Kashfa: Tigopesa wanadhulumu hela za wateja?

Kashfa: Tigopesa wanadhulumu hela za wateja?

Tigo ni majambazi hawafai wanahisa na matapeli wa mtandaoni milioni moja yangu imepotea hivihivi toka mwezi wa 2 mwaka hiu
 
Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba wafanyakazi wao ni wa kiwango cha chini sana , wengi ni wale wahitimu wa hizi Training college , kama Eagle Training college etc.

Mkuu nakubaliana Na hoja kuhusu Tigo,Voda Na airtel money kuhusu uhudumiaji wa wateja.
Ila sikubaliani nawe Kuhusu wahudumu wamesoma wapi.Hata kama umemaliza Harvard Au Oxfords kampuni itakufundisha namna wanavyo taka ufanya kazi Yao.
Matatizo yako kwenye wamiliki wa kampuni, sio Wafanyakazi maana mazungumzo yanarekodiwa kati ya mteja na mhudumu kwahivyo wamiliki wanafahamu yote.
 
Mtu mmoja usiku wa manane akiwa amelala usingizi mzito saa ile ile Natazama ikatwaliwa laki3 tigoni mwa pesa yake na mjoli aliyetambuliwa kwa jina la Grace Mbaga baada ya ufuatiliaji mkuu sana lakini duru zinaeleza kuwa michezo hiyo ni michezo ya watu wa tigo pesa wenyewe ndipo yule Ndugu aliyetwaliwa fedha yake akalia sana kilio kikuu asiweze kupewa fedha yake hata leo hii na hapo ilikuwa yapata wiki mbili zilizopita.
hahahahah
 
mkuu unatakiwa uvute subira hasa mimi nilirudishiwa baada ya mwezi na wiki tatu nlifuatilia mpaka nkachoka kila ukiwauliza wanakwambia vuta subira
Mm toka mwezi wa tano sh 26000 tu mpaka leo Mara ya mwisho huyo mdada ambae ni sijui mnamuita customer care alinijibu utumbo nikaamua kukaa kimya maana umri wangu haukuniruhusu kumrudishia utumbo alionijibu mpaka leo nimeshukuru mungu
 
Pole sana mkuu .
 
***
Erythrocyte
Kiriport ni lazima kuwe promptly on the sports kabla yule iliyomfikia hajafanya lolote,lakini akiwa sharp akatoa faster,sasa hapo Kampuni itakuwa imezuia nini?/
•BAADA YA KU-MISSEND TURIPOTI WITHIN A MINUTES.
Je kama umeripoti na tigo wamekubali kwamba hela yako ipo na imezuiwa lakini hawarudishi inakuwaje ? Halafu kingine ni hiki , kwanini kampuni kubwa kama hii wanakuwa waongo ? Uongo ni kati ya vitu vikubwa vinayoua makampuni mengi sana .
 
Tigo na wizi ni upendo wa mama kwa mwana ..

1. Nilinunua vocha yao, bahati mbaya katika kukwangua namba mbili za katikati zikafutika,. Nikawarudishia pale ofisini kwao kisha wakanipatia fomu nikajaza namba ya simu, jina na nikasaini.. Wakanambia watanirushia kama muda wa maongezi, matokeo yake hadi leo wananipiga dana dana na ni zaidi ya miezi saba sasa.

2. Baada ya kuishiwa salio, nikatumia huduma ya niwezeshe salio (dk 2 kwa tsh. 350), maajabu ni pale nilipoweka salio la tsh. 1000 wakakata 850 na kuniachia tsh 150 tu, nikaweka tena 500 bado wakakata 350 na kuniachia 150 kama kawaida yao. Kiufupi TIGO ni wezi na wanatumia ukimya na ujinga wa wateja wao kutukamatia chini.
 
Asante kwa ushahidi mwanana .
 
Ni mitandao yote iko hivyo kifupi swala la huduma kwa wateja hapa bongo ni sifuri!
 
Mbona Vodacom ukiwataarifu tu kwamba uwetuma pesa kimakosa hawana muda wa kushauriana na aliyetumiwa wanazuia pesa kwanza alafu ndani ya saa 24 pesa yako inarudishwa kwenye akaunti yako.
 
Niliwahi kupata haya matatizo na huu mtandao na mawazo yangu kiukweli yalikua ni kama ya wengi waliochangia humu ila baada ya maelezo ya kina kutoka kwa mmoja wa mtu ndani niligundua yafuatayo....na kuanzia hapo nilipunguza kulalamika pindi napokosea kufanya muhamala kimakosa.
1.Sababu ya kuchelewa kurudisha pesa uliyotuma kimakosa,au kutoa kimakosa.
-kuna tabia kati yetu watanzania kupata huduma then ukamlipa mhusika kwa tigo pesa then mtu huyo huyo akaenda kupiga simu tigo kuomba zirudishwe,hapa tigo wakiamua kurudisha pesa bila kukoconfirm na receiver kampuni yao lazima iwajibike.
Eg:Mtu kalipa nauli(tax,bus) kwa tigo pesa then akishuka anapiga simu tigo kwamba alikosea,hapa tigo wakirudisha pesa bila kumchek receiver wanakua hawako sahihi.
-pia inatia mashaka kukosea kutuma hela kimakosa kwani process husika inatoa muda kuverifyy jina na number husika
2.Kuhusu kucheleweshewa pesa ili ziibwe na wafanyakazi wa tigo,hii pia sio kweli kabisa....katika taratibu za utumaji na upokeaji pesa kuna wahusika wawili tuu....mtumaji na mpokeaji(sender n receiver),endapo kuna kosa kati ya mmoja wao... Tigo wanachoweza kufanya ni either kurudisha kwa mtumaji au kuziacha kwa mpokeaji....there is no way ukai-divert pesa ya mteja into other number or channel,ndo maana unaona kuna kitu kinaitwa kumbukumbu namba....zile zinatumika kufunga na kurudisha mhumala husika uliokosewa.
NB:kwenye hizi huduma kuna changamoto ya mitandao kudelay na kuleta hasira kwa watumiaji lakini kubwa zaidi ni tabia yetu watumiaji kutokua waaminifu......hizi ni changamoto ambazo zinasababisha kwa kiasi kikubwa delays na baadae mis-interpretation ya huduma za mobile money
UGWADU mimi nimetoa kwenye tigo pesa yangu na kupeleka kwenye account yangu ya bank. Sikukosea kitu chochote, hela imekatwa kwenye tigo pesa na haikuingia kwenye account ya bank. Hii ni siku ya 17 wananihangaisha tu.
 
Back
Top Bottom