Kashfa ya Richmond: The FACTS

Wabunge wa CCM hawana uhuru wa kutoa hoja binafsi bungeni mpaka ziruhusiwe na viongozi mafisadi wa chama chao ili kulinda maslahi ya chama hicho.

Posted Date::4/16/2008
Kanuni mpya yawafunga mdomo wabunge
*Yawataka kupitishia hoja zao kwenye vyama
*Makinda alieza kwanini hoja ya Rostam ilizuiwa

Na Ramadhan Semtawa, Dodoma
Mwananchi

MOJA kati ya kanuni mpya za Bunge ambazo zimeanza kutumika katika mkutano unaoendelea mjini Dodoma, inawafunga mdomo wabunge kwasababu kuanzia sasa watalazimika kupitisha hoja zao binafsi kwenye kamati za uongozi za vyama vyao.

Kanuni hiyo mpya iliibua mjadala mkubwa bungeni jana baada ya Naibu Spika, Anna Makinda kuitolea ufafanuzi kufuatia baadhi ya wabunge kuozungumzia hoja zao katika vyombo vya habari, kabla ya kuzipitisha kwenye kamati za uongozi za vyama vyao kupata baraka.

Makinda pia alinukuu kanuni ya 110, ambayo imewekwa mahususi kwa ajili ya kuviwezesha vyama kujiwekea utaratibu bora wa kuratibu masuala ya vyama vyao, pamoja na kushughulikia masuala mbalimbali yanayokusudiwa kuwasilishwa bungeni.

Alisema utaratibu huo upo katika mabunge yote ya Jumuiya Madola, ambayo ndiyo wakati mwingine huwezesha kambi moja kususa na kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge.

Makinda aliongeza kwamba, azma ya kuweka kanuni hiyo ni kuwezesha uwajibikaji wa pamoja kichama bungeni(Collective Responsibility).

Kanuni hiyo inataka mkakatika kifungu cha kwanza (1) kwamba: Kamati za vyama vya siasa bungeni zitajiwekea utaratibu kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zake, inasema nakuongeza katika sehemu ya pili (2) kwamba:

Majadiliano yote kwenye mikutano ya kamati na mengineyo yanayohusu Kamati hizo yatakuwa na hadhi, kinga na nafuu zote zinazotolewa kwa mujibu wa sheria kuhusu majadiliano, kumbukumbu na mambo mengineyo ya Bunge na Vikao vyake kwa mujibu wa mashariti ya Ibara ya 100 (1) na (2) ya Katiba na Sheria ya Kinga, Madarakana Haki za Bunge.

Kutokana na maelezo hayo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe alisimama na kumtaka Naibu Spika kwanza, aeleze maslahi yake kutokana na kwamba yeye ni mjumbe wa Kamati hiyo ya CCM.

Pia Zitto aliwatetea wabunge hasa wa CCM akisema kuwa mara nyingine kamati za vyama zinanyima wabunge demokrasia katika kuwasilisha hoja na maelezo yao, kwa kutumia njia mbalimbali zinazokubalika bungeni.

Wakati Zitto akieleza hayo huku akiwatetea wabunge wa CCM, wabunge wa chama hicho tawala waliku wawakiguna:, Mmh!, huku wakionekana kumkejeli.

Hata hivyo, Makinda alijibu akisema amezungumzia kanuni na wala si mambo ya chama kama ilivyoelezwa na Zitto na kufafanua kimaslahi, hakuna asiyejua kama yeye na Spika wanatoka CCM jambo ambalo liko wazi.

Baada ya hapo, Anna Abdallah aliomba mwongozo wa Spika, akihoji maslahi ya wabunge hao wa upinzani kuwazungumzia wa CCM.

Makinda alisimama na kufunga mjadala akisema: Waheshimiwa wabunge, hiyo kwa kiingereza tunaita 'light moment'. Hapa bungeni hatupo kwa ajili ya maslahi ya chama bali kwa sote tupo hapa kwa maslahi ya wananchi.

Katika hatua nyingine, uamuzi wa Spika wa Bunge Samwel Sitta, kumzuia Rostam Azizi, kuwasilisha maelezo yake binafsi kuhusu sakata la Richmond, umeibua mjadala bungeni.

Mjadala huo ambao siku zoteulikuwa ukienda chini kwa chini, jana uliwekwa hadharani baada ya Naibu Spika kuzungumzia suala la Rostam.

Dalili za kuibuka mjadala huozilianza kujitokeza baada ya Naibu Spika Makinda, kusoma taarifa ambayo kwa wachambuzi, waliweza kubaini ilionekana kuwa na siri nyuma yake.

Katika taarifa hiyo, Makinda aliongeza kwamba baadhi ya wabunge hao wamekuwa wakifanya hivyo hata kabla yakupata baraka za vyama vyao vya siasa kuhusu hoja au miswada hiyo.

Baada ya maelezo hayo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed

alihoji mwongozo akisema:, �Hivi kama mbunge ameshaleta hoja binafsi bungeni, je bado chama kina nafasi?

Mara baada ya Rashid kumaliza kuomba mwongozo, Makinda alimtaka atoe mfano wa mbunge,

ndipo akasimama na kumtaja Rostam, kwamba litaka kutoa maelezo binafsi kama alivyotakiwa na Kamati Teule ya Bunge kuhusu Richmond, lakini akazuiliwa.

Waheshimiwa wabunge, nimefurahi sana hili la Rostam kuulizwa, suala hili limekuwa likizungumzwa, alisema Makinda, akithibitisha kwamba tangu awali kuna kitu alikuwa akikilenga ambacho kilijificha nyuma ya taarifa yake.

Bada ya hapo Makinda alifafanua sakata hilo, akisema kanuni ya 54(4) pia ilitumika kumzui Rostam kuwasilisha hoja hiyo ambayo tayari ilikuwa katika kumbukumbu za Bunge(Hansard), huku maelezo yake yakiwa hayana tofauti yoyote na aliyowasilisha katika Mkutano wa 10wa Bunge.

Alisema Spika aliona hakuna haja ya kuibuliwa mjadala ambao ulishafungwa huku pia mbunge huyo, akitaka kurudia maneno ambayo tayari ameshatoa na yapo katika kumbukumbu hizo.

Hata hivyo, haikuthibitika n ivipi maelezo ya Rostam katika mkutanohuu wa 11 yalikuwa ni sawa na ya awali, kutoka na mambo hayo kuwa siri kati ya Ofisi ya Spika na Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kamati ya Uongozi ya CCM inaundwa na wabunge wote wa chama hicho ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu (CC), wakiwemo Naibu Spika na Spika wake.

Katika siku za karibu, uamuziwa Spika kumzuia Rostam kutoa maelezo binafsi umeonekana kuibua hisia tofautindani ya bunge.

Baadhi ya wabunge wanahisi uamuzi huo wa kumzuia Rostam haukuwa sahihi, kwani unaonekana kuwa na shinikizo la Kamati hiyo ya CCM, huku wengine wakiona hakukuwa na
haja ya kurudisha mjadala wa Richmond.

Katika maelezo ya Rostamkatika mkutano wa 10 wa bunge, ambayo yapo katika kumbukumbu za bunge pamoja namambo mengine alikana kuwa na hisa au umiliki wa aina yoyote ndani Kampuni ya Richmond.

Pia Rostam alisema, Spika Sitta alishindwa kudhihirisha kauli mbiu yake ya Kasi na Viwango katikautekelezaji wa majukumu ya Kamati Teule, hasa baada ya kuongeza muda baada ya kamati hiyo kuwa haijatoa mapendekezo.
 
Rostam Azizi anawakimbiza watanzania kwa sababu ambazo hazijulikani kabisaaa. Hata kama yeye ni shemeji ya mkuu wa kaya lakini bado hawezi kuwa na sauti kubwa hivi. Wanapagawa masikini viongozi wa CCM hata hawana cha kusema tena! Inatisha sasa
 
WAHISANI wameitaka serikali kuhakikisha inatekeleza mapendekezo ya ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoundwa kuchunguza mchakato wa zabuni ya umeme ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond ya Marekani, ifikapo Juni, mwaka huu la sivyo hawatachangia bajeti ya 2008/9.

Uamuzi huo wa Wahisani ulielezwa jana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo alipokuwa akitoa mada katika semina ya Mafunzo kwa Wabunge wa Kamati za Bunge za Hesabu iliyokuwa ikifanyika mjini hapa.

Mkullo alikiri kwamba ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na katika zabuni ya Richmond, umeitikisa nchi na dunia, hali iliyosababisha wahisani kuonyesha nia ya kutoisaidia Tanzania katika bajeti yake, lakini baada ya mazungumzo na serikali wahisani hao wamerejesha tena nia hiyo.

Mkullo alisema wahisani hao waliridhika na jinsi Rais Jakaya Kikwete alivyoshughulikia ufisadi katika EPA kwa kuchukua hatua iliyosababisha kuvuliwa madaraka aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali, hivyo kuonyesha nia yao tena ya kuisaidia Tanzania.

Hata hivyo, Waziri Mkullo alisema baada ya mazungumzo na wahisani hao, walikubaliana

kuhakikisha kuwa mapendekezo yote yaliyopo katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, chini ya uenyekiti wa Dk Harrison Mwakyembe, yanatekelezwa ifikapo Juni, mwaka huu.

Alisema ili kuhakikisha jambo hilo linatekelezeka, serikali pamoja na wahisani hao, wameweka utaratibu wa kukutana kila mwisho wa mwezi ili kupeana maendeleo na kwamba, kikao cha kwanza kilikuwa kifanyike jana.

Kutokana na kikao hicho, Waziri Mkullo ambaye jana alikuwa akitoa mada katika semina ya Mafunzo kwa Wabunge wa Kamati za Bunge za Hesabu iliyokuwa ikifanyika mjini hapa, alishindwa kuendelea mpaka mwisho wa semina hiyo na kuomba arudi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukutana na baadhi ya mabalozi wa nchi mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano waliojiwekea.

''Baada ya masakata yote haya ya ufisadi, tulikaa na wafadhili tukaweka action plan (ratiba ya utekelezaji) ili kuwatoa hofu wafadhili wetu kuwa mambo haya hayatatokea tena. Hivyo, tulikubaliana kuhakikisha upande wetu wa serikali unatekeleza mapendekezo yote ya ripoti ya Dk Mwakyembe, kwa upande wao waliomba wakutane na Waziri wa Fedha kila mwezi ili kuwapa feedback (mrejesho) ya nini kilichofanyika katika kutekeleza hilo,'' alisema Waziri Mkullo.

Alisema tayari wahisani wameshamuandikia barua kujua utekelezaji wa mapendekezo hayo yamefikia katika hatua gani na kama inatekelezeka hivyo katika kikao hicho cha jana alikuwa akienda kuwapa maelezo namna serikali ilivyotekeleza mapendekezo hayo.

Baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge, ni pamoja na kuitaka serikali kuwawajibisha wahusika, kulieleza Bunge ilikofikia na kuangalia uwezekano wa kusitisha mkataba wa Kampuni ya Dowans iliyonunua hisa za Kampuni ya Richmond.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkullo alisema serikali ina mpango wa kupeleka sheria bungeni ili kuweza kuwashughulikia wote wanaojihusisha na matumizi mabovu ya fedha za umma.

Alisema katika sheria hiyo, watakaobainika kujihusisha kwa namna yoyote na matumizi mabaya ya fedha za umma, watapewa adhabu kali kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, waziri huyo hakuwa tayari kutaja adhabu hizo ingawa alisema adhabu zote zimeainishwa katika sheria hiyo.

Wote watakaopatikana na hatia ya matumizi mabaya ya pesa, wanaojihusisha na uvujaji wa pesa za serikali na umma kinyume cha taratibu za nchi watawajibika kwa,mujibu wa sheria, hizi ni pesa za umma. Wahisani wanachangia asilimia 40 ya bajeti yetu asilimia 60 inayobaki ni kodi zetu, ni lazima wawajibishwe kwa mujibu wa sheria na kuchukuliwa adhabu kali kwa kosa la kutafuna pesa zetu, alisema Waziri Mkullo.

Pia alisema sheria zote za mrabaha zinatarajiwa kubadilishwa kutokana na baadhi ya mashirika ya umma kutolipa gharama za mrabaha.

Alisema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Wete, Mwadini Abbas Jecha aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali kutokana na baadhi ya mashirika ya umma kutolipa mrabaha huku akitoa mfano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa nchini (TANAPA) na Hifadhi ya Mbunga za Wanyama ya Ngorongoro.

Wakati huo huo, Mbunge wa Igalula, Tatu Ntimizi, amepasua bomu kwa kumbana Waziri Mkullo kutoa ufafanuzi kwa nini Ofisi ya Waziri Mkuu, iliagiza magari ya kifahari ambayo yaligharimu kiasi kikubwa cha fedha na bila kufanya utafiti kujua yalihitajika magari gani badala yake magari hayo yaliachwa na kuagizwa aina nyingine ya magari.

''Hii ni mianya ya rushwa, ni aibu hata ofisi za wakuu wa nchi na maafisa wake, wanajitengenezea mianya na mazingira ya fedha kuliwa na si matumizi halisi kwanini? Tunaomba mheshimiwa waziri utujibu katika suala hili,'' alisema Ntimizi na kuongeza:

''Ofisi ya Waziri Mkuu iliagiza magari ya kifahari aina ya Lexus. Lakini muda mfupi baada ya magari hayo kufika tu, ikagundulika kuwa hayafai kwa ajili ya Waziri Mkuu na ndipo ofisi hiyo ilipoamua kuagiza aina nyingine ya magari kwa jili ya kiongozi huyo. Wewe ndio waziri wetu tunahitaji majibu katika hili, hapa ukaguzi unaendaje?''.

Alisema taasisi za serikali zimekuwa na matumizi mabaya ya fedha na kumtaka waziri kueleza kama ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ameliona hilo na hatua gani zimechukuliwa.

Ntimizi pia alisema serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imenunua dawa mbalimbali, zikiwamo za mabusha na kuzipeleka sehemu ambazo hazina matatizo ya ugonjwa huo, huku akitoa mfano wa Tabora ambapo alidai zimepelekwa kwa wingi.

''Hii ni aibu nchi ina matatizo mengi watu wachache wanapitisha ununuzi wa dawa kama ya mabusha na kupeleka sehemu ambazo hazina matatizo hayo huku wananchi wakila mlo mmoja na wenyewe wanajiwekea mazingira ya kula pesa,'' alisema Ntimizi.

Kikao hicho cha wabunge ambacho kimekaa kwa siku tatu mjini hapa, jana kilionekana kuwa mwiba kwa serikali baada ya wabunge kumbana waziri huyo kwa maswali lukuki na kumtaka ajibu maswali hayo kwa maandishi, ili kuepuka kutoa majibu kirahisi na yasiyokidhi.

Kabla ya kujibu, Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo alimtahadharisha Waziri Mkullo kuwa kikao hicho si legelege kwa kuwa sasa wabunge wamekomaa na kwamba, wamehitimu na wanataka majibu ya kina.

Kabla ya kujibu maswali hayo, Waziri Mkullo alisimama na kusema alishajiandaa kujibu maswali yote kwa kuwa kabla ya kuja katika kikao hicho, alisoma vizuri na baada

Ya kufika hotelini hapo alipewa mambo yote yaliyojiri kikaoni, hivyo ingekuwa rahisi kwake.

Hata hivyo, Waziri Mkullo alisema kwa kuwa wabunge wameamua awape majibu hayo kwa maandishi, atafanya hivyo na kuahidi kuwapa majibu hayo kabla ya kikao kijacho cha Bunge la Bajeti kinachotarajiwa kufanyika Juni.

Hata hivyo, Mkullo alijibu baadhi ya maswali aliyoyaita kuwa ni mepesi na kuwa alikuwa na majibu yake.

Pamoja na mambo mengine, wabunge hao walitaka kujua kwa nini bajeti ya serikali siku zote inakuwa tegemezi, kwa nini kunakuwa na utumiaji mbovu wa misamaha ya kodi na kutaka suala hilo liangaliwe upya.

Maswali mengine, ni kwanini pesa za bajeti zinazobaki kila mwaka katika baadhi ya wizara, hazionyeshwi katika bajeti ijayo kuwa zimetumikaje na zinaenda wapi.

Swali hilo liliulizwa na Mbunge wa Pangani, Mohamed Rished, kwanini ripoti ya CAG, haipelekwi moja kwa moja kwa Spika ambaye ndiye aliyemtuma kwa niaba ya wabunge na wananchi na badala yake, ripoti hiyo anakabidhiwa kwanza Rais ndipo ipelekwe bungeni na hatua zinazochukuliwa kwa halmashauri zinazopata hati chafu kwa kuwa, Ripoti ya CAG inaonyesha kila mwaka kuna halmashauri zinavurunda, lakini hazifanywi chochote.

Source: Gazeti mwananchi
 
Posted Date::5/3/2008
Wahisani wampa mtihani mgumu Rais Kikwete kuhusu visa vya Richmond
* Atakiwa kuwatosa marafiki zake serikali yazidi kupata kigugumizi

Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

KITENDO cha nchi wahisani kuipa masharti serikali kuwa ihakikishe inatekeleza maazimio ya Bunge kuhusiana na Mchakato wa Zabuni ya Umeme wa Dharura iliyoipa ushindi Kampuni ya Richmond, ni mtihani mwingine mgumu kwa Rais Jakaya Kikwete.

Wahisani wameibana serikali iwe imetekeleza mapendekezo hayo ifikapo Juni mwaka huu, ambao ni mtihani mgumu kwa serikali ya Kikwete, kutokana na ukweli kwamba, imekuwa ikipata kigugumizi kuwachukulia hatua watu mbalimbali waliobainika kuhusika katika kashfa za ufisadi.

Kashfa ya Zabuni ya Richmond ambayo imewafanya watanzania kuilipa Kampuni Downs iliyochukua kazi za Richmond kiasi cha Sh152 milioni kwa siku na kashfa nyingine, hivi sasa zinaitikisa serikali.

Kushindwa kuwachukulia hatua watu waliohusika moja kwa moja katika kuingia mtakaba huo, ndio sababu iliyowafanya wahisani kuamua kuingilia kati na kuibana serikali kuwachukulia hatua watu hao.

Ili kuhakikisha jambo hilo linatekelezeka, serikali pamoja na wahisani wameweka utaratibu wa kukutana kila mwisho wa mwezi, ili kupeana maendeleo na kwamba kikao cha kwanza kiimefanyika hivi karibuni.

Hofu ya wahisani kwa serikali inatokana na ukweli kwamba, Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Dk Harison Mwakyembe iliyochunguza kashfa ya zabuni ya Richmond ilitoa mapendekezo yake katika kikao cha Bunge cha Februari, mwaka huu na kusababisha mawaziri watatu akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Loawssa kujiuzulu.

Baada ya hapo serikali iliunda timu ya kupitia upya mapendekezo hayo na ikaahidi katika kikoa cha Bunge la Aprili mwaka huu, ingetoa taarifa ya utekelezaji lakini katika kikao hicho suala hilo liliahirishwa hadi katika Bunge lijalo la bajeti.

Wachunguzi wa mambo wanaona suala hilo la Richmond huenda likakosa nafasi ya kujadiliwa katika kikao hicho ambacho huwa kinajadili bajeti ya serikali na bajeti za wizara na kulifanya sasa litupwe hadi katika kikao cha Oktoba, mwaka huu.

Hofu nyingine ya wahisani kwa serikali kuwachukulia hatua mafisadi wanaohusika katika kashfa nyingi zilizoibuka nchini, inatokana na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hivi karibuni kuwa mafisadi ni watu hatari ambao hawakamatiki.

Kauli hiyo inaonyesha kuwa serikali hata serikali nayo haina uhakika kama ina uwezo wa kuwadhibiti mafisadi hali, ambayo wahisani wameamua kuweka mkono wao.

Baadhi ya kashfa ambazo zimebuka, lakini serikali mpaka sasa haijawachukulia hatua wahusika ni pamoja na kuliwa kwa Sh133 bilioni za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mikataba mobovu ya sekta ya madini, TICTS, ununuzi wa rada, mkataba bomu wa kulibinafsisha Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuwa TRL; IPTL, Songas, uuzaji nyumba za serikali na ununuzi na ndege ya Rais.

Kutokana na hali hiyo ni wazi kwamba serikali ya Kikwete huenda ikawama kutekeleza masharti ya wahisani, ambao wanachangia asilimia 40 ya bajeti ya nchi na hivyo kukosa msaada wao.

Kama itaweza kutekeleza basi Rais Kikwete atakuwa amekubali kuwatosa marafiki zake ambao wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa hiyo, kwa kuwafikisha mahakamani ikimanisha kwamba kama wakipatikana hatia watafungwa.

Duru za kisiasa zinaeleza kwamba uamuzi huo wa serikali kukubali kutekeleza masharti ya wahisani unaonyesha kwamba sasa utakuwa ni kusambaratika rasmi kwa mtandao ambao ulimweka madarakani kutokana na wengi wana mtandao kuhusika moja kwa moja katika kashfa hii ya Richmond.

Baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge, ni pamoja na kuitaka serikali kuwawajibisha wahusika waliosainidia serikali kuingia mkataba huo.

Waliopendekezwa kuondolewa kazini na kuchukuliwa hatua ni Mwanasheria mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, Dk Ibrahim Msabaha, waziri aliyekuwapo katika wizara hiyo, Nazir Karamagi, Katibu Mkuu, Arthur Mwakapugi, Kamishna wa Nishati, Bashir Mrindoko na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hosea.

Hata hivyo, Karamagi na Dk Msabaha walijiuzulu katika kikoa cha Bunge la Februari, mwaka huu.
 
•
Richmond yafanya utapeli mwingine

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Richmond Development Company LLC ambayo ilishindwa kukamilisha mradi wa megawati 100 wa umeme wa dharura nchini imezidi kuonesha taswira yake ya kisanii baada ya uchunguzi wa gazeti hili kubaini kuwa hivi sasa imeanza kufanya utapeli mwingine kwa kutumia jina la Tanzania.

Kwa mujibu wa habari ambazo Majira Jumapili imezipata, viongozi wa Richmond hasa walioko Marekani, Bw. Mohammed Gire na Dkt. Mohammed Huque, wamekuwa wakiutumia mradi wa umeme wa dharura uliowashinda wa Ubungo hapa nchini ili kupata mikataba mingine minono duniani.

Gazeti hili lilithibitisha taarifa hizo kupitia tovuti ya kampuni hiyo yenye anuani ya www.rdevco.com, ambapo ukifungua kiunganishi cha 'recent projects' (miradi ya hivi karibuni) bila aibu Richmond inajinasibu duniani kuwa mwaka 2006 walikamilisha mradi huo kwa ufanisi katika zile megawati 25 za kwanza.

"Mwaka 2006, tulikamilisha mradi wa umeme wa dharura wa Ubungo, Dar es Salaam, Tanzania. Tuliukamilisha mradi huo kihandisi, kimanunuzi na kiuendeshaji kwa zile megawati 25 za kwanza," inasema taarifa ya tovuti hiyo.

Lakini taarifa za hakika zilizokusanywa na Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dkt. Harrison Mwakyembe, zinaonesha kuwa ni Dowans ndio waliofunga na kuwasha megawati 25 za kwanza, huku Richmond wakiwa ndio waliouleta mtambo huo lakini ukawashinda kuufunga.

Oktoba 30, 2006 Richmond baada ya mvutano wa muda mrefu na TANESCO, taarifa za Kamati ya Bunge zinaonesha, ndipo walipoleta nchini mtambo wa megawati 22 tu ambao hata hivyo ulikaa bila kufungwa kwa muda mrefu hadi Novemba 14 vilipowasili viunganishi vyake.

Ripoti ya Kamati ya Bunge pia ikimkariri Mhandisi Boniface Njombe, ambaye alikuwa Meneja wa Mradi huo kwa upande wa TANESCO akikiri kuwa Richmond walionekana hawana hata utaalamu wa kufunga mashine na mara kadhaa walikosea kiasi cha kusababisha mlipuko.

Tofauti na Richmond wanavyojinadi kwenye tovuti hiyo, uchunguzi wa gazeti hili umezidi kuonesha kuwa baadaye Dowans, ambao walichukua rasmi kazi za Richmond kuanzia Desemba 23, ndio waliosimamia hadi mtambo huo ukatengemaa na kuanza rasmi kuzalisha umeme mwanzoni mwa 2007, tofauti na tovuti hiyo inavyosema ulikamilika 2006.

Katika tovuti hiyo Richmond pia inajitangaza kuwa ndiyo iliyoandaa taratibu zote kwa ajili ufungaji wa mtambo uliokamilisha uzalishaji wa megawati 100 za umeme jambo ambalo kwa mujibu wa ripoti rasmi za Bunge si la kweli pia kwani tangu Desemba 2006 Dowans ndio walioshika kazi zote za kihandisi na kimanunuzi na ndio wanaolipwa hadi sasa.

Katika hatua nyingine, imebainika kuwa tofauti na awali ilipokuwa ikitangaza kwenye tovuti hiyo kuwa ina mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wenye uwezo wa kuchukua watu 65,000 katika eneo la Afrika Mashariki, ukarabati wa viwanja vya ndege na ujenzi wa bomba la mafuta, hivi sasa matangazo hayo yameondolewa kwenye tovuti hiyo bila maelezo yoyote.

Kuwepo kwa matangazo hayo yaliyokuwa yakitaja miradi ya uongo au ambayo kampuni hiyo iliishindwa ni moja ya mambo yaliyowapa watanzania wengi shaka kiasi cha kushinikiza kampuni hiyo ichunguzwe kuona iwapo ilikuwa na sifa ilizokuwa ikijigamba nazo.

Juhudi za gazeti hili kuwasiliana na viongozi wa Richmond walioko nchini Marekani hazikuzaa matunda.

Awali gazeti hili lilijaribu kupiga simu ya kampuni hiyo lakini mara zote simu hiyo ilikuwa ikielezwa kuwa haipo au imeshindwa kuunganishwa.

