Katika kile kinachoonekana kuwa ni kitu cha kawaida kwa viongozi wa serikali kuwa wababe (wenye tabia ya kijambazi) na kulindwa na serikali yao. Naibu Waziri wa Viwanda na biashara Lazaro Nyalandu, tarehe 11/04/2012, saa 6:00 Usiku katika Kijiji cha Mwanyonye, Lazaro Nyalandu na watu wengine waliotajwa kuwa nao ni Elia Digha pamoja na Reuben walifika na gari No. T.505 BKM, aina ya VX, walikuta kizuizi kilichowekwa na serikali kwa ajili kukagua mazao ya wanyama na misitu, walishuka na kuwatishia walinzi kwa bastola, wakavunja kizuizi, na kuondoka na taa ambayo walinzi hao waliitumia. Baada ya tukio hilo Wanakijiji wa Mwanyonye walipiga simu kijiji kinachofuata.
Kijiji kinachofuata ni Kinyeto, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinyeto na walinzi walijizatiti ili wazuie ile gari itakapofika, walipofika mtu mmoja alishuka kwenye gari haraka akiwa amenyoosha bastola na kuwauliza walinzi mnafungua au hamfungui, walikataliwa, wakavunja kizuizi. haijulikani Nyalandu alikuwa anatorosha nini katika mazingira hayo. Ila walinzi walipopiga picha gari hiyo, na kuchukua namba za usajili, waliripoti polisi mapema kufungua jalada SI/IR/1570/2012 KWA KOSA LA KUTISHIA KUUA KWA BASTOLA.
Walinzi na watendaji walienda TRA kuomba umiliki halali wa gari T. 505 BKM, wakazuiliwa mpaka wapate kibali cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, walipewa na walipoenda TRA nao wakathibitisha mwenye gari ni Lazaro Nyalandu.
Taarifa za kuaminika inasemekana Nyalandu alikuwa anatorosha Nyara za serikali. Pesa zimemwagwa Singida kuanza kurubuni waandishi wa habari, na maofisa wa usalama wanahaha kusaidia habari hizi zisitoke. Ila kwenye JF Where we dare to talk openly tumeweka jamvini. hii ndio serikali yetu.