Je bidhaa zote zinazoagizwa nje haziwezi kuzalishwa baadhi ndani ya nchi na ikawa fursa kwa Watanzania

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
1,006
1,171
JE BIDHAA ZOTE ZINAZOAGIZWA NJE HAZIWEZI KUZALISHWA BAADHI NDANI YA NCHI NA IKAWA FURSA KWA WATANZANIA ?
Wakuu kutokana na changamoto ya ukosefu wa ajira na salary kutokukidhi kwa wale wenye ajira naona Ni vema tukashirikishana Kila Aina ya Fursa inayoonekana au kupatikana

Viongozi mada ya Leo tuangalie Fursa za kiuchumi na Kijasiriamali ambazo zinaweza kutokana na kuzalisha bidhaa ambazo zinaagizwa nje

Kanuni mojawapo na rahisi ya kuongeza na kukuza uchumi wa nchi ni kuongeza mauzo ya nje ( exports)na kupunguza uagizwaji wa bidhaa za nje

Kwa rekodi ya haraka bidhaa ambazo zimekuwa zikiagizwa nje
Oil Mineral fuels
Industrial machinery
Motor vehicles & parts
Iron &steel
Plastics
Electrical machinery
Pharmaceutical
Chemical products
Iron steel article s

**Fats and oils
Wheat
Rice
Palm oil
Dairy products

Kwa Leo ningependa tuanze kuangalia zaidi bidhaa za chakula ambazo ambazo kiuhalisia Kama watanzania ziko ndani ya uwezo wetu kwa Sasa

Kuna andiko moja liliandikwa linasema

Why food potential exporters still import food
Pia wakaeleza kwamba

Tanzania agricultural sector is sleeping giant

Tukiachana na mipango mingi ya serikali juu ya kilimo
Lakini naamini sisi Kama wananchi tunayo nafasi zetu Fursa kupitia sector binafsi kufanya Jambo

Nikianza na mfano wa ngano kuagizwa nje
Naamini Kuna maeneo mengi ambayo tunaweza kulima ndani ya nchi na tukachukua Fursa ya Hilo soko la nje na pengine kupunguza Bei ya bidhaa zinazotokana ngano

Huu ni mfano tu na Maoni yangu Ila Kila mmoja anaweza kutoa Maoni yake
 
Hiyo idea ilishindikana tangu enzi ya Mwalimu Nyerere alikuwa na malengo mazuri ya nchi kumiliki viwanda ila waliomzunguka wakawa wanamrudisha nyuma kwa kuviua viwanda kwa makusudi.
 
Usinikumbushe samaki.kuna kipindi tulikuwa tunanunua samaki kilo moja 4500.zikaja siasa samaki wa kichina sijui nini .wakapigwa stop halafu wakaanza kuja samaki wanaopishana vipimo.na bei ikipanda 1000,1000 kila mwaka na sasa ni kilo moja TShs 11,000 Morogoro mjini.nani wapetevu au wamechina sababu ya umeme.
 
Usinikumbushe samaki.kuna kipindi tulikuwa tunanunua samaki kilo moja 4500.zikaja siasa samaki wa kichina sijui nini .wakapigwa stop halafu wakaanza kuja samaki wanaopishana vipimo.na bei ikipanda 1000,1000 kila mwaka na sasa ni kilo moja TShs 11,000 Morogoro mjini.nani wapetevu au wamechina sababu ya umeme.
Hao samaki wanaopishana vipimo ni wa kutoka wapi
 
Tanzania ipp uchumi huria, hizo bidhaa inawezekana kuzalisha, cha kufanya ni wew hapo kuanza kuzalisha bidhaa moja wapo, waambie na marafiki zako wazalishe nyingine,

Tuache kulilia serikali kitu
 
Tanzania ipp uchumi huria, hizo bidhaa inawezekana kuzalisha, cha kufanya ni wew hapo kuanza kuzalisha bidhaa moja wapo, waambie na marafiki zako wazalishe nyingine,

Tuache kulilia serikali kitu
Kila kitu lawama Kwa serikali, serikali iki-devalue shillings dhid USD ili ku-discourage importation mayowee yanapigwa kama wote, serikali ukifungua mipaka mazao yauzwe nje ili kukuza export na kuongeza fedha za kigeni bado mayowee yanapigwa yaani watz hatunaga jema.
 
Back
Top Bottom