Lakini hadi jana ikiwa ni wiki mbili tangu gazeti hili lilipomtumia maswali kupitia anuani ya baruapepe ya kampuni yake kuomba ufafanuzi juu ya masuala hayo, Bw. Gire hakujibu chochote.

Hivi sasa Serikali iko katika mchakato wa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wa umma waliohusika katika kuipa zabuni kampuni hiyo.

Sakata hilo pia lilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa pamoja na waliokuwa mawaziri waandamizi, Dkt. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi kujiuzulu kutokana na kuhusishwa na kashfa hiyo.

Kuendelea kwa Richmond kung'ang'ania mradi wa Ubungo wa kufua umeme wa dharura, kunaweza kufasiriwa kuwa ni kuzidi kuiumbua kampuni hiyo lakini pia wachunguzi wengine wa mambo, wanapata shaka kuwa huenda madai kuwa kampuni hiyo bado inanufaika au inajihusisha na mradi huo kupitia kampuni ya Dowans yakapata nguvu.

Dowans ambayo ililetwa na Richmond ikiwa haifahamiki hapa nchini wala miongoni mwa makampuni makubwa ya nishati, imekuwa ikilipwa mamilioni na Serikali kupitia TANESCO kwa mkataba huo iliourithi
 
In 2006, we completed the Ubungo Emergency Supply Power Plant Project in Dar es Salaam, Tanzania. We provided full project development and engineering, procurement and commissioning (EPC) for the first 25MW, and all preparatory work for the second phase, of a 100MW ISO gas-based generation plant..
Richmond wameamua kujinadi kwa mtandano waliochemka wa Ubungo
 
Sababu serikali ya JK imeshindwa kuanzisha kesi against hawa wezi wakina Gire na familia yake. Hawa watu wanatisha sana, they can do anything for money.
 
Sababu serikali ya JK imeshindwa kuanzisha kesi against hawa wezi wakina Gire na familia yake. Hawa watu wanatisha sana, they can do anything for money.

Ataanzisha vipi hiyo kesi wakati na yeye ana ka-harufu kama hako. Ajisafishe kwanza ndipo anaweza kuwa na Guts hata za kuwakodolea macho.
 
Sasa mnakataa nini wakati mmeshaambiwa kuwa mwenye RD ndo mwenye Dowarns, kwani mradi haujakamilika? Na mmiliki si ndio huyohuyo mmoja?

Serikali yetu imelala sana hawa watu kwanini wasiulizwe kama wako serious kwenye kazi, wanasema uongo kila sehemu na kupata tenda ambazo hawawezi kuexcute.

Mara bomba la mafuta kutoka Dar mpaka mwanza mara uwanja wenye uwezo wa kubeba watu 60,000 Dar. Wanaonekana ni matapeli kwenye kila kitu wanachofanya.
 
ANALYSIS: Media and independent motion on Richmond: End of truth pursuit?

THISDAY CORRESPONDENT
Dar es Salaam

EXCITEMENT about the manner in which the government shall move to implement proposals on the Richmond Development Co. power supply scandal hit a snag once it became impossible for the legislature to hear a different view of things.

Up to that point, the media had more or less been quite sure of its line of analysis, that Igunga MP, Rostam Aziz did not appear before the committee when summoned to give evidence, as was the case with ex-premier Edward Lowassa. The cause of the failure didnt need investigative reporting to affirm, as the guilty are afraid.

Scarcely has politics taken a turnabout as on this score, when those who believed they were hunting suddenly discovered they were being hunted, and fell back rapidly on parliamentary regulations (conveniently called standing orders) to ensure that the motion doesnt surface. Nor indeed has there been an effort since then to leak what there was in the said motion, though it is entirely possible that the author would have been happy to share what he wanted to say in the House. Its happier that way.

Similar indications are also coming up in relation to investigations on the External Payment Arrears account, where a prominent individual whose name wasnt given and listed among beneficiaries of the funds was telling the media what would happen if he was hauled to court. The point was that there is plenty that cannot be stomached by the government, in which case it wouldnt make sense to cross certain limits and demand too strict of the issues, as then its reaction would swing into the defensive. That would put an end to institutional encouragement of pursuing truth on the basis of cooperation with authorities, congratulating the media.

So unlike the Richmond issue which at least saw a first reading of the conclusion of its investigation, but appears to defy gravity when it comes to making a comeback to insist on its pound of flesh, meting punishment to all concerned, it now has to take a turn. It is supposed to be treated in a conservative manner before seeing its youth blossom, tasked with greening the picture for legislative habits of inquiry and government habits of deep responses, knowing where the blame would be directed. When the probing comes perilously close, active participating in probes ceases, or is directed to irrelevant pursuits from an early hour, clearly.

In behaviour terms, according to theorists like German sociologist Max Weber, the stage of charisma in relation to graft scandals is rapidly coming to an end, and instead it shifts to bureaucracy. Here the key is hierarchy, and obtaining one bit of information if laborious, and could lead to confronting bureaucracy on other aspects, for instance by an intentional breaching of the National Security Act, now reflected in the PCCB Act. Once PCCB takes up a probe, it marks the end of all probing.
 
