

Tunaomba tufahamu mipaka ya private affairs nchini

Kama ameweza kuijibu hoja ya uzinzi, kwa nini hakutaka kuijibu hoja ya "double agent" kwa maana kuwa, mchana ni mpiga vita mafisadi na usiku ni mpokea pesa za mafisadi
 
...Dhu!! gamba hili ....king taratiiiiiiiiiiiiibu
 
Ndugu yangu suala la uzinzi japokuwa sikubaliani binafsi na tabia hii hasa kwa viongozi wa umma na hata jamii kiujumla, lakini jambo hilo limekuwa tatizo kubwa kwa jamii yetu, ninaamini ni watu wachache sana tena sana ambao hawana kashfa hii, sina hakika kama wewe pia huna. Ebu jaribu kuwa mkweli wewe ni mwaminifu kweli kabisa katika jambo hilo?
 
Clinton alikuwa impeached, Mandela alichapiwa kwa hiyo hakufanya jambo la kipuuzi kama alilofanya Mbowe.
Kama katiba ya CDM inatilia mkazo famili kama ndiyo kiini cha utawala (conservatives pillar) basi waonyeshe mfano na siyo kuweka vifungu kwenye katiba yao ili wapte wafadhili ilhali ni chma cha wasiooa na waasherati.

Tundu Lissu amejishusha.
 
Viongozi wa CHADEMA ni majanga tupu.

Kwa hiyo kumbe Mh. Mbowe ni mzinzi kwa maana nyingine, tuhuma hizi ni za kweli.

Sasa kama maswala ya Uzinzi ni private affairs. Vipi hili swala la kupewa millions pesa za Tanzania na wale wale kila mara alikuwa akipanda kwenye majukwaa alikuwa anawaita mafisadi.

Pesa za huyu kada wa CCM alizochukua nazo ni private affairs

View attachment 132573

Tunaomba tufahamu mipaka ya private affairs nchini

Kama ameweza kuijibu hoja ya uzinzi, kwa nini hakutaka kuijibu hoja ya "double agent" kwa maana kuwa, mchana ni mpiga vita mafisadi na usiku ni mpokea pesa za mafisadi
unaweza kuthibitisha kuwa mbowe alipokea pesa kutoka kwa hao unao wadai kumbuka hata aliyeanzisha huo uongo anajuta na kwenye twitter haukukaa hata dakika tano akawa amefuta kama angekuwa na ushahidi asingefuta..
 
kama raisi wsko alisema swala la uraisi ni binafsi iweje swala kugonoja lisiwe binafsi...
Rais alishasema mvua inaletwa na mungu ....
kiherehere cha vigoli ndiyo kinchowapa mimba

Huyo pia ni rais wako wewe na Lema, ila usimwamini kwa sababu rais haihitaji board certification, siyo kazi ya kitaalam.
 
viongozi wa chadema ni majanga tupu.

Kwa hiyo kumbe mh. Mbowe ni mzinzi kwa maana nyingine, tuhuma hizi ni za kweli.

Sasa kama maswala ya uzinzi ni private affairs. Vipi hili swala la kupewa millions pesa za tanzania na wale wale kila mara alikuwa akipanda kwenye majukwaa alikuwa anawaita mafisadi.

Pesa za huyu kada wa ccm alizochukua nazo ni private affairs

View attachment 132573

tunaomba tufahamu mipaka ya private affairs nchini

kama ameweza kuijibu hoja ya uzinzi, kwa nini hakutaka kuijibu hoja ya "double agent" kwa maana kuwa, mchana ni mpiga vita mafisadi na usiku ni mpokea pesa za mafisadi

hakuna kizuri kama siraha ya adui vitani. Nenda jkt utajuzwa. Mafisadi tutawaondoa kwa mbinu zote na baadae kutaifisha kitakachokuwa kimebakia. Kwa kuwa ww ni mtoto wao ipate hivyo. Hutakuwa na cha kurithi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom