Kashfa mpya: Kamati ya Bunge yahongwa

Mkulima

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
1,034
1,022
Hii ni kamati ipi?

Kashfa mpya: Kamati ya Bunge yahongwa
• Katibu wa Bunge akiri kufahamu tuhuma hizo

na Mwandishi Wetu (Tanzania Daima)


IKIWA takribani wiki moja sasa tangu gazeti hili liliporipoti jinsi wabunge wanavyochuma mamilioni ya fedha kupitia malipo yao halali ya mishahara, posho na fedha nyinginezo zinazotokana na malipo yao rasmi wanayostahili, baadhi ya wabunge wametuhumiwa kuhongwa zaidi ya sh milioni 200 na kampuni moja binafsi ili kuipa upendeleo.

Habari za uhakika zilizolifikia Tanzania Daima Jumatano zinadai kuwa, wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge (majina tunayahifadhi kwa sasa), walihongwa na kampuni ambayo pia tunahifadhi jina lake kwa sasa, ili wasiikwamishe kupata mradi iliyokuwa ikiunyemelea.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa, kamati hiyo ya Bunge yenye wabunge kadhaa machachari wakiwamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ilipewa fedha hizo ili kuwaziba mdomo wajumbe wa kamati hiyo, wasihoji uwezo wa utendaji wa kampuni unaodaiwa kuwa ni wa kiwango cha chini kulingana na ukubwa wa mradi iliyoomba kuutekeleza.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa sharti la kutotaja jina lake gazetini, alithibitisha yeye na wanakamati wenzake kupewa fedha hizo.

Alisema suala hili lilifanyika kwa tahadhari kubwa kwani hakuna ushahidi unaoweza kuwatia hatiani kuhusu kuchukua fedha hizo.

Uchunguzi wa kina wa timu ya waandishi wa gazeti hili umebaini kuwa, tayari viongozi wa juu serikalini wamekwishapata taarifa za kamati hiyo kuhongwa, na wameamuagiza Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah kuchunguza tuhuma hizo na kutoa taarifa.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, serikali ilishtushwa na taarifa za wabunge hao kuhongwa, kwa kile kilichoelezwa kuwa baadhi yao walikuwa wakichukuliwa kama viongozi wa kupigiwa mfano.

Kwa mujibu wa habari hizo, serikali imetoa pia kazi ya kuchunguza tuhuma hizo kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama ambavyo vitatoa taarifa kwa viongozi wa juu serikalini.

Akizungumza na gazeti hili jana kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu kuwapo kwa tuhuma hizo, Katibu wa Bunge, Dk. Kashillilah alikiri kuwa na taarifa hizo, lakini alieleza kuwa hajapata maelezo ya maandishi kutoka serikalini ya kumtaka kuchunguza suala hilo.

“Ni kweli nimesikia kuhusu jambo hilo, taarifa hizo ninazo, kuna kitu kama hicho, lakini sijapata barua rasmi kutoka serikalini inayonitaka kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo.

“Hata hivyo, mimi sina nguvu za kufanya uchunguzi kama huo hata kama nikitakiwa kufanya hivyo, lakini jambo linalonishangaza, na kwa kweli siamini, ni kama barua hiyo ambayo ni ya siri sana imenyofolewa kutoka katika ofisi za Bunge.

“Lakini baadhi ya wabunge wanajua ni kwa nini wanafanya hivi! Mimi sina ruhusa ya kutoa maelezo kuhusu mambo ya Bunge, msemaji ni Spika, akielekeza jambo kwangu naweza kulitolea ufafanuzi. Na ni vizuri uelewe kuwa hawa wabunge ni viongozi wakubwa, sasa kuzungumzia tuhuma zao magazetini ni jambo kubwa mno.

“Tuvute muda, ngoja niwasiliane na wakubwa, nikiwa katika hali ya kulizungumzia hili, nitatoa maelezo. Lakini kwa sasa ninachoweza kusema ni kwamba sijui ni kamati gani, na ilipewa sh ngapi,” alisema Dk. Kashillilah.

Naye Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alipoulizwa kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu tuhuma hizo, alijibu kwa ufupi kwamba hana taarifa zozote kwa sababu hakuwapo ofisini kwa siku kadhaa, na kwamba aliingia nchini jana akitokea nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo, Spika Sitta aliahidi kuwa atawasiliana na wasaidizi wa ofisini kwake ili kujua kama kuna barua yoyote kutoka serikalini inayotaka wabunge wanaotuhumiwa kwa kosa hilo kuchunguzwa.

Kwa muda wa takribani mwezi mmoja sasa, kumekuwa na malumbano baina ya wabunge, huku baadhi yao wakishutumiana kwa kuhongwa na kukiuka maadili ya ubunge.

Malumbano hayo sasa yanaonekana kuanza kuchukua sura ya kuumbuana baada ya baadhi ya wabunge kuanza kutoa siri za wenzao ambazo hapo awali zilikuwa zimefichika
 
Kamati Machachari kuna ya Shelukindo, Dr. Slaa, Zitto na mama Kilango.

