Mbona huna busara mkuu. Ndo maana hukurudishiwaAliyeibiwa ni mimi au wewe?
Na waliahidi kurudisha salio langu ila mpaka kesho hawajanirudishia.
Pathetic!
Mkuu wanaiba..hizo huduma huwa wanaunganisha juu kwa juuVoda huwa hawaibi salio la vocha. Ukiwa unaona salio lako linapungua baada ya kiweka vocha jaribu kuhakiki mambo haya;
1. Angalia kama kuna huduma za kulipia ulizojiunga nazo. Mfano: Caller tune, huduma za kupata habari kama nipashe, kabumbu, mwananchi, sokoni, etc..
2. Angalia kama simu yako ni Tecno au Aitel. Hizi simu huwa zinakuwa na uwezo wa data hata zikiwa zile simu ndogo za burtton. Hakikisha umezima data.
Aidha, kama unatumia smartphone hakikksha umezima data kabla ya kuweka vocha.
3. Hakikisha hudaiwi nipige tafu.
Nasisitiza tena, VODACOM HAIWEZI KUKUIBIA VOCHA
Kuunganishwa juu kwa juu kweli inawezekana. Japo watu wengine hujiunga bila kujua.Mkuu wanaiba..hizo huduma huwa wanaunganisha juu kwa juu
Asante kwa maelezo yako. Hizo ni assumption tu,mwenye haki ya kubatilisha muamala ni yule aliyefanya. Hayo mengine ni ngumu kama kampuni kuthibitisha eti kwa kuhakiki kwa mpokeaji what if naye akasema uongo? Yaanze kufanya kazi za mahakama. Vodacom wanaweza vipi?Niliwahi kupata haya matatizo na huu mtandao na mawazo yangu kiukweli yalikua ni kama ya wengi waliochangia humu ila baada ya maelezo ya kina kutoka kwa mmoja wa mtu ndani niligundua yafuatayo....na kuanzia hapo nilipunguza kulalamika pindi napokosea kufanya muhamala kimakosa.
1.Sababu ya kuchelewa kurudisha pesa uliyotuma kimakosa,au kutoa kimakosa.
-kuna tabia kati yetu watanzania kupata huduma then ukamlipa mhusika kwa tigo pesa then mtu huyo huyo akaenda kupiga simu tigo kuomba zirudishwe,hapa tigo wakiamua kurudisha pesa bila kukoconfirm na receiver kampuni yao lazima iwajibike.
Eg:Mtu kalipa nauli(tax,bus) kwa tigo pesa then akishuka anapiga simu tigo kwamba alikosea,hapa tigo wakirudisha pesa bila kumchek receiver wanakua hawako sahihi.
-pia inatia mashaka kukosea kutuma hela kimakosa kwani process husika inatoa muda kuverifyy jina na number husika
2.Kuhusu kucheleweshewa pesa ili ziibwe na wafanyakazi wa tigo,hii pia sio kweli kabisa....katika taratibu za utumaji na upokeaji pesa kuna wahusika wawili tuu....mtumaji na mpokeaji(sender n receiver),endapo kuna kosa kati ya mmoja wao... Tigo wanachoweza kufanya ni either kurudisha kwa mtumaji au kuziacha kwa mpokeaji....there is no way ukai-divert pesa ya mteja into other number or channel,ndo maana unaona kuna kitu kinaitwa kumbukumbu namba....zile zinatumika kufunga na kurudisha mhumala husika uliokosewa.
NB:kwenye hizi huduma kuna changamoto ya mitandao kudelay na kuleta hasira kwa watumiaji lakini kubwa zaidi ni tabia yetu watumiaji kutokua waaminifu......hizi ni changamoto ambazo zinasababisha kwa kiasi kikubwa delays na baadae mis-interpretation ya huduma za mobile money
Mi nilifikiri niko peke yangu. Mwezi wa 11 mwaka jana nlilikosea tuma tigo pesa tsh 25,000/= nilifuatilia kupitia customer care kila mtu akawa akinipa majibu yake kila nilipo piga. Nimezungushwa wiki nikaamua kunyanyua mikoo juuu. Tarehe 31/12/2016 nikajikuta tena natuma tsh 60,000/= kimakosa kwenda namba ya tigo nikaambiwa ndani ya masaa 72. Nimepiga juzi nikaambiwa eti pesa nimesha rudishiwa tayari tangu tarehe 31/12/2016 ilihali saokweli. Nikachukua line ya tigo na kuitupilia chooni. Hawa jamaa tigo ni wezi sana!Huu ni upuuzi sana, nilishawahi mtumia mtu fedha kwa bahati mbaya akaibiwa simu kabla ya kuitoa, na sehemu aliyokuwepo hakukuwa na huduma ya kurenew sim card, hivyo akaniambia niwapigie simu wairudishe ili nimtumie kwenye no nyingine..
Niliwapigia hao jamaa simu nikawaeleza lakini wakalazimisha hadi wawasiliane naye, mimi nikawaeleza hali halisi jinsi ilivyo but walisumbua sana na mtu mwenyewe alikuwa na shida sana na pia hata kiasi nlichotuma kilikuwa kikubwa kiasi,
Ikabidi yule mtu aende mjini na ilikuwa ni mbali akarenew tu ile line, but baada ya siku kama nne!
Hapa naona tu kuna ujanja ujanja wanafanya, ikitokea uliyemtumia hatopatikana hewani tena au umekosea kutuma kwenye no ambayo haipo ni maumivi, million 2 inaweza kuwa vapour hivi hivi...
Basi kubali kuwa voda ni wezi wa salio.Mbona huna busara mkuu. Ndo maana hukurudishiwa
Wanafanya makusudi tu. Mimi niliituma hela from tigo pesa to crdb akaunti ya mtu mwingine. Kwenye salio langu hela ilitoka kwenye akaunti haikuingia.Nimekuwa mtumiaji wa mtandao wa [HASHTAG]#Tigo[/HASHTAG] toka mwaka 2005, nimeiona ikipitia katika hatua mbalimbali kihuduma hata kubadili brand ya Nina lao. Nawafaham vizuri. Katika jambo ambalo nadhani wanfanya vibaya kabisa ni katika kitengo cha huduma kwa wateja na [HASHTAG]#TigoPessa[/HASHTAG]. Nitatoa mifano michache.
Kama kunamtandao ambao wahudumu wao wanachelewa kupokea simu pale wanapohitaji msaada ni hawa Tigo. Na wengi wa vijana wale wanaopokea simu labda hawajafunzwa vizuri juu ya Yale wanayopaswa kusaidia wateja ama wamekaa mud a mrefu na kuifanya kazi ile kwa mazoea au no wachache kiasi kwamba unaweza kuwekwa online kusubiria hadi dakika 40+ au mpaka simu unakata yenyewe bila kupewa msaada.
Mwezi wa Tisa mwaka Jana nilienda kuwachukulia vijana Wang wawili Vyeti vya kuzaliwa pale RITA nikaambiwa na mtoa huduma nilipie Vyeti vile katika akaunti ya RITA ya tigo ambayo IPO pale ofisini jumla ya tsh 13,000. Baada ya kufanya malipo mhudumu yule akaniambia alikosea Kunipa maelekezo, na kwamba nilipaswa kufanya muamala mmoja mmoja kwa kila cheti (6,500 kwa kila cheti). Hivyo nikaamua kulipa tena 6,500 kwa kila cheti hivyo nikawa nimelipa jumla ya tsh 26,000 badala ya 13,000.
Ikabidi muda ule ule niwapigie [HASHTAG]#Tigo[/HASHTAG] kuwaeleza jambo hilo na wakanuambia nivumilie baada ya masaa 72 watanurudishua hela ile iliyozidi. Siku tatu zukapita nikawapigia, wakasema nisubiri 24hrs tena, lakini hakuna kitu. Nikawapigia tena wakanipa masaa 72 tena lakini PSA haijarudi.
Nikaenda ofisi kwao wakanipa tena 72 hrs lakini hakuna pesa iliyorudi. Mpaka muda huu zaidi ya miezi minne hakuna dalili zozote za kupata pesa hiyo.
Ukienda kuwaeleza TCRA kitengo cha huduma kwa wateja malalamiko ya namna hii utaishia kupewa vipeperushi juu ya huduma zao!...mambo ya MSI GI kama haya watakuambia wanayashughulikia lakini huwezi kuona mambadiliko yeyote. Nimeamua kunyamaza. Labda huto tupesa wanatotupiga tunawasaidia kuongeza mbwembwe mjini.