Kashfa ya Jairo: Malipo ya zaidi Billioni 1 kusaidia Bajeti ipitishwe - Adai MP Beatrice Shelukindo

Status
Not open for further replies.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza uchunguzi wake juu ya madai ya Wizara ya Nishati na Madini kuzichangisha taasisi zilizo chini yake fedha kwa ajili ya kufanikisha bajeti hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah amesema kwamba tuhuma hizo ni nzito na tayari taasisi hiyo imeanza kuzichunguza. Amesema taasisi yake inafanya uchunguzi kwa umakini na kwamba kila anayetuhumiwa atapewa nafasi ya kujitetea na kusisitiza kwamba ofisi yake inalichukulia suala la nishati ya nchi kwa uzito mkubwa."Tumeshaanza uchunguzi... jambo zito kama lile hadi Bunge linaahirishwa unafikiri tunaweza kuliacha hivihivi? Suala la nishati tunalichukulia ‘very serious'. Tutafanya uchunguzi wetu na tutaona matokeo baada ya kukamilika," alisema.

Wakati huohuo PM, Mizengo Pinda ana siri nzito kuhusu hatima ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo baada ya kukaririwa akisema kuwa Rais Jakaya Kikwete amempa maelekezo mapya kuhusu suala hilo ingawa haijulikani ni maelekezo yapi kapewa.

What dude is TAKUKURU? This stupid institute has been sitting idle while or country's riches have been looted by our corrupt leaders and had at times sided with the looters of our national property like Chenge who was once defended by the very Director who is telling us today that his institute will pursue this issue! Afterall it has already been too late to take action if at all TAKUKURU is worth its name; that is the Prevention and Combating of Corruption Bureau, what a name!
To many Tanzanians today this institute is a hopeles burden to the nation with its 'usefulness' seen by our corrupt leaders and CCM in general.
 
Endapo jairo hatajiuzulu, people must act. Watz tutaonekana wa ajabu sana kama jairo, ngeleja na malima hawatajiuzulu.

What people ? These same Tanzanians that I know ? Kwani rushwa imeanza leo !
 
Huwezi kufanya uchunguzi huru kama bado wako kazini
Na cha ajabu, hiyo barua ya Jairo isingefichuliwa na mbunge Takukuru ingekuwa haina habari kabisa. Hivi hawana kitengo cha intelligensia? Kwa sababu kila mara wanaposema wanachukua uamuzi wanafanya hivyo baada ya facts kuvuja hadharani.
 
Who knows! Kila anayefanya ubadhirifu anaogopwa na mkuu wa kaya. Jamaa naye kaamua kuibuka na hilo apate vijisenti kama wenzake. Siku hizi ukipata nafasi ya kazi kubwa katika wizara zenye ufisadi mwingi ukaondoka maskini watu wanakucheka. Jairo amefuata mkumbo tu. Kuna uvumi kwamba hata JK alipokuwa huko naye aliibuka na chake.

Majenereta na kampuni za kufua umeme kila Mkuu anazitaka yeye kaibuka na upitishaji bajeti. Usishangae JK akimwambia apime mwenyewe. Anyway sijui ni kampuni gani lakini nimeguswa na upuuzi huu wa watu wenye nyadhifa kubwa katika dola.
 
Cometh the moment,cometh the man.It is moments like this that separate the men from the boys. Will Hosea take the bull by the horns? Time will tell.
 
Ndugu zangu watanzania kuna jambo hapa bado sijalisikia likisemwa. Hivi waziri ngeleja yeye anasimamai wapi katika sakata hili la Jairo ina maana huu ulikuwa mpango wa wizara ua wa Jairo? Manake sijasikia Ngeleja akibanwa juu ya hili. Hebu nisaidieni hapo kuwa ngeleja naye atawajibishwa pamoja na Jairo au yamemfika Jairo mwenyewe?
 
Wakuu mimi binafsi natatizwa kidogo na kigugumizi ambacho serikali inaanza kuwa nacho dhidi ya hatua stahili zinazopaswa kuchukuliwa kwa katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo.

Kwa wale tuliomsikiliza Waziri Mkuu Pinda siku alipokuwa anaondoa mjadala wa Wizara hii tuliamini kuwa alikuwa akiongea kwa dhati kabisa kwamba scandal ya Jairo ilikuwa kubwa na serikali isingeweza kuivumilia hata kidogo na ingechukua hatua za haraka sana dhidi yake. Kwa hisia kali kabisa Pinda alishawishi akili za watu kuwa hatua stahili ilikuwa ni kufukuzwa kazi (pamoja na kwamba hakutamka sentensi hiyo lakini maelezo yake yalimaanisha hivyo). Pinda aliliambia bunge kuwa anasubiri bosi wake atue tu Afrika Kusini na amweleze yaliyojili na akaahidi kuwa wangekubaliana hatua za kuchukua na wasingeshindwana katika hilo.

Kinachonishangaza ni kwamba Pinda amekaririwa akisema kuwa amepewa maelekezo mapya. Baadae amekwenda mbele zaidi na kusema kuwa anasubiriwa rais aje kufanya maamuzi. Ninachojiuliza ni kwamba Pinda alitoa wapi ujasiri wa kutuaminisha kuwa angeweza kumalizana na bosi wake kwa simu na mambo yakaisha kama alijua kuwa hilo haliwezekani?

Je, si ni kweli kwamba Pinda alitumia lugha ile ili kupooza morali za wabunge ambazo kwa wakati huo zilikuwa juu sana? Hivi rais anaposafiri ina maana maamuzi yote nyeti ya nchi yanasimama? Nini maana ya kukaimisha ofisi? Ambacho kinamfanya rais ashindwe kufanya maamuzi hata akiwa nje ni nini? Kwa nini asubiriwe yeye? Akija atakuja kufanya nini? Kumhoji Jairo?

Napata mashaka sana juu ya utendaji wa serikali yetu. Nionavyo mimi inawezekana kabisa serikali inataka kupotezea suala hili. Hili linawezekana ili kuwanusuru Mabosi wa Jairo yaani Ngeleja na Malima. Kwa hali ya kawaida kabisa Ngeleja na Malima walitakiwa kuwajibika kwa kuachia nafasi zao kwa scandal hii.

Kwa mtazamo wangu naamini wao walikuwa wanajua kabisa juu ya suala hili na inawezekana ni wao walioratibu mpango huu. Hata kama sio wao basi kwa sababu limetokea kwenye wizara yao wangeachia ngazi kuonyesha dhana ya uwajibikaji. Inawezekana kwa nyuso zao zisizo na aibu wanaona hata Jairo asiondoke ili kujinusuru na wao! Nahisi serikali inataka kupotezea suala hili kwa sababu hata Jairo mwenyewe kwa kashfa hii hakupaswa kusubiri. Suala lilikuwa ni yeye kuachia ngazi mara moja na si kusubiri uamuzi wa rais.

Kwa hiyo inawezekana ameambiwa "SUBIRI, HILI NALO LITAPITA KAMA MENGINE"

Nawasilisha
 
Mkuu kama niaminivyo mimi.hapa hakuna tofauti na ze comedy!!
Kama alishasema kwamba hakuna kununua mgari na yakanunuliwa na kupewa yeye na akajiadai kuwa halitaki apewe mwingine pasipo kumwajibisha alofanya manunuzi. Unategemea kupata jipya hapa????
 
Mkuu issue hapa ni intention ya hizo hela siyo nani alichukuwa. Iko wazi kabisa hizo hela zilikuwa kwaajili ya kufacilitate kupenya kwa budget ikiwa na mapungufu yake.

Swali la kujiuliza hapa je masilahi ya kupita au kukataliwa kwa budget ile yalikuwa ya Jairo peke yake au ni ya wizara nzima? Ndiyo maana wamehusishwa idara na agencies zake kwa sababu ilikuwa kwa faida ya wote. Jairo ni mtendaji mkuu wa wizara lakini mwisho wa siku wenye maamuzi ya mwisho ni ngereja na malima. Kimsingi hapa ngereja imemkalia vibaya zaidi kuliko hata jairo japo barua ile haina signature yake. Kama angekuwa mwadilifu ngereja asingekuwa bado hajachia ngazi mpaka sasa hivi kwa kashifa hii.

Kimaadili uongozi wote wajuu wa wizara unatakiwa kuachia ngazi ndipo hatua za kisheria ziendelee kuchambua ni nani hasa ametenda kosa hilo. Kisheria atakayekamatika ni yule tu ambaye ushahidi utamkata kama hii barua ya Jairo.
umeona eee!
Sasa kumpeleka likizo yenye malipo mwizi ni stahili gani hii bwana luhanjo. Nchi hii inaongozwa kwa sheria au mtu? Natural justice kawaulize vibaka wanouawa kwa wizi kuku wa sh.5000-6000. Hiyo natural justice ambayo jairo anainjoi ni ufisadi pia .

Tatizo ni urafiki alio nao kikwete kwa jairo, kuwadi wake. Kama kuna natural justice how about babu na mwanae. Nyie hamna kitu hapa usanii mtupu 2015 naona mbali mno. Lazima muachie ngazi kwa kura, nguvu ya umma au kwa vyovyote vile.
 
Uozo uozo mtupu . Viongozi wa tanzania mbendembende. Hivi mnasubiri nini kumuondoa kabisa bwana jairo. Bwana harudi hadi desemba, 2012? Hatuna watu hapa . unaonaje mwizi wa kuku hana rufaa wa kusomewa mashtaka .hiyo natural justice the guy is enjoying where does it emanate? eti preliminary investigation? preliminary investigation si tayari barua mnayo? i thought you would impose detailed investigation so as to establish the magnitude of the petitions against mr david jairo.
 
anyway mm mwensijajua hivi bajet inapitishwa kwa kutumia pesa? au maoni ya wabunge ndio yanapitisha,.... sasa tujiulize vp kwa bajet zilizopita tayari, nako pesda imetumika au.... wizi mtupu pum**@#fu zao
 
285587_224280750941126_100000776075386_556463_2312589_n.jpg
 
UP TO DATE:

Tume ya bunge inatoa report yake sasa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom