Kashfa ya rushwa bungeni; Kamati yawatia hatiani wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya rushwa bungeni; Kamati yawatia hatiani wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Raia Mwema | Toleo la 260 | 26 Sep 2012


  KAMATI ya Bunge iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali (mstaafu), Hassan Ngwilizi, imewatia hatiani baadhi ya wabunge waliokuwa wakituhumiwa kuhusika katika kashfa ya kuikwamisha kwa njia ya rushwa, bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Raia Mwema, limebaini.

  Uchunguzi wa kamati hiyo ambao Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amekataa kuuzungumzia akisisitiza hilo ni suala ambalo bado lipo katika mchakato wa utendaji wa Bunge, umebaini kuwa baadhi ya wabunge akiwamo Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Tambwe, wamekuwa wakifanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).


  Tambwe na baadhi ya wenzake ndiyo waliokuwa mstari wa mbele kumtetea Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando, aliyesimamishwa wadhifa huo ili kupisha uchunguzi wa matumizi mabaya ya madaraka pamoja na tuhuma za rushwa katika shirika hilo pekee la uzalishaji na usambazaji umeme nchini.


  Munde na baadhi ya wenzake wamebainika kuwa na maslahi katika TANESCO, hususan na menejimenti iliyosimamishwa. Wamebainika kufanya biashara na TANESCO, uhusiano wa kimaslahi ambao unathibitisha kashfa iliyorindima na kuwahi kushikiwa bango na baadhi ya wabunge, akiwamo Mbunge wa Viti Maalumu, Vicky Kamata, aliyekuwa akisisitiza kwamba wapo wabunge katika Kamati ya Nishati na Madini, wanaonufaika na ‘ufisadi' uliomo TANESCO.


  Vicky Kamata ni kati ya wabunge waliokuwa mstari wa mbele kupinga baadhi ya wabunge wenzao waliokuwa wakishinikiza uongozi wa Wizara ya Nishati utiwe shinikizo la kujiuzulu kwa sababu, pamoja na mambo mengine umemkandamiza Mhando na menejimenti ya TANESCO kwa ujumla.


  "Wabunge Munde na baadhi ya wenzake waliokuwamo katika Kamati ya Nishati iliyovunjwa , na hata aliyekuwa Mwenyekiti, Selemani Zedi wamekutwa na makosa katika Kamati ya Ngwilizi. Wengine walikuwa na mgogoro wa kimaslahi kutokana na kunufaika na menejimenti ya TANESCO ambayo walikuwa wakiitetea kiasi cha wao kutishia kuikwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, wakihoji ni kwa nini Mkurugenzi Mtendaji alisimamishwa kazi," kinaeleza chanzo chetu cha habari.


  Kutokana na kuwapo kwa taarifa hizo za wabunge hao kupatikana na hatia, zipo taarifa nyingine zinazodai kwamba kuna juhudi za kuchakachua matokeo ya uchunguzi wa kamati hiyo. Hata hivyo, taarifa hizo hazikuweza kuthibitishwa na Naibu Spika, Ndugai katika mawasiliano ya simu yaliyofanyika kati ya mwandishi wetu na Naibu Spika huyo, ambaye hakuwa tayari pia kuthibitisha au kukataa wabunge hao kukutwa na hatia katika uchunguzi uliokwishakamilishwa na Kamati ya Ngwilizi, kama chanzo chetu cha habari kilivyoeleza.


  Ndugai alimwambia mwandishi wetu; "Hilo suala bado lipo katika mchakato wa Bunge, si wakati wake kulizungumza kwa sasa. Sina kingine cha kusema zaidi ya hayo. Wananchi watajulishwa wakati ukifika, ripoti hiyo haiwezi kuwa siri."


  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Kamati ya Ngwilizi imependekeza hatua za kuchukuwa dhidi ya wabunge hao na ni juu ya Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye aliunda kamati hiyo ya uchunguzi, baada ya kuivunja Kamati ya Nishati na Madini iliyokuwa ikitihumiwa, kuamua kutekeleza ushauri wa kamati hiyo au la.


  Spika Makinda ndiye aliyeivunja Kamati ya Nishati na Madini, kamati ambayo ni ya kwanza kuvunjwa kwa kashfa ya rushwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Imefichuliwa na uchunguzi wa kamati kuwa baadhi ya wabunge hao wamekuwa wakifanya biashara na TANESCO lakini pia wangali wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ambayo hata hivyo, baada ya baadhi ya wajumbe wake kutuhumiwa kupokea rushwa ili kuikwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliivunja kamati hiyo kutokana na wito wa wabunge wengine wasiokuwa wajumbe wa kamati hiyo.


