Kashfa ya Jairo: Malipo ya zaidi Billioni 1 kusaidia Bajeti ipitishwe - Adai MP Beatrice Shelukindo

Status
Not open for further replies.
Wizara ya Nishati na Madini, wasingefanya hayo waliofanya kama Wabunge wasingekuwa wanahongeka?

Alafu CAG kwa nini unakubali Wafanyakazi wa Serikali kulipwa cash... weka kanununi kwamba lazima walipwe through their bank account... hapa watakamatika wakati wote.


Kasheshe.
kwani pesa haiwekwi kwenye acc zao?
 
Hii kampuni maarufu ya PR lazima itakuwa ile inayoandaa ma-Bonanza ya Wabunge kule Dodoma (ES)
 
kwani pesa haiwekwi kwenye acc zao?

Najua mishahara inalipwa through bank account lakini malipo mengine mengi yanapitia kwenye dirisha la muhasibu hapa ndio rahisi kushindwa ku-audit ki-urahisi... yaani ndio sehemu ufisadi rahis kutokea.

Ili uelewe hoja yangu ni kwamba hizo hela zilizopelekwa Dodoma kama zisingeruhusiwa kulipwa by cash zingetoka je?
 
January, Rostam na Lowassa wanaangusha serikali ya JK hata wasemeje. Hii mizimu yote ni ya January. ALijifanya kuibua Rushwa ndani ya Kamati yake, kumbe ni yeye ndo alisuka mpango mzima. Watu wameanza kumuangalia na macho ya upole kweli. Huyu kijana anakuja kuiua CCM hasa serikali ya JK sasa vita na ngeleja na Jairo ni ya nini jamani?

Unafiki tu hapa. Kama Ngeleja ni mtu wa Rostam, na January ni mtu wa Rostam, kwanini January am-target Ngeleja? Saa zingine uwongo wenu jaribuni ku-connect the dot. Leo mnasahau mlichosema jana!
 
Najua mishahara inalipwa through bank account lakini malipo mengine mengi yanapitia kwenye dirisha la muhasibu hapa ndio rahisi kushindwa ku-audit ki-urahisi... yaani ndio sehemu ufisadi rahis kutokea.

Ili uelewe hoja yangu ni kwamba hizo hela zilizopelekwa Dodoma kama zisingeruhusiwa kulipwa by cash zingetoka je?
hadi tips ukamwekee mtu banki?
 


Mh ama kweli hapa Eric Wainaina aliimba. Anaimba kuhusu Kenya ila kila anacho sema kina apply hata hapa kwetu.
 
Last edited by a moderator:
Jamani, ifazali imefichuka. Hii ni kawaida, makatibu wakuu wote wanafanya hivyo. Kuandika barua kwenda kwenye taasisi wakitaka pesa kutoka kwenye taasisi hizo eti kwa ajili ya miradi ambayo haikuwa kwenye budget. Hii ni sababu mojawapo wa hizi taasisi kutokufanya vizuri, na wizara husika kushindwa kuchukua hatua kwa management kwa kuwa tu huwa wanatoa fadhila.

lazima ichukuliwe hatua nzito.
 
Kwa sakati hili sasa naamini Dr Slaa was right kuwa elimu bure hadi chuo kikuu inawezekana
 
Kwa sakata hili sasa naamini Dr Slaa was right kuwa elimu bure hadi chuo kikuu inawezekana
 
Jamani ufisadi ndio kazi yao hao magamba nashangaa walikuwa wanampiga zito kwamba mawaziri hakupewa rushwa tunashukuru mungu ni mwema na atawahukumu bado wataumbuana sana tu na tutayajua mengi.
 
sasa wewe unafikiri bila hao wabunge wa CCM hiyo bajet si ingepitishwa? Sasa upinzani kutoa hoja ina faida gani wakati kwenye kupiga kura wanapigwa bao?
Wewe nadhani itabidi tukufatilie tukujue ni nani hasa maana ndoa yako na ccm is too much wivu mwingi hutaki mme wako akosolewe hata kidogo!Hivi unadhani kupigia kura budget ndo mwisho wa kila kitu? Umeona walivyoumbuka, ulisahau kama cdm walikataa budget kuu kwa sababu hii ya umeme maana hakukua na pesa ya maana iliyotengwa kutatua tatizo la umeme pamoja na kuwa wametanka kwenye mpango wa miaka mitano.Sasa unaona hasara yake ambayo ni kwenda kuifumua budget nzima na kuchota pesa kutoka vifungu vingine kupeleka kwenye umeme? Hii ni akili ai matope ya wanamagamba? Wakiambiwa cdm wanaakiri kuliko wao hawakubali sasa imekula kwao na aibu imewapata!Hukumsikiliza PM alivyokuwa anawadanganya watanzania eti mwisho wa mwezi wa nane watakuwa wamepata 300MW kitu ambacho hakiingii akilini kwa mwenye akili kama kwa miaka 6 wameweza kuongeza 170MW tu!Subiri uone hata kwa hizi wiki tatu kama watakuja na a workable proposal kama siyo usanii tu wa kuwatuliza wabunge na kupitisha budget ileile. Hapa wananchoenda kukifanya ni kuongeza 100MW tena mwezi wa decemba na serikali kuwachimba mkwara wabunge wao kuungana mkono budget lasivyo mtu atemeshwa ubunge! Nani katika magamba anaweza kuthubuti kupinga hilLi?Chadema wana nguvu ya umma na wanachotafuta ni kukijenga chama chao kikubalike, hivyo hata magamba wafanyaje credit zote ziko cdm maana ndo walioanza kuwakaba koo kwenye swala la umeme. Cdm itaendelea kupaa tu kwa sababu magamba siku zote wanaanza kukataa halafu mambo yakishabana wanakubali. Hapa ndo wanapowapa credit cdm siku zote. Cdm is a pool of intelligent people wanajua ni wapi wabonyeze button za watanzania magamba siku zote hawajui wanasubiri cdm waseme kwanza.Kwa taarifa yako cdm ndo inayoongoza hii nchi kwa sasa maana ndiyo wanaotoa mwelekeo tuende wapi na wananchi wanawasikiliza na kuwaunga mkono.
 
David Jairo, William Ngeleja, Andrew Chenge, Edward Lowasa, Rostam Azizi. Hii list naona wakristo ni vinara wa kuiua hii nchi inabidi viongozi wa dini zote wawakatae hawa washenzi na watengwe na jamii! Ni imani yangu kama kuna maaskofu na mapadre wenye uchungu na waumini wao ukiwatoa wale wanaohusishwa na madawa ya kulevya basi watakuwa na uthubutu wa kuweza kuwa shughulikia ipasavyo. Viongozi wa kidini ni watawala, wanatutawala nafsi zetu na wa siasa wanatawala miili yetu nguvu kuwa ipo kwa viongozi wanaotawala nafsi zetu. Ikiwa maaskofu na masheikh leo hii watatuambia hakuna kwenda popote tujimwage barabarani kupinga ushenzi huu nina imani muitikio utakuwa mkubwa sana. Ni wakati sasa kwa waumini na viongozi wa dini kuweka tofauti zao kwa maslahi ya umma na wasiliachie hili tatizo kwa wanasiasa.
 
Wala usimuonee huruma. Anajua kuwa hapo wanamagamba wanabwabwaja tu ila mwisho wa siku leo bajeti yake itaambiwa NDIOOOOOOOOOOOOO!!!!

mheshimiwa tuko azma yangu bado ni thabiti namalizia mambo yangu hapa nielekee igunga naamini utakuja kuniunga mkono ukiwa unapata tusker baridi nami nashusha heineken baada ya kampeni nzito
 
Wakuu, kwa sisi wachache wenye akili tunajua fika kwamba Hili suala si la Jairo tu bali ulikuwa mkakati mzito akiwahusisha mabosi wake, ila lilivyokaa jamaa itabidi awe mbuzi wa kafara.

Wananchi wenzangu kwa style hii Tanzania kwisha kazi, na nina wasiwasi huenda huu mchezo umekuwa ukichezwa miaka yote - yaani kipindi cha Bajeti kinakuwa kipindi cha MAVUNO kwa baadhi ya wabunge. Inauma sana.

USHAURI: Mimi naomba wizara na nishati na Madini ifumuliwe yote, na ipekuliwe utendaji wake wa kazi kwa idara zote, watendaji wabovu wote watolewe na washitakiwe, mikataba yote ambayo ni siri ya Serikali upelekwe bungeni ijadiliwe. Nchi hii ni yetu sote.

Mungu ibariki Tanzania
 
Wakulu, Nimestushwa sana na kauli ya Waziri Mkuu kwamba Mamlaka ya kumwajibisha Jairo yeye hana, sababu aliyoitoa Raisi kaondoka kuelekea Afrika ya kusini. Inamaana, Raisi anapo safiri husafiri na taasisi ya Uraisi? na hakunaa mamlaka/kiongozi kukaimu hiyo taasisi na kuchukua maamuzi? hatuombei baya likitokea huko aliko safiri itakuwaje!
Kilicho nishitua zaidi ni kwa wabunge wa magamba kumshangilia Waziri Mkuu!
Kweli kuna umuhimu wa katiba mpya.
 
Hajagawiwa ndo maana amesanua deal,mwenzie sendeka nae ameunga mkono,inaonekana pro-ccj hawakupewa mgawo

Mama huyu nilikwisha kaa naye kwa muda na kumsikia anavyoongea na yaliyo moyoni mwake; kwa kifupi ni 'opportunist' na hapo ni kweli kakosa tu mgao.
 
Yes...naomba rekebisha title yaako Mpwa naona kuna ka tatizo ka spelling halafu ntaweka materials hapa wakayasome waelewe maana na application ya Chain Of Command
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom