Karibuni Ruangwa

Sawa bwa shemeji yaishe ..jannaino salama pe
 
Ruangwa ni jehanamu ndogo nliishi miaka miwili sitamani tena kurudi uko asee...
1. Maji shida ya kwenye visima vya kuvuta na kamba Tena ya jumvi maji ya mamlaka ya maji yanatoka mara moja kwa wiki.

2. Gharama za maisha ziko juu mfano vitu vinasafirishwa kutoka mtwara na masasi nakumbuka kuna siku nimezunguka wilaya nzima hakuna mkate wilaya haina ata kiwanda cha mkate kweli ni wilaya hii? Bei ya nyama kilo moja tu iko juu sana around 8000

3. Hakuna fursa zozote zaidi ukiacha kilimo cha ufuta na korosho wilaya ya ruangwa iko nyuma sana yaani ata uanzishe kitu apo kitakufa maana muitikio ni mdogo sana na mzunguko wa pesa ni mdogo kupita kiasi..apo kuna kiji lodge kimoja ndio kinaogopwa kua nicha kisasa.

4. Usafiri wa shida kwakua hakuna miundombinu mizuri rami iliyopo ni km azizid 8 uku udongo mwekundu ukitaradadi pamoja na ukame...kampuni zaMabasj azifiki ata 6 maana nakumbuka kuna SB, Shivu, Mashallah na vicosta costa ambapo vinakuja baada ya masaa 2 ndio vinapatia na kurudi vijijini .

5. Majungu na fitina ukitaka usitoboe nenda kwa wamwela asee aufanikiwi utaanza pigwa figusu na majungu balaa hautafanikiwa na biashara yako wao wanapenda majungu , unafiki kufatilia maisha ya mtu binafsi pasipo kufatilia biashara yako wana muattack mtu direct.

Kuna mengi zaidi ya haya, mfano kuabudu watu ukiwa unafahamiana na mtu fulani mkubwa unaogopeka sana ata kama mtu kavunja sheria kisa anajuana na mtu fulani basi anaogopwa,

7. Halmashauri haina mapato nakumbuka kampuni flani ilikua inadai kama 3M ilichukua miaka 4 na sidhan mpk mda huu kama imelipwa.
Watumishi wengi walikua wanaacha kazi na kuomba uhamisho kuhama kwasababu wanaishi maisha ya dhiki sana just imagine shule inawanafunzi 200 walimu 3 hakuna huduma bora za kukidhi viwango nyumba za walimu tu ziko katika hali mbaya.

8. Elimu kwa wakazi ni ndogo sana kijana anakomaa akijua soma na kuandika basi inatosha anakua boda boda vijana wengi hawapendi shule kabisa, ata shule za Advance zenye ubora hakuna ipo shule Moja tu ya Advance Mbekenyela wilaya nzima hakuna shule ya advance ata private ni hatari hii...
 
Tatizo mikoa ya kusini ina laana na uchawi umezidi,mnarogana sana,hayo unayoita maendeleo ukicompare na maeneo mengine ni takataka tu,kusini haitakuja kuendelea kamwe
Sana Siyo kuloga tu Pia wanaoneana wivu wenyewe kwa wenyewe
 
hiki kitakua ni kijiji cha Primitive Communalism
 
Mtumieni majaliwa vizuri dakika za mwisho mwisho hizi 2025 waziri Mkuu mwingine.
 
Neno zuri sn mkuu
 
Kale katabia ka kupenda kupumzika zaidi mmekaacha siku hizi au bado kapo. Maana mitaa hiyo kazi ngumu ngumu hatutaki.
 
hiki kitakua ni kijiji cha Primitive Communalism

Mtoa mada amezani kua hatujawai kuishi uko, mkuu na kwambia pale ni hatari mtu anaefanya kazi halmashauri Masijala anaogopwa sana kuliko ata mtendaji wa kijiji na ukiwa unafanya kazi CRDB au NMB maana bank zipo izo mbili tu utatafuna wanawake wote maana wao wamekalili watu ao ndio wanapesa ...

Trafik wanakimbizana na Boda boda maana wilaya nzima ata wanaomiliku magari private hawafiki 35 utamkamata nani kila mtu anajuana na mkubwa
 
Ishu ya wafanya kazi wa kiume kung'oa mademu kirahisi ipo hata huku usukumani aisee wadada wa huku washamba sana wanatudharau sisi mafundi seremala ila wenzetu wanang'oa.
 
Kwamba wanawaona wana kuliko wachimbaji wa Namungo??
 
Ilikua mwaka gani mkuu,kwamba Ruangwa Lami haifiki Km 8 ok huenda upo sawa,kuhusu shule za advance zipo zaidi ya hio idadi...Kitu cha ukweli ulichoongea hapo ni kuhusu majungu ya wamwera tena bro bora Ruangwa mjini ukizama vijijin ndo utajua hujui,wanapenda majungu kuliko kula
 
Hivi unachosema ni kweli Manispaa ya Lindi kuwa na shule moja ya advance??

Kama ni kweli tz bado tuna safari ndefu sana

wakati kata ninayotoka ina shule za advance mbili.
 
Uliyoyaongea ukweli kabisa sina la kuongeza
 
Ruangwa anayoizungumzia ni hii ya lindi au ipo nyingine africa ya kusini. Sirudi tena ruangwa hata nilivyoviacha acha vipotee. Kule nashukuru sana kupata kiongozi mkubwa angalau anawainua. Kila kitu garama usije jaribu kuanza biashara ukaona Kua eti ni fulsa sababu vitu utajuta Hakuna pesa
 
Hivi unachosema ni kweli Manispaa ya Lindi kuwa na shule moja ya advance??

Kama ni kweli tz bado tuna safari ndefu sana

wakati kata ninayotoka ina shule za advance mbili.
YMkuu usiamn yot advance zlo nyingi mbekenyera n arts (pure arys) ,nkowe high school (pure science i e PCM,pCB,CBG), hpo hawa mchopa, hipo majali ruangwa high school ,nk hzo data zake n za mwaka 70s .
 
Wananchi na wakazi wa Ruangwa tuna bahati sana na iwapo tutatumia bahati hiyo basi tutanufaika sana katika level ya mtu mmoja mmoja, vikundi, vyama mashirika na hata taasisi nk.
Mwaka huu nilikuwa na NGO moja ambayo nilizunguka nayo Jimbo la Mchinga (Mabebery yameshanusa gesi). Katika safari zetu tukafika kijiji kimoja kinaitwa Rutamba. Nikiwa pale nikabahatika kufika hadi kwa Mzee Membe kwa sababu sio mbali na Rutamba ingawaje kule kwa Membe hakukuwa kwenye mpango wetu. Nilitamani sana nifike hadi Ruangwa manake nilioneshwa barabara ya Ruangwa lakini inaonekana barabara ile gari nyingi hazifiki Ruangwa. Je, hivi sasa kuna magari ya kufika Ruangwa? Naulizia hivyo kwa sababu kuna kitu nimekipenda pale Rutamba na nina mpango mwaka huu wakati wa likizo niende tena pale. Ningefurahi sana nikikamilisha mishe mishe zangu pale Rutamba, basi niende hadi Ruangwa ili nako nikacheki fursa
 
Kama ndivyo, basi Katelephone nae ni fisadi mwingine manake hai-make sense mkoani pawe na shule moja tu wakati wilayani, tena wilaya ya pembezoni na ya juzi juzi tu hapa wawe na shule 6! Lakini siwezi kushangaa manake nasikia hata Bohari ya Madawa ipo Ruangwa wakati Ruangwa yenyewe ipo kushoto kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…