  Kabla ya Spika Makinda kuivunja kamati hiyo katika Bunge la Bajeti lililopita, wabunge kadhaa walitoa hoja ya kutaka kamati hiyo ivunjwe, huku mazingira ya wakati huo yakiwa yanaashiria Bunge kugawanyika, lakini wengi wa wabunge wakiwapinga wenzao waliokuwa wakituhumiwa kupewa fedha za baadhi ya mafisadi ambao walikuwa wakiathiriwa na uamuzi wa uongozi mpya wa Wizara ya Nishati na Madini kudhibiti mianya ya ufisadi TANESCO.


  Kamati hiyo iliyovunjwa ilikuwa ikiundwa na wajumbe zaidi ya 20 ambao ni pamoja na Mwenyekiti wake, Selemani Zedi na Makamu mwenyekiti, Diana Chilolo.


  Wengine katika kamati hiyo ni Profesa Kulikoyela Kahigi, Yusufu Haji Khamisi, Mariam Kisangi, Catherine Magige, Dk. Anthony Mbassa, Abia Nyabakari, Charles Mwijage, Yusufu Nassir, Christopher Ole Sendeka na Dk. Festus Limbu.


  Wajumbe wengine waliokuwamo katika kamati hiyo iliyovunjwa kwa tuhuma za rushwa ni Shafin Sumar, Lucy Mayenga, Josephine Chagulla, Mwanamrisho Abama, David Silinde, Suleiman Masoud, Kisyeri Werema Chambiri, Munde Abdallah, Sara Msafiri, Vicky Kamata na Ali Mbaruk Salim.


  Sakata hilo la kuvunjwa kwa kamati liliambatana na vijembe kati ya wabunge kwa wabunge, ambako Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliwataja kwa majina wabunge wenzake kwamba wamehusika katika kupokea rushwa na wabunge aliowataja ni Mbunge wa Simanjiro, ole Sendeka, ambaye naye alikanusha na kutaka Bunge lichukue hatua zaidi kutokana na yeye pamoja na wabunge wenzake kutajwa na Lissu.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa Hayo Majina yatakuwa SIRI ? Wezi wanafichwa hata Majina wananchi hawawezi kuyaona ?
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh Vicky Kamata!!!!!! Ripoti kama itamtaja kwa kosa nitashangaa!!!! Ataambiwa ni maslahi binafsi? Yapi?
   
 4. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du Sendeka na Limbu wamo!! Hii sasa quishney watapiga kelele tena?
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mbona habari hii imekaa kiudaku zaidi..Hivi kweli inawezekana kuwa tayari habari zimekwisha leak hata kabla ya kamati kumaliza kazi yake? Je sii kuonyesha jinsi watu wetu walivyokosa Uzalendo ktk majukumu walopewa kiasi kwamba mtu anaweza kusambaza habari kama hii mbele ya maamuzi yalofikiwa na Kamati..

  Haya tuseme mathlan kuna ukweli ktk habari hii nakuwaje huyu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na madini ambaye kaishika kazi hiyo hata haikuchukua miezi sita tayari awe mkisiwa tayari kwa kufaidika na TANESCO badala ya Naibu waziri January Makamba ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti?.

  Hii habari inaonyesha wazi mchezo ule wa kisiasa baina ya Wanasiasa na watendaji wa serikali zetu. Na nadhani kutokana na ULAJI tumeyaona haya yakitokea sana wakati huu wa Utawala wa JK ambapo nina hakika WMawaziri na Wakurugenzi wamekuwa wakitofautiana sana ktk utekelezaji wa kazi na hii inatokana na mirija iliyopo au inayoandaliwa...Vita ya Wanasiasa vs wataalam itaendelea hadi pale mfumo bora wa kiutawala utakapo jengwa.
   
 6. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,320
  Likes Received: 1,495
  Trophy Points: 280
  Ningependa moderators waweke kitufe cha unlike, kingekuwepo mchango wako nike unlike mara kadhaa, unaongea kama sio Mtanzania, unataka siri ya ufisadi iwe inatunzwa? Hivi uliisha jiuliza kwanini watu wengu hutembelea humu jamvini? sababu ni hiyo hiyo, hapa ufisadi haufichwi, wanachama wa humu wapo everywhere, wakihisi kuna harufu au ushahidi fulani wa kifasadi unataka kutokea au umetokea na wahusika wanataka iwe siri tu, watu wanaruka nao hewani, safi sana Raiamwema na chanzo chenu cha habari!
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  habari hii imeandikwa kwa ujinga wa hali ya juu....ndio magazeti ya tanzania haya???
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wanaficha nini hapo si wataje tu
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  hapo kwenye red, naona in an opposite direction! Naona uelewa wako ndio upo hivyo ndio maana ukaiona hii habari that way!
   
 10. r

  raymg JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili suala lipo kibunge zaidi...so sio vizur kulijadri saiz!
   
 11. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Habari iko too vague!
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hii habariimetawanyika sana
   
 13. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Vicky Kamata si ana mtoto na naniluhu nyie?????????????????
   
 14. a

  afwe JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Polepole Edson, habari kwako ni nini? kama imekugusa jipe subira kwani kama ni ujinga si utajulikana soon!
   
Loading...