BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,766
- 23,230
Huduma ya uzazi kwenye mahospitali ya serikali itaendelea kuwa majanga mpaka lini??
Mjomba Watu8 umeona kwa nini waheshimiwa wanakimbia hospitali ZETU???
Ndio maana bado nina majonzI baada ya naniliu kufilisiwa
Hahaha...waheshimiwa wana wodi na madaktari wao hata katika hospitali za serikali.
Wale ndugu zetu walifungiwa kwa kukosa kulipa pango, wenye jengo lao wakakosa uvumilivu...
Ila hali ya hospitali zetu ni mbaya jamani, haswa sehemu zinazohudumia wanawake...
Inasikitisha sana...
hii kesi unakula hela nzuri sana, kumbuka kesi ya bw. Hussein dhidi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo kwa ule mama
kuachwa na mkasi tumboni mwake baada ya operesheni
Mkuu ninaanza kwa kukuomba msamaha kama ntakukwaza;
Hebu jiulize, Umemaliza uchungu wa kumpoteza mtoto?
Hivi, huyo mtoto alikuwa na thamani ya shs ngapi?
Huyo mama ni shs ngapi bei yake? Najua huwezi nipa gharama zao. Hivyo, Mshukuru Mungu, mtoto hatunaye ila mama amanusura naye lakini kabaki.
Mtunze mama vizuri kabisa, apone tukimwomba Mungu, tutapata mtoto mwingine kwa mama huyu huyu. Mpango wa kupoteza muda na rasilimali muda kuzunguka sijui kwa dc, sijui kwa wakili etc. Huku ni kupotezeana muda na kujiongezea mastress bure.
Komaa na afya njema ya mama, mtoto ajaye apate nguvu ya kumbeba mwanzo mwisho.Waache hao wasio na huruma bali wasaka mshahara wa hilo lihospitali waendelee lakini ni mwisho kuuona uso wa huyo mama/mkeo/shemejio. Ni kaushauri tuu.
Mawazo ya kijima kabisa haya unatoa mkuu. Uzembe hauwezi kuisha namna hii kwa kuendelea kulalamika lalamika bila kuchukua hatua! Ushauri wako ni mbovu kabisa kabisa! Wahenga walisema ni bora kukosa mali kuliko akili.
Watu wa disaini yako mkuu ndio mnawarudisha hawa wazembe kila wakati wa uchaguzi huku mkibaki kulalamika pembeni! Hakuna tatizo litakaloisha kwa kulificha au kujifanya kama halipo wakati lipo.
Mkuu kwa niaba ya mhanga wa tukio napokea pole yako.
Ushauri wako nitaufikisha kwa mhusika ila siwezi kumlazimisha akubaliane na huo ushauri maana tambua mkuki kwa nguruwe mtamu ila kwa binadamu mchungu, ndivyo waswahili wanavyosema.
Mawazo ya kijima kabisa haya unatoa mkuu. Uzembe hauwezi kuisha namna hii kwa kuendelea kulalamika lalamika bila kuchukua hatua! Ushauri wako ni mbovu kabisa kabisa! Wahenga walisema ni bora kukosa mali kuliko akili.
Watu wa disaini yako mkuu ndio mnawarudisha hawa wazembe kila wakati wa uchaguzi huku mkibaki kulalamika pembeni! Hakuna tatizo litakaloisha kwa kulificha au kujifanya kama halipo wakati lipo.
Pole sana ndugu na wahanga wengine!
Palestina ya Sinza siyo penyewe kabisa Usipotoa rushwa au kuwa kichaa utampoteza mgonjwa wako hivi hivi!
Serikali inapaswa kuingilia kati...
Shida ni kwamba panya wote nao wanatamani kuwa kama Paka..nani atafunga au kufungwa kengele????