Posted Date::5/31/2008
Spika Sitta:Bunge linaisubiri serikali kuhusu Richmond
*Asema Bunge halitakubali kuona suala hilo linayeyuka
*Muswada wa CAG kuwajibika bungeni kuwasilishwa

Na Kizitto Noya
Mwananchi

BUNGE limesema linasubiri taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya kamati yake iliyoiunda kuchunguza zabuni ya mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura na Kampuni ya Richmond, na halitakubali Serikali kuichezea taarifa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samwel Sitta, alisema kimsingi, Bunge sasa halina haja ya kuijadili taarifa hiyo kwa kuwa, Serikali ambayo ni mhimili mwingine wa dola inalifanyia kazi.

Hata hivyo, alisema kuwa Bunge halitegemei na wala halitakubali kuona ripoti ya utekelezaji wa mapendekezo yake inachezewa. "Bunge na Serikali ni taasisi zinazofanya kazi kwa kuheshimiana, Serikali ikisema tusubiri, tunaipa muda, lakini hatutakubali kuona ripoti hiyo inachezewa," alisema Sitta.

Alisema Bunge liko makini kufuatilia mijadala inayohusu maslahi ya taifa, ukiwamo ule unaotokana na ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe kuchunguza mchakato wa mkataba wa Richmond kwa kuwa Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, Bunge halitakubali kuona masuala hayo yanaishia hewani.

Kwa mujibu wa Sitta, nia ya Bunge kutaka ripoti ya uchunguzi wa ukwapuaji wa Sh 133 bilioni katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ijadiliwe bungeni ilikoma, baada ya Rais Jakaya Kikwete kuunda kamati ya kuchunguza na kuwashtaki watuhumiwa wa ufisadi huo, hivyo Bunge linasubiri kwa hamu taarifa ya uchunguzi huo na matokeo yake.

Alisema Bunge linasubiri taarifa za mijadala yote inayohusu maslahi ya taifa, ikiwamo EPA, Richmond na TICTS na litahakiki kama matokeo ya uchunguzi na hatua zilizochukuliwa ni sahihi.

Kuhusu TICTS, Sitta alisema atatakiwa kutolea maelezo ushahidi wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, aliouwasilisha kwake, badala ya waziri huyo kusimama mwenyewe bungeni kujitetea. "Kuhusu suala la Karamagi, baada ya kupokea ushahidi wake, mimi (Spika) nitautolea maelezo ndani ya kikao cha Bunge na siyo yeye kujieleza tena," alisema.


Katika hatua nyingine, kikao cha 12 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinatarajiwa kuanza Juni 10 kikiwa na miswada mipya minne, ukiwamo Muswada wa Ukaguzi wa Hesabu za Umma (Public Audit Bill,2008).

Akielezea muswada huo, Sitta alisema umelenga kuiondoa ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutoka usimamizi wa Hazina na kuwajibika bungeni.

Sitta alisema kitendo cha ofisi hiyo nyeti kuwa chini ya Wizara ya Fedha kinamnyima CAG kuwa huru kufanya ukaguzi kwa makini na kuruhusu kukithiri kwa ufisadi.

"Tunataka CAG awajibike bungeni na sio serikalini ili awe huru katika kazi yake kwa sababu uzoefu unaonyesha kuwa, kila dosari inayoonekana kwenye ofisi yake, ina uhusiano na Hazina," alisema na kuongeza kuwa muswada mwingine unaotarajiwa kuwasilishwa ni wa Utawala wa Bunge, (National Assembly Administration Bill, 2008).

Alisema katika muswada huo, Bunge linataka uhuru wa utawala na kujitosheleza kwenye maamuzi badala ya kupata maelekezo kutoka serikalini kupitia Waziri Mkuu. "Kwa kufanya hivyo tunaamini Bunge litajiongezea umadhubuti katika utendaji wake na kujitosheleza katika maamuzi ya kazi zake za uwakilishi, kutunga sheria na kuisimamia Serikali," alisema.

Sitta aliongeza kuwa kikao hicho pia kitajadili Muswada wa Sheria wa Fedha wa mwaka 2008 (The Finance Bill, 2008) na Muswada wa Sheria ya Matumizi wa Mwaka 2008 (The Appropriation Bill, 2008).

Kikao hicho pia kitapokea miswada mingine binafsi itakayowasilishwa na Kamati za Bunge na kuisoma kwa mara ya kwanza, lakini mijadala ya miswada hiyo itafanyika katika mkutano wa 13. Mkutano huo wa Bajeti utaanza Juni 10 hadi Agosti 25. Katika kikao hicho, Bunge litaanza kutumia kanuni mpya kadhaa zilizowekwa kwa lengo la kuboresha utendaji wake ikiwamo kanuni inayompa Spika au Naibu Spika nguvu ya kutoa maamuzi bila kubanwa na vyama vya siasa.

Kanuni zingine ambazo zitatumika kwa mara ya kwanza ni Bunge kuendeshwa na wenyeviti watatu, kuundwa kwa idara ya sheria bungeni, Wabunge kuruhusiwa kumuuliza waziri Mkuu maswali bila kutoa taarifa ya awali, Kamati za Bunge kuruhusiwa kutunga sheria na Kamati za Bunge kufanya kazi kwa uwazi.

Alisema Bunge limeunda kamati maalum kwa ajili ya kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa, ikiwamo Kamati ya Ukimwi na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
 
Kibano kama kawaida, wataendelea kubanwa na kuulizwa hatua waliyofikia kwenye utekelezaji wa mapendekezo ya bunge.
 
