KASHFA WIZARA YA AFYA: Yaajiri zaidi ya 'Madaktari' 80 wasiokuwa na sifa

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
549
Wiki moja iliyopita wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilitoa orodha ya majina na vituo vya kazi kwa waajiriwa wapya wa kada ya Afya kwa mwaka 2012/13 wakiwemo madaktari(Medical Doctors) 260. Zaidi ya wadaktari 500 wenye sifa stahiki walioomba ajira hizo wakiachwa kwa kukosa nafasi.

Lakini cha kuchangaza katika orodha hiyo hiyo kumegundulika zaidi ya majina 80 ya watu waliochaguliwa kwenda kufanya kazi za kidaktari(Medical Doctor) wakiwa hawana sifa kabisa yaani hawakuwahi 'kitaaluma' kufuzu kuwa madaktari wa kuweza kutibu watu hapa Tanzania.

Sifa kuu zilizokuwa zinahitajika ili kuweza kuajiriwa, mbali na sifa za msingi za kawaida(Uraia wa Tanzania, usiwe umestaafu nk) ni:

1/Shahada ya kwanza ya Utabibu(1st Degree of Doctor of Medicine)

2/Cheti cha kumaliza mafunzo kwa vitendo na kufaulu(Internship certificate)

3/Leseni 'hai' ya kufanyakazi za Kitabibu nchini Tanzania(Medical Practice Lecence(Active) From Medical Council of Tanganyika).

Hatua hii tayari imezaa kelele na manung'uniko mengi kutoka kwa baadhi ya madaktari waliokosa nafasi hizo za ajira na wakati huo huo imezaa woga kwa wagonjwa kuhusu ni kwa vipi watahudumiwa na madaktari hao 'vihiyo'.

SOURCE: Ofisi ya Msajiri wa Madaktari(Medical Council of Tanganyika)
 
Hii inawezekana kabisaaa....upangaji wa mwaka huu wenyewe ndo wanajua madudu waliyofanya
 
Mbna cjaelewa,hao madaktari wamegundulikaje
Issue iko hivi.
Madaktari(Medical Doctor) wote wanaofanya kazi hapa Tanzania ni Lazima kwanza wathitishwe kisheria na kupewa Leseni ya kuweza kufanyakazi za kutibu watu hapa nchini kutoka baraza la madaktari(MCT).

Sasa serikali ilipotangaza nafasi za Ajira katika kada ya Afya mtu yoyote(Mwenye sifa na asiyekuwa na sifa) aliweza kuomba ila wenye sifa tu ndio wanapaswa kuajiliwa.

Sasa orodha ya waliopata ajira hizo imetolewa huku wengi wenye sifa wakiachwa kwa kukosa nafasi, lakini baraza la madaktari limegundua kwenye orodha hiyo kuna majina zaidi ya 80 ya watu wameajiriwa kama madaktari(Medical Doctors) ambao hawajawahi kuthibitishwa popote pale kuwa ni madaktari 'kisheria na kitaaluma' na pia hawana leseni za Udaktari.
 
Kwa Tanzania vitu hivi vinazidi kuzoeleka. Na kama tutaendelea kuikumbatia CCM tutafika mahali tutaanza kushangaa nchi nyingine zikiwa na wataalamu wa kila aina wakati sisi tuna waganga njaa wakila aina ktk kila sekta.

Tukumbuke ya muhi2 mtu mwenye tatizo la goti kufanyiwa oparesheni ya kichwa na wa kichwa kufanyiwa mguu... Haya yote ni majanga!
 
Wiki moja iliyopita wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilitoa orodha ya majina na vituo vya kazi kwa waajiriwa wapya wa kada ya Afya kwa mwaka 2012/13 wakiwemo madaktari(Medical Doctors) 260. Zaidi ya wadaktari 500 wenye sifa stahiki walioomba ajira hizo wakiachwa kwa kukosa nafasi.

Lakini cha kuchangaza katika orodha hiyo hiyo kumegundulika zaidi ya majina 80 ya watu waliochaguliwa kwenda kufanya kazi za kidaktari(Medical Doctor) wakiwa hawana sifa kabisa yaani hawakuwahi 'kitaaluma' kufuzu kuwa madaktari wa kuweza kutibu watu hapa Tanzania.

