Labda anamaanisha ana mashine za kusaga nafaka kule Same anasambaza unga wa sembe!!!! Kama ni mengineyo naanza kurudia yale yale, kwamba sasa wezi wanatugeuzia kibao. Na bado. Kamati inayolengwa sina shaka kwamba ni ya Kina Mwakyembe na tutasikia mengi sana mwaka huu hadi tuwaachie kina Lowassa na Rostam wapete, vinginevyo kila kukicha kutakuwa na mapya. Kwa sasa nazidi (nilikuwa) kutilia shaka Tanzania Daima. Nitafafanua siku nyingine.
Mkuu Halisi,
Hawa Tanzania Daima nao wamepata virus vya Rostam nini?
Nimeona makala zao kama mbili tatu, nikakuna kichwa kwamba kulikoni hapa?