Spika Sitta:Bunge linaisubiri serikali kuhusu Richmond
*Asema Bunge halitakubali kuona suala hilo linayeyuka
*Muswada wa CAG kuwajibika bungeni kuwasilishwa

Na Kizitto Noya

BUNGE limesema linasubiri taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya kamati yake iliyoiunda kuchunguza zabuni ya mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura na Kampuni ya Richmond, na halitakubali Serikali kuichezea taarifa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samwel Sitta, alisema kimsingi, Bunge sasa halina haja ya kuijadili taarifa hiyo kwa kuwa, Serikali ambayo ni mhimili mwingine wa dola inalifanyia kazi.

Hata hivyo, alisema kuwa Bunge halitegemei na wala halitakubali kuona ripoti ya utekelezaji wa mapendekezo yake inachezewa. "Bunge na Serikali ni taasisi zinazofanya kazi kwa kuheshimiana, Serikali ikisema tusubiri, tunaipa muda, lakini hatutakubali kuona ripoti hiyo inachezewa," alisema Sitta.

Alisema Bunge liko makini kufuatilia mijadala inayohusu maslahi ya taifa, ukiwamo ule unaotokana na ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe kuchunguza mchakato wa mkataba wa Richmond kwa kuwa Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, Bunge halitakubali kuona masuala hayo yanaishia hewani.

Kwa mujibu wa Sitta, nia ya Bunge kutaka ripoti ya uchunguzi wa ukwapuaji wa Sh 133 bilioni katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ijadiliwe bungeni ilikoma, baada ya Rais Jakaya Kikwete kuunda kamati ya kuchunguza na kuwashtaki watuhumiwa wa ufisadi huo, hivyo Bunge linasubiri kwa hamu taarifa ya uchunguzi huo na matokeo yake.

Alisema Bunge linasubiri taarifa za mijadala yote inayohusu maslahi ya taifa, ikiwamo EPA, Richmond na TICTS na litahakiki kama matokeo ya uchunguzi na hatua zilizochukuliwa ni sahihi.

Kuhusu TICTS, Sitta alisema atatakiwa kutolea maelezo ushahidi wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, aliouwasilisha kwake, badala ya waziri huyo kusimama mwenyewe bungeni kujitetea. "Kuhusu suala la Karamagi, baada ya kupokea ushahidi wake, mimi (Spika) nitautolea maelezo ndani ya kikao cha Bunge na siyo yeye kujieleza tena," alisema.

Katika hatua nyingine, kikao cha 12 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinatarajiwa kuanza Juni 10 kikiwa na miswada mipya minne, ukiwamo Muswada wa Ukaguzi wa Hesabu za Umma (Public Audit Bill,2008).

Akielezea muswada huo, Sitta alisema umelenga kuiondoa ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutoka usimamizi wa Hazina na kuwajibika bungeni.

Sitta alisema kitendo cha ofisi hiyo nyeti kuwa chini ya Wizara ya Fedha kinamnyima CAG kuwa huru kufanya ukaguzi kwa makini na kuruhusu kukithiri kwa ufisadi.

"Tunataka CAG awajibike bungeni na sio serikalini ili awe huru katika kazi yake kwa sababu uzoefu unaonyesha kuwa, kila dosari inayoonekana kwenye ofisi yake, ina uhusiano na Hazina," alisema na kuongeza kuwa muswada mwingine unaotarajiwa kuwasilishwa ni wa Utawala wa Bunge, (National Assembly Administration Bill, 2008).

Alisema katika muswada huo, Bunge linataka uhuru wa utawala na kujitosheleza kwenye maamuzi badala ya kupata maelekezo kutoka serikalini kupitia Waziri Mkuu. "Kwa kufanya hivyo tunaamini Bunge litajiongezea umadhubuti katika utendaji wake na kujitosheleza katika maamuzi ya kazi zake za uwakilishi, kutunga sheria na kuisimamia Serikali," alisema.

Sitta aliongeza kuwa kikao hicho pia kitajadili Muswada wa Sheria wa Fedha wa mwaka 2008 (The Finance Bill, 2008) na Muswada wa Sheria ya Matumizi wa Mwaka 2008 (The Appropriation Bill, 2008).

Kikao hicho pia kitapokea miswada mingine binafsi itakayowasilishwa na Kamati za Bunge na kuisoma kwa mara ya kwanza, lakini mijadala ya miswada hiyo itafanyika katika mkutano wa 13. Mkutano huo wa Bajeti utaanza Juni 10 hadi Agosti 25. Katika kikao hicho, Bunge litaanza kutumia kanuni mpya kadhaa zilizowekwa kwa lengo la kuboresha utendaji wake ikiwamo kanuni inayompa Spika au Naibu Spika nguvu ya kutoa maamuzi bila kubanwa na vyama vya siasa.

Kanuni zingine ambazo zitatumika kwa mara ya kwanza ni Bunge kuendeshwa na wenyeviti watatu, kuundwa kwa idara ya sheria bungeni, Wabunge kuruhusiwa kumuuliza waziri Mkuu maswali bila kutoa taarifa ya awali, Kamati za Bunge kuruhusiwa kutunga sheria na Kamati za Bunge kufanya kazi kwa uwazi.

Alisema Bunge limeunda kamati maalum kwa ajili ya kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa, ikiwamo Kamati ya Ukimwi na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
 
Let hope something will change for better, kwani tunachohitaji ni watendaji kama CAG kuwa huru kufanya kazi yake badala ya kureport kwa waziri mkuu kama ilivyo sasa
 
Back
Top Bottom