Sifa kuu zilizokuwa zinahitajika ili kuweza kuajiriwa, mbali na sifa za msingi za kawaida(Uraia wa Tanzania, usiwe umestaafu nk) ni:

1/Shahada ya kwanza ya Utabibu(1st Degree of Doctor of Medicine)

2/Cheti cha kumaliza mafunzo kwa vitendo na kufaulu(Internship certificate)

3/Leseni 'hai' ya kufanyakazi za Kitabibu nchini Tanzania(Medical Practice Lecence(Active) From Medical Council of Tanganyika).

Hatua hii tayari imezaa kelele na manung'uniko mengi kutoka kwa baadhi ya madaktari waliokosa nafasi hizo za ajira na wakati huo huo imezaa woga kwa wagonjwa kuhusu ni kwa vipi watahudumiwa na madaktari hao 'vihiyo'.

SOURCE: Ofisi ya Msajiri wa Madaktari(Medical Council of Tanganyika)

nackia wizara imepewa nafasi za kuajili madaktari wa ziada 200, naamini wakiondolewa hao vihiyo madaktari wote watapata ajira kabisa
 
Hao watakuwa ni Waunguja na Pemba maana huko huitwa waganga wa Miti Shamba na Qur'an tukufu aka kutibu kwa albadili..Hamtaki mnaacha
 
Si kwa madaktari tu ni almost kad zote wamefanya uchakachuaji maana kuna wameajiriwa kama Pharmaceutical Technologist ilhali kwa sasa ni Pharmacist na wengine wako shule wanajiendeleza na wale wenye sifa na wanaohitaji nafasi wameachwa wanajaza nafasi then baadae wanaziuza kwa watu kwa kuzuga wale wengine hawakutokea this is very bad kwa kweli.
 
Na mfano mwingine..kuna majina yametokea mara mbili..mtu mmoja kapangwa mikoa miwili tofauti..km si wizI ni nini
 
Wiki moja iliyopita wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilitoa orodha ya majina na vituo vya kazi kwa waajiriwa wapya wa kada ya Afya kwa mwaka 2012/13 wakiwemo madaktari(Medical Doctors) 260. Zaidi ya wadaktari 500 wenye sifa stahiki walioomba ajira hizo wakiachwa kwa kukosa nafasi.

Lakini cha kuchangaza katika orodha hiyo hiyo kumegundulika zaidi ya majina 80 ya watu waliochaguliwa kwenda kufanya kazi za kidaktari(Medical Doctor) wakiwa hawana sifa kabisa yaani hawakuwahi 'kitaaluma' kufuzu kuwa madaktari wa kuweza kutibu watu hapa Tanzania.

Sifa kuu zilizokuwa zinahitajika ili kuweza kuajiriwa, mbali na sifa za msingi za kawaida(Uraia wa Tanzania, usiwe umestaafu nk) ni:

1/Shahada ya kwanza ya Utabibu(1st Degree of Doctor of Medicine)

2/Cheti cha kumaliza mafunzo kwa vitendo na kufaulu(Internship certificate)

3/Leseni 'hai' ya kufanyakazi za Kitabibu nchini Tanzania(Medical Practice Lecence(Active) From Medical Council of Tanganyika).

Hatua hii tayari imezaa kelele na manung'uniko mengi kutoka kwa baadhi ya madaktari waliokosa nafasi hizo za ajira na wakati huo huo imezaa woga kwa wagonjwa kuhusu ni kwa vipi watahudumiwa na madaktari hao 'vihiyo'.

SOURCE: Ofisi ya Msajiri wa Madaktari(Medical Council of Tanganyika)
Bila shaka itakua wamefanya vizuri katika masomo yao ya shahada ila bado tu hawajakamilisha taratibu za kupata hizo document nyengine, vinginevyo wasingechaguliwa. Kwa upande mwengine kuna madaktari ambao wamekamilisha vigezo vyote lakini performance zao ziko chini ukilinganisha na hao ambao wamechaguliwa bila kukamilisha document nyengine
 
mie mwenyewe kuna mtu namjua yuko pale sehemu eti ni daktari
wakati alisoma degree ya Sociologia sasa sijui kama siku hizi
mwana Sociology anaweza kuwa daktari
 
Jamani huu ni wizi....nimeona watu zaidi ya 20...majina yao yakijitokeza mara mbili...yani mtu mmoja kapangwa sehemu mbili. Hii ni kwa manufaa ya nani...ina maana huwa hawafanyi uhakiki wa wanachoandika...I wsh ningeyapost hayo majina hapa mjionee
 
inapokuja swala la afya ni sensitive issue siasa zikae pembeni wajiiriwa lazima wawe na viwango
 
Back
Top Bottom