Kenya: Afisa Wa Serikali atishia shambulio la Al Shabaab baada ya kushindwa kesi ya Shamba Mahakamani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,028
1,633
Italipuka hapa!" Afisa mwenye hasira atishia shambulizi la kigaidi baada ya kupoteza kesi mahakamani.

Maafisa wa polisi katika eneo la Transmara Narok wanachunguza afisa wa serikali mwenye cheo kikubwa aliyenaswa kwenye kamera akitaja kikundi cha kigaidi kwa lengo la kuwatisha wananchi kwenye mzozo wa kibinafsi kati yake na wakazi wa eneo hilo.

Katika video hiyo, ambayo imesambaa sana mtandaoni, Naibu Kamishna wa Kaunti ya Transmara Kusini (DCC) Abdihakim Mohamud Jubat anaonekana akiwatisha wakazi wa kijiji cha Olempongiot katika eneo la Transmara Mashariki.

"Kitu mimi nakudhibitishia, Leo mimi na kundi langu tutakuja kulala hapa...al shabaab itakuwa hapa...italipuka," alisema Jubat katika video.

Tukio hilo lilitokea baada ya uamuzi wa Mahakama ya Mazingira na Ardhi huko Kilgoris kufuta hati ya umiliki ya ekari 43 ambayo DCC alidai kununua kutoka kwa familia ya James Laton Konchellah mwaka 2013.

Mahakama iliamua kuwa ununuzi wa ardhi uliofanywa na Jubat ulifanywa kwa njia isiyo halali na isiyo ya kawaida.

Walakini, Jubat anadai kuwa ameomba rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Mwanafamilia amesema kuwa Mahakama iliamua kuwa ardhi ile ni yao baada ya kusubiri rufaa kutoka kwa Jubat kwa siku 14, hivyo inataka serikali ichukue hatua dhidi ya naibu kamishna wa kaunti

"Serikali inapaswa kuingilia kati haraka katika suala hili kwani DCC alitumia ugaidi kututishia

Inasemekana kwamba ardhi inayozozaniwa imekuwa chini ya uchunguzi wa polisi na maafisa hao wanaopiga doria katika ardhi hiyo wanadaiwa kufanya kazi kwa maagizo ya Jubat.

Mkuu wa Kaunti ya Narok, Isaac Masinde, anasema serikali inatambua suala hilo na kwamba taasisi husika za usalama zinashughulikia suala hilo.

Chanzo: Citizen Digital
 
Afisa wa serikali anawatishia ugaidi wananchi na hatafanywa chochote, subirini mtaona. Hii ndo afrika na hii ndo Kenya!
 
...al shabaab itakuwa hapa...italipuka," alisema Jubat katika video.

Hayo ni maneno tu kama mimi nikisema ntakupiga ngumi za Tyson wakati hata speed hiyo sina
Au nitishe kuwa ntapigana kama Russia na Ukraine

Hapo anaongeza nguvu kwenye maneno tu
 
Katika nchi ambayo kuna mashambulizi ya kigaidi na huchukua uhai wa raia wake huo haukuwa mfano sahihi wa kutumia kwa kiongozi mkubwa kama yeye.

Kwa kutamka alshaabab tu amegusa vidonda vya wahanga na kuzua taharuki, mpaka sasa hakupaswa kuwa ofisini.
 
Katika nchi ambayo kuna mashambulizi ya kigaidi na huchukua uhai wa raia wake huo haukuwa mfano sahihi wa kutumia kwa kiongozi mkubwa kama yeye. Kwa kutamka alshaabab tu amegusa vidonda vya wahanga na kuzua taharuki, mpaka sasa hakupaswa kuwa ofisini.
Hakutumia hekima kwa hilo
Hapo umenena
 
Back
Top Bottom