Kasheshe vituko na vitimbwi vya mimba

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
169,837
2,000
Acha kabisa hii maneno
Kuteseka ni lazima kwa mama hata kwa baba pia
Huruma zaidi huja pale mimba inapomgeukia baba na kuwa kama yeye ndio kaibeba! Yaani vichefu chefu vyote yeye malimao mbilimbi na ubuyu ni yeye. .huwa inatia huruma mno
Miezi tisa ya ujauzito si safari rahisi asilani kuna mengi hapo yanayohitaji kujitoa na uvumilivu wa kiwango cha juu mno
.mimba zina hulka ya kupenda watu fulani
.mimba zina hulka ya kuchukia watu fulani bila sababu
.mimba zinaleta hasira na kisirani
.mimba zina tabia ya kupenda sana ama kuchukia sana vyakula vya aina fulani (usiombe mjamzito akose akitakacho ni shida kubwa)
.baadhi ya mimba huja na na baraka lakini nyingine huja na mikosi
.baadhi ya mimba ni kuugua mwanzo mwisho na baadhi ni kutapika kila kinachoingia mdomoni kwa miezi yote tisa
Inasemekana mimba za watoto wa kiume ndio zenye mateso sana kuliko zile za watoto wa kike
Jamani jamani jamani kwa wale ndugu zangu ambao ndio wanatarajia kupata watoto wa kwanza figisu za mimba zaweza kuwa kitu kigeni kwao...nawashauri sana mkiona mabadiliko wakati wa ujauzito wa shemeji jitahidini kuvumilia kwakuwa sio wao na si kwamba wanafanya kusudi ni hio hali waliyo nayo
-mkeo anaweza kuongeza wivu maradufu! vumilia
-mkeo anaweza kuwa mtu wa kususa na kuzira hata kwa kitu kidogo kabisa! vumilia
-mkeo anaweza kuwa na ongezeko la hamu ya kufanya ngono au kupoteza hamu kabisa! Vumilia
Yapo mengi mengi mno yatokeayo kipindi cha ujauzito na kama ndio unaingia kwenye ndoa na mimba hapo hapo unaweza kuona maisha ya ndoa ni jehanam kubwa...Vumilia baada ya miezi 9 yote huisha na furaha ya kiumbe kipya hutamalaki
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
169,837
2,000
1469032223360.jpg
 

sister

JF-Expert Member
Nov 23, 2011
9,017
2,000
Ah mie embe hapana nilikuwa napenda ubuyu..... Kipindi hicho ofisi iko karibu na imalaseko supermarket.....asubuh napitia ubuyu wangu....unaliwa mpaka nikitoka. Napitia pweza na supu yake....nikifika nyumbani barafu natafuna mpaka meno yanakufa ganzi......ila sasa haya yote siwezi kuyafanya....mimba kiboko.....
 

shaks001

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
1,246
2,000
Mwanaume ukiwa na wivu kipindi hicho unaweza ukaua mtu pindi mimba ya mkeo ikawa inampenda mwanaume fulani kama ilivyonitokea mimi.

Mke wangu wakati wa ujauzito alikuwa anampenda sana rafiki yangu wa kiume mpaka ikafika kipindi nikitaka kutoka naye kwenda clinic mpaka amuite yule rafiki yangu twende naye.Kingine alikuwa anapenda sana kula soseji-hii ilinitia adabu,maana bajeti yake haikuwa mchezo.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
169,837
2,000
Usicheke mwathuu wanchosha hawa kila saa Kasinde n mwathuu n mwathuu haaaaa na wanibatize niitwe Nakadori ama Naki ama Neteghenjwa.....

Wanchosha kwerikweri. .... na wathomee haiyee Kasie si mwathuu ni mbeba mizigo aka reli ya kati. ..
Kwani Kasie wee ni mrefu kwenda down?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom