Kashfa ya Jairo: Malipo ya zaidi Billioni 1 kusaidia Bajeti ipitishwe - Adai MP Beatrice Shelukindo

Status
Not open for further replies.

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Hakika Ngeleja Mungu kasikia kilio cha Watanzania,mama asiye na break Mrs shelukindo katoa mpya kwa kutoa waraka bungeni unaonyesha kuwa kila idala ndani ya wizara ya Nishati na Madini kutoa shilingi millioni 50 ,kwa ajili ya kuzituma kwenye account ya madini kitengo cha utafiti dodoma ili zitumike kwenye bajeti inayoendelea bungeni.

Mama shelukindo anataka kujua pesa hizo zimeenda kwa nani.kawasilisha nakala ya barua kwa spika,hofu kuna dalili zote za kifisadi kwenye isssue nzima hiyo

Ameleta kizaazaa ndani ya bunge hewa imechafuka kwa Ngeleja.kinachoendelea mwisho wake umefika.leo hii wanaojua kwenye Mkwanja huo watajuze huko?

UP TO DATE LEO TAREHE [19/11/2011]:
Taarifa ya tume ya Bunge inatolewa sasa ndani ya Bunge La Jamhuri ya Muungano,Who is Next?

Mwenyekiti wa tume amewasilisha report kuwa tume imeeona utaratibu uliotumiwa na katibu wa wizara ya madini bwana David Jairo hakuwa sahihi na hivyo ni kosa dhahiri kwamba yaliyotendwa na David Jairo hayakuwa na kibali toka kwa waziri wa fedha hivyo hakukuwa na kasma mahususi toka wizara ya fedha ama wale wote waliombwa kuchangia pesa hizo.
 
Huyu mama anatufaa CDM acha aseme akitoswa tunampa jimbo kama Shibuda.
 
Ngereja ana kazim ya ziada sidhani kama bajeti yeke itapita maana shelukindo kasema jioni atapeleka hoja binafsi kuomba wabunge waitose bajeti hiyo ili ikapitiwe upya na kurudishwa bungeni baada ya wiki tatu ili wabunge waijadili upya. Ole Sendeka katika mchango wake pia ameunga mkono hoja hiyo kabla haijawasilishwa.
 
Hata Sendeka hajaunga mkono hoja. Hapa kuna jambo . Ngeleja kawa mpole , leo wanamkaanga hata magamba wenzie.
 
Jamani hizi news mbona mnatuonjesha tu naomba mtupe zote ili tujue kinacho ila hii nchi. Ngeleja ana connection kwenye Richmund, Meremeta na EPA kwa hiyo Magamba itajifunza kwamba mtu yoyote mwenye connection na ufisadi wa aina yoyote inatakiwa aondoke.

Hapa pia inaweza kuwa trick ya huyu mama ambaye ni rafiki wa karibu na Lowassa kutumika kuwajibu akina Sita kwa kuanza kumwaga mboga baada ya kuwaoana dhahiri wanataka kumpiga chini.
 
Hakika Ngeleja Mungu kasikia kilio cha Watanzania,mama asiye na break Mrs shelukindo katoa mpya kwa kutoa waraka bungeni unaonyesha kuwa kila idala ndani ya wizara ya Nishati na Madini kutoa shilingi millioni 50 ,kwa ajili ya kuzituma kwenye account ya madini kitengo cha utafiti dodoma ili zitumike kwenye bajeti inayoendelea bungeni.

Mama shelukindo anataka kujua pesa hizo zimeenda kwa nani.kawasilisha nakala ya barua kwa spika,hofu kuna dalili zote za kifisadi kwenye isssue nzima hiyo

Ameleta kizaazaa ndani ya bunge hewa imechafuka kwa Ngeleja.kinachoendelea mwisho wake umefika.leo hii wanaojua kwenye Mkwanja huo watajuze huko?

Hapo RED,Watazigawana leo sasaba kabla ya kupitisha budget maana wana kikao.
 
Saa 7 hii mchana wabunge wa Magamba wanakutana katika kikao cha dharula ukumbi wa Msekwa,kujaribu kuinusu bajeti ya Ngeleja hapo jioni.Mjadala umekuwa mkali na 90% ya wabunge waliochangia wametangaza kutoiunga mkono bajeti hii.Hata spika Makinda alisha anza kupoteza utulivu ktk kiti wakati anasikiliza Makombora ya wabunge.Spika ameobwa atoe mwongozo ili bajeti hiyo ikafanyiwe marekebisho kwanza ili kuepuka aibu ya kukataliwa hapo baadae saa 11jioni.Lakini makinda anasema kama ni marekebisho basi muda huu kabla ya saa 11 jioni unamtosha waziri na watuwake kufanya marekebisho.Tusubiri tuone kitakacho endelea hapo baadae pamoja na hoja binafsi ya Mh.Mrs shelukindo.
 
Yawezekana JK aliagiza pesa hizo ilizikasaidie kulainisha wabunge wa CCM, wamekwenda kunyweshwa chai na vyuku. Yetu macho.
 
Jamani hizi news mbona mnatuonjesha tu naomba mtupe zote ili tujue kinacho ila hii nchi. Ngeleja ana connection kwenye Richmund, Meremeta na EPA kwa hiyo Magamba itajifunza kwamba mtu yoyote mwenye connection na ufisadi wa aina yoyote inatakiwa aondoke.

Hapa pia inaweza kuwa trick ya huyu mama ambaye ni rafiki wa karibu na Lowassa kutumika kuwajibu akina Sita kwa kuanza kumwaga mboga baada ya kuwaoana dhahiri wanataka kumpiga chini.

Bonyeza hiyo link hapo chini itakupeleka kwa browser ya wetransfer, litakupeleka kwa download then kuna faili lipo recoded la baadhi ya michango bungeni, sina uhakika kama inafanya kazi kwenye simu ila kwenye komputa itafanya kazi.

http://wtrns.fr/_dZ7KCoREbGAJM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom