KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 10,569
- 21,075
Mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni za kuwania nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani, zimeingia dosari baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Mwanga, Ibrahim Mzava, kudaiwa kuendesha mchakato huo kwa ubaguzi wa dini pamoja na kuomba rushwa kwa baadhi ya watia nia wa Ubunge kwenye jimbo hilo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro.
Sauti iliyovuja inamuhusisha Mwenyekiti huyo, ikisikika akizungumza na mmoja wa watia nia, wakijadiliana umuhimu wa nafasi ya Mbunge wa jimbo, ikishikwa na mtu anayetokea kwenye dini ya uislamu.
Sauti hiyo ilisisitiza kwamba ili mchakato huo uende vizuri, lazima mgombea awe Muislamu badala ya watu wa imani nyingine.
#KitengeUpdates