Huu ni upuuzi sana, nilishawahi mtumia mtu fedha kwa bahati mbaya akaibiwa simu kabla ya kuitoa, na sehemu aliyokuwepo hakukuwa na huduma ya kurenew sim card, hivyo akaniambia niwapigie simu wairudishe ili nimtumie kwenye no nyingine..
Niliwapigia hao jamaa simu nikawaeleza lakini wakalazimisha hadi wawasiliane naye, mimi nikawaeleza hali halisi jinsi ilivyo but walisumbua sana na mtu mwenyewe alikuwa na shida sana na pia hata kiasi nlichotuma kilikuwa kikubwa kiasi,
Ikabidi yule mtu aende mjini na ilikuwa ni mbali akarenew tu ile line, but baada ya siku kama nne!
Hapa naona tu kuna ujanja ujanja wanafanya, ikitokea uliyemtumia hatopatikana hewani tena au umekosea kutuma kwenye no ambayo haipo ni maumivi, million 2 inaweza kuwa vapour hivi hivi...