Mama Kilango ni maadili, sidhani ana nguvu kwenye kupendelea miradi. Dr. Slaa sidhani kama yake ina uhusiano na miradi.

Hapo naamini itakuwa kamati ya Shelukindo au ya Zitto.
 
Kamati Machachari kuna ya Shelukindo, Dr. Slaa, Zitto na mama Kilango.

Mama Kilango ni maadili, sidhani ana nguvu kwenye kupendelea miradi. Dr. Slaa sidhani kama yake ina uhusiano na miradi.

Hapo naamini itakuwa kamati ya Shelukindo au ya Zitto.


Yote haya ni kwa vile ni 1-4-2009
 
Kamati Machachari kuna ya Shelukindo, Dr. Slaa, Zitto na mama Kilango.

Mama Kilango ni maadili, sidhani ana nguvu kwenye kupendelea miradi. Dr. Slaa sidhani kama yake ina uhusiano na miradi.

Hapo naamini itakuwa kamati ya Shelukindo au ya Zitto.

Na kwa kuwa habari imetolewa na 'Tanzania Daima' it is unlikely ikawa ni kamati ya Zitto (labda kama yeye hakuhongwa!).
 
Hii habari mboni haipatikani kule kwenye 'chanzo'?..Aithee acheni ujinga bana..thikukuu imeishaisha ..Thaa iidhi thaa tano na robo, nyie vp na sherehe zisowahusu kuzivalia kibwebwe? Ebo!
 
maadili mtu alikua muuza unga. DOnt be stupid..


Thibitisha!!! Uzuri wa JF tunaenda kwa vithibitishao kwa issiue nyeti!!! Weka hapa jinsi huyu mama yetu alivyoshiriki biashara ya unga. Weka mtandao wake na ni mara ngapi alishafikishwa kwa pilato au moja ya hiyo mitandao!!! Tusipende kuchafuana. Au nayo ni part ya wajinga leo, ili wajinga waamini kuwa mama ni madau katika unga!! ??? Halafu ni ya siku ya Wajinga!!! Tanzania Daima leo hakuna habari hii!!!!!
 
Wana JF leo waoga kweli kuchangia, wanaogopa wasifungwe magoli na sikukuu ya Wajinga.
 
MODS ipelekeni hii mada kunakohusika..Kule kwenye kona ya Udaku na Kuvunja Mbavu
 
Wana JF leo waoga kweli kuchangia, wanaogopa wasifungwe magoli na sikukuu ya Wajinga.

Mkuu muda wa sikukuu ya wajinga umeisha......sahivi ni saa sita kasoro, na shughulia zile huisha saa NNE asubuhi saa za Afrika Mashariki!
 
Mimi sishangai ,kwani watatanzania ni tuko kama wadudu. hatujui tunachokifanya na bora hata hao wadudu. mtatanzanıa hana thamani popote pale duniani pamoja ndani ya nchi yake. tumekua kama mifugo tunayoongozwa na bakora ndefu(serekali). mtu anaiba mamilioni ya umma , na bado anadunda mtaani .mtu aliyekamatwa na sigara ya bangi anahukumiwa kama muhalifu. ndio maana wazungu wanasema "we are died men walking" . mimi vile vile mbongo . msinune tuambizane ukweli.
 
Kinyambiss,

Acha uhuni bwana! Una maana mama yetu alikuwa mwuza unga?

Kweli hii inawezekana pia ni siku ya wajinga.

Labda anamaanisha ana mashine za kusaga nafaka kule Same anasambaza unga wa sembe!!!! Kama ni mengineyo naanza kurudia yale yale, kwamba sasa wezi wanatugeuzia kibao. Na bado. Kamati inayolengwa sina shaka kwamba ni ya Kina Mwakyembe na tutasikia mengi sana mwaka huu hadi tuwaachie kina Lowassa na Rostam wapete, vinginevyo kila kukicha kutakuwa na mapya. Kwa sasa nazidi (nilikuwa) kutilia shaka Tanzania Daima. Nitafafanua siku nyingine.
 
Hii habari mboni haipatikani kule kwenye 'chanzo'?..Aithee acheni ujinga bana..thikukuu imeishaisha ..Thaa iidhi thaa tano na robo, nyie vp na sherehe zisowahusu kuzivalia kibwebwe? Ebo!
Mkuu,ipo sana tu labda hujacheck vizuri.Kashfa mpya: Kamati ya Bunge yahongwa
suala sasa ni kuwa ni kutokana na leo kuwa siku ya wajinga,au Tanzania Daima wameamua kumbeba mbunge kijana&RA.Maana tangu lianze lile la kamati mbili kutaka kukutana naona TD limekuwa na taarifa zenye mrengo flan hivi ambao sina hofu kuuita ni wa kutetea maslahi ya 'mafisadi' na 'watetea ufisadi'
But kama wameandika as a result of fools day,then they should know that kuwa makini ktk kufuatilia ujinga na viambata vya ujinga ikiwemo siku yao nao ni UJINGA vilevile.Sasa adanganyae leo anaweza jihisi/jiona kuwa amewafanya wengine wajinga but to my percpective is that he/she belong to the same group.Period
 
Back
Top Bottom