Kashfa mpya serikali ya Kikwete- waziri atishia wananchi bastola

Ni mapema mno kusema ni kashfa ya serikali ya JK.....kashfa nyingine si za serikali za mtu binafsi hadi pale itakapothibitishwa serikali imejiingiza officially kumkingia kifua na uhalifu huo kama kweli ulitokea.
hapo hakuna chakuuliza maana au kutomlalamikia JK hii stori haipishani na ya Waziri wake aliyekutwa Morogoro na,"SMG"!,Dollar 4000,Laptop 3,Bastola vyote hivyo wewe unadhani vilikuwa vya nini??Je JK kamchukulia hatua gani??Je hiyoSMG ingekutwa kwa raia sasa hivi huyo raia angekuwaje kama siyo maiti??acheni kurema kwenye maswala ya msingi lazima JK alaumiwe yeye na serikali yake!!Wewe umeona Polisi wanasema nini??leo ukikutwa na bastola wewe ni jamabazi na unapigwa risasi kwenye msitu wa mabwepande je SMG siunakatwa shingo??
 
Huu nao ni uwaziri wa kishamba kabisa. Hivi kwa level ya waziri kuna mlinzi au mtendaji gani wa kijiji mwenye ubavu wa kumkagua. Alikuwa ana sababu gani ya kutumia hiyo bastola? Hivi angeshuka tu wamuone kwamba ni yeye angepata shida gani? Au yeye hakuwemo kwenye gari? Na hivyo gari yake ndiyo ilitumika kufanya vitengo vya kihalifu? Na kama ni hivyo unaweza ukakuta Nyalandu mwenyewe hajui, unaweza kumwazima gari mtu halafu akaenda kuitumia kufanyia kitu kibaya sana bila wewe kujua.
 
Lazaro is one of huligan, tuliosoma naye tunashangaa madaraka aliyopewa, anyway nchi ya kutupiana pande. WATU TUWE macho na tukumbuke wakuu wa nchi walikuwa wasanii hivi hivi tukapumbazika na mikogo yao, sasa tunalia

"huligan" ndio kitu gani...........?
 
Wakuu kwenye hizi road block za maliasili magari madogo huwa hayakaguliwi, kama taratibu zimechange tuambiane, si nia yangu kumtetea nyalandu, nia yangu ni kuwa tufike kwenye jawabu sahihi kwa formula tutakayoiderive!
 
Singida kuna nyara gani? Au wake za watu?

Safari_ni_Safari

Je, wewe ni mgeni katika nchi hii???

Hujui kwamba nchi hii ya Tanzania imejaa RASLIMALI ZA KILA AINA KILA KONA? Singida nina uhakika kuwa kuna DHAHABU iko kwa wingi tu na madini ya aina nyinginezo mbali na WANYAMA toka mbuga za Wanyama zilizoko jirani na Singida kama Serengeti. Nyalandu siyo malaika anaweza akatuma jamaa zake wakawinda Tembo,Faru n.k kupata pembe zake na wakamwambia aje achukue mzigo kwa kutumia wadhifa na ubabe wa Serikali ya CCM.

Maana kama hilo gari lake halikuwa na kitu chochote cha WIZI/UFISADI/UHUJUMU UCHUMI kwanini walikuwa hawataki kusimamia kwenye check-points hizo ambazo zimewekwa kwa kibali maalumu cha Serikali. Hawa lazima walikuwa wanatorosha nyara, ni nyara gani wanajua wao maana hakuna waliposimamishwa na kukaguliwa.

Kwanza katika Mawaziri wa Serikali ya Kiwete Bwana Nyalandu ni mmojawapo wa Mawaziri bomu kabisa katika Baraza lake. Sijui hasa alipewaje nafasi hiyo kwa sifa ipi hasa. Lakini anyway Kiwete na Nyalandu ndiyo wanajua.
 
Ground of Great Thinkers; mie nina pata utratra hapo kidogo labda mtoa Thread anaweza nisaidia;
1. Je wanakijiji hao walithibitisha kuwa huyo alokuwemo kwenye hilo gari ni Nyalandu?
2.Kama gari haikukamatwa na wanakijiji hao majina ya walokua kwenye hiyo gari kwa usiku huo wameyafahamu vipi wakati hawakushuka kwenye gari?
3. Je kama walinzi walijidhatiti kimapam bano pale barier na walikua na NIA ya kuwazuia majangiri kwann wasingetumia silaha zao kupambana nao kwa hicho kibastola walikotishiwa nacho
 
Lazima tuifuatilie hii asante kwa taarifa mkuu kwani ulinzi wa taifa ni jukumu letu wote wakuu
 
Mmm,this is too much.Nadhani inatosha sasa,these guys must go.
a
Msihukumu haraka bila kuchunguza. Kwani wezi hawawezi kughushi namba za gari la Nyalandu?
Acheni vyombo vya dola zifanye kazi. Tutaujua ukweli tu. Najua Nyalandu ana maadui wengi wanaotaka kumvurugia mambo yake.
Nyaraka za serikali hazilindwi kwa rungu. Silaha maalum lazima zitumike.
 
Hii kitu ni mbaya sana; lkn Mtoa habari hujatuambia kama kuna jitihada yoyote ambayo ilifanyika kuwaarifu police haraka kwa usiku huo ili kuomba msaada wa kulifukuzia gari hilo kwa usiku huo kabla ya kwenda kufungua jalada na kupata RB kama ulivyotujuza; je huko Singida hakuna utaratibu wa Ulinzi shirikishi?
~Ktk Check Point hizo walinzi walikua na silaha za aina gani?
 
ni tukio la aibu na kusikitisha. nawapongeza wanakijiji kwa kuwa imara kupata taarifa zaidi za hao wezi. kwa vyovyote kulikuwa na kitu kinafichwa. ni vigumu kwa wanakijiji wale kujua kwa mazingira ya tukio zima yalivyo, ila lililowazi ni kosa la jinai lililotendwa na waziri. wanakijiji wasitulie mpaka haki ionekane imetendeka.
 
Katika kile kinachoonekana kuwa ni kitu cha kawaida kwa viongozi wa serikali kuwa wababe (wenye tabia ya kijambazi) na kulindwa na serikali yao. Naibu Waziri wa Viwanda na biashara Lazaro Nyalandu, tarehe 11/04/2012, saa 6:00 Usiku katika Kijiji cha Mwanyonye, Lazaro Nyalandu na watu wengine waliotajwa kuwa nao ni Elia Digha pamoja na Reuben walifika na gari No. T.505 BKM, aina ya VX, walikuta kizuizi kilichowekwa na serikali kwa ajili kukagua mazao ya wanyama na misitu, walishuka na kuwatishia walinzi kwa bastola, wakavunja kizuizi, na kuondoka na taa ambayo walinzi hao waliitumia. Baada ya tukio hilo Wanakijiji wa Mwanyonye walipiga simu kijiji kinachofuata. Kijiji kinachofuata ni Kinyeto, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinyeto na walinzi walijizatiti ili wazuie ile gari itakapofika, walipofika mtu mmoja alishuka kwenye gari haraka akiwa amenyoosha bastola na kuwauliza walinzi mnafungua au hamfungui, walikataliwa, wakavunja kizuizi. haijulikani Nyalandu alikuwa anatorosha nini katika mazingira hayo. Ila walinzi walipopiga picha gari hiyo, na kuchukua namba za usajili, waliripoti polisi mapema kufungua jalada SI/IR/1570/2012 KWA KOSA LA KUTISHIA KUUA KWA BASTOLA. Walinzi na watendaji walienda TRA kuomba umiliki halali wa gari T. 505 BKM, wakazuiliwa mpaka wapate kibali cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, walipewa na walipoenda TRA nao wakathibitisha mwenye gari ni Lazaro Nyalandu. Taarifa za kuaminika inasemekana Nyalandu alikuwa anatorosha Nyara za serikali. Pesa zimemwagwa Singida kuanza kurubuni waandishi wa habari, na maofisa wa usalama wanahaha kusaidia habari hizi zisitoke. Ila kwenye JF Where we dare to talk openly tumeweka jamvini. hii ndio serikali yetu.

Umechelewa kuileta kwani navowajua magamba issue itakuwa imeshazimwa, na nyarandu anaendelea kutesa na kauwaziri kake.
 
Ni mapema mno kusema ni kashfa ya serikali ya JK.....kashfa nyingine si za serikali za mtu binafsi hadi pale itakapothibitishwa serikali imejiingiza officially kumkingia kifua na uhalifu huo kama kweli ulitokea.

Haya ndo madhara ya kupeana ulaji na matokeo yake uwajibikaji unakosekana. Viongozi wetu wengi wa awamu ya nne aidha wamepewa nafasi kiushikaji au kwa sababu za kidini. Na hii ndo sababu kuu ya matatizo tunayoyapata sasa. Serikali ya JK haiwezi kuzikwepa hizi lawama. Laiti Kama JK angekuwa anawachagua Watu kutokana na sifa na uadilifu wao, naamini haya matatizo yanayoikumba Tanzania yasingekuwepo kabisa.
 
Back
Top Bottom