Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 127,883
- 244,449
Wakuu Naomba hili tuliangalie kwa jicho la tatu .
Kuna malalamiko mengi sana kuhusiana na ucheleweshaji wa kurudisha fedha za wateja zinazotumwa kwa makosa kwa watu wasiohusika .
Ukiongea na customer care unaambiwa fedha zako ziko salama na utarudishiwa ndani ya masaa 24 lakini hawarudishi hata baada ya wiki , ukiwauliza unaambiwa utaratibu ni lazima wawasiliane na yule uliyemtumia hela , na kwamba kutokupatikana kwake ndio sababu ya kuchelewesha kurudisha hela , uongo mtupu ! Maana ni kwamba wateja wote hata kama wako hewani , hakuna ofisa yeyote wa Tigo anayejishughulisha kuwapigia simu kama wanavyodai , Tatizo liko wapi ? Ni kweli kwamba baadhi ya watu wa kitengo cha fedha si waaminifu kama nilivyodokezwa na mtu wa jikoni ? Na kwamba wanasubiri baadhi ya wateja wakate tamaa ili wazipige hela zao ?
Viongozi wa TIGOPESA tupeni majibu .
NB - UZI HUU NI WA UCHUNGUZI NA UTAENDELEA KUONGEZWA NYAMA KWA KADRI TAARIFA ZINAVYOTUFIKIA .