Karibuni mjiunge na chama cha kijamii

Swali lamsingi kabisa hilo unasema la kipuuzi? nnahisi yumo lakini kama "kawa" anajifanya hayumo.
Mwanakijiji yupo humo na ndio mwenye hii ID alioanzishia hii thread. hapo ndio huwa nashindwa kumuelewa huyu Mwanakijiji amepewa pesa kiasi gani na mtu ambaye yuko nyuma ya chama hiki.
 
Haya sasa imeshakuwa Mwanakijiji... Jamani mwanakijiji hawezi kushindwa kujiunga na chama na akatueleza hapa janvini. Maadam chama hiki kimeundwa makhsusi kuua nguvu ya Upinzani nitawasikiliza na kuwaacha kama walivyo kwa sababu naamini kitu kimoja tu nacho ni kwamba UMOJA ni NGUVU.. Mtu yeyote anayejiona yeye mbora zaidi na kuanzisha chama kwa sababu ya Uongozi wa vyama vingine hunipa mashaka na kufikiria kwake kwa sababu vyama vyote 16 vimeanzishwa nchini kutokana na watu kutokubaliana na viongozi wa chama tangulizi.

sasa ikiwa mtu kashindwa kukirekebisha chama alichotoka, akashindwa kuwasiliana na wengine nje ya Itikadi, sera na ilani ya chama inanipa wasiwasi zaidi..Binafsi nilitegemea sana kutokea kwa chama ambacho kitaviunganisha vyama vyote vya Upinzani isipokuwa Chadema, NCCR na CUF kwa sababu ambazo viongozi waliotangulia walishindwa kushirikiana. Sasa kinapotokea chama kingine kama hiki japokuwa kimenigota haswa ktk ITIKADI yake bado kinanipa wasiwasi na malengo yake haswaa..

Lakini pamoja na yote haya Siasa za Bongo kwa asili yetu ni za makundi na haya matumizi ya Itikadi hayatakiwi kabisa kwa sababu tuneongozwa na mila na desturi za Kiafrika zaidi ya Itikadi za wazungu (vitabuni). Hata hivyo tunaomba uongozi wa chama hiki cha CCK watueleze vizuri kina nani viongozi wao na wameshindwa vipi kujiunga au kuungana na vyama vingine vya Upinzani.
 
Unavyofanya ni vyema kwani hizi siasa zisitufanye mpaka tusisaidiane tunapofikwa na shida au isifikie mpaka tusizikane, Watanzania tuna asili ya kupendana na kusaidiana bila itikadi za chama wala imani.

Hao wanaojidai wanasiasa wenyewe ni wapo kwa maslahi tu, mfano mzuri ni pale wanapokuwa hawateuliwi kugombea nafasi za kula wanapoamua kuhama vyama. Tumeyaona kwa wengi tu. Siwalumu kwa hilo, wakale wapi? Polisi?

Umelitambua leo hii? CCM wameonyesha njia mbaya kwa hiyo wanaambukiza na vyama vingine vyenye kutaka kuleta maendeleo. Nape anakuchunia kwa sababu anaona unajipotezea mda CCM haitakiwi tena na wananchi bora utoke kwenye hilo chama ndugu yangu
 
Haya sasa imeshakuwa Mwanakijiji... Jamani mwanakijiji hawezi kushindwa kujiunga na chama na akatueleza hapa janvini. Maadam chama hiki kimeundwa makhsusi kuua nguvu ya Upinzani nitawasikiliza na kuwaacha kama walivyo kwa sababu naamini kitu kimoja tu nacho ni kwamba UMOJA ni NGUVU.. Mtu yeyote anayejiona yeye mbora zaidi na kuanzisha chama kwa sababu ya Uongozi wa vyama vingine hunipa mashaka na kufikiria kwake kwa sababu vyama vyote 16 vimeanzishwa nchini kutokana na watu kutokubaliana na viongozi wa chama tangulizi.

sasa ikiwa mtu kashindwa kukirekebisha chama alichotoka, akashindwa kuwasiliana na wengine nje ya Itikadi, sera na ilani ya chama inanipa wasiwasi zaidi..Binafsi nilitegemea sana kutokea kwa chama ambacho kitaviunganisha vyama vyote vya Upinzani isipokuwa Chadema, NCCR na CUF kwa sababu ambazo viongozi waliotangulia walishindwa kushirikiana. Sasa kinapotokea chama kingine kama hiki japokuwa kimenigota haswa ktk ITIKADI yake bado kinanipa wasiwasi na malengo yake haswaa..

Lakini pamoja na yote haya Siasa za Bongo kwa asili yetu ni za makundi na haya matumizi ya Itikadi hayatakiwi kabisa kwa sababu tuneongozwa na mila na desturi za Kiafrika zaidi ya Itikadi za wazungu (vitabuni). Hata hivyo tunaomba uongozi wa chama hiki cha CCK watueleze vizuri kina nani viongozi wao na wameshindwa vipi kujiunga au kuungana na vyama vingine vya Upinzani.

Mkuu Mkandara labda nikuondowe wasiwasi ili uelewe dhahiri shahiri kwamba CCJ ndio CCK, ili ni genge la wanasiasa wenye uchu wa pesa na madaraka ambao wanaamini hawawezi kupata madaraka endapo watajiunga kwenye vyama vilivyopo, halafu kibaya zaidi chama hiki asilimia kubwa ya wamiliki wake ni wanachama wa CCM, hiki ni chama cha kupigwa vita kama alivyofanikiwa Msajili wa Vyama ndugu Tendwa kukifutilia mbali baada ya kugunduwa ni chama cha wababaishaji.

Ila ningemshauri Mwanakijiji kuendelea kukipigia debe chama hiki ni sawa na kujivunjia heshima na kuwataka watu waanze kumpuuza na kumuona ni mtu wa hovyo tu, maana tusitumie neno Demokrasia kutaka kuwavuruga Watanzania, huu ni uhuni siwezi kukiunga mkono chama hiki kamwe.
 
Umelitambua leo hii? CCM wameonyesha njia mbaya kwa hiyo wanaambukiza na vyama vingine vyenye kutaka kuleta maendeleo. Nape anakuchunia kwa sababu anaona unajipotezea mda CCM haitakiwi tena na wananchi bora utoke kwenye hilo chama ndugu yangu
Sasa mkuu unataka kuturudisha kwenye chama kimoja? mwache yeye abaki CCM ila tushindane kwa nguvu za hoja, atakapoelemewa kwa hoja itakuwa ni juu yake kupima na kuchukuwa hatuwa.
 
Tawi lingine la ccm limechipua...mnatujazia mivyama ili kupunguza kura zetu za kukimaliza ccm
 
asante lakini hatuhitaji utitiri wa vyama, CHADEMA wameonyesha kama ndio chama mbadala, kama vipi join them ili tuwe na chama chenye nguvu kuliko kila siku kuja na tuvyama tudogotudogo tusitokua na ushawishi wowote, huwezi kujenga chama kwa miaka minne, na sie tuataka kuchuka nchi 2015 sasa we ubaongea habari za chama kipya leo?
 
HOTUBA YA UTAMBULISHO WA CHAMA KIPYA CHA SIASA NCHINI CHA CCK

Kwanza nikupongeze kwa wewe na viongozi wenzako kupata usajili wa Chama chenu baada ya kupitia misukosuko mingi. Pili, pia nikupongeze kwa ujasiri wa kutuletea maelezo kuhusu chama chenu humu JF, kwani huo ni ujasiri wa hali juu, ukizingatia kwamba wengi wasio waelewa wa dhana ya demokrasia kazi yao kubwa itakuwa ni kuwavunja tu moyo. Usife moyo kwa kauli chache za ovyo ovyo dhidi yenu, mwanzo wenu ni mzuri. Kama ulivyokwisha baini hadi sasa humu JF, maoni ya wengi yanatoa tafsiri kwamba vyama vilivyopo vinatosha. Lakini wengi humu wanasahau kwamba "to everything, there is an opposite". Kwahiyo, while Chadema inaanza kuwa mbadala kwa wengi wa CCM, kwa principle ya 'to everything there is an opposite', basi pengine ni CCK, NCCR etc, ndio kitakuwa an opposing force to whoever manages to remove CCM from the political map in Tanzania. Lakini siri ya mafanikio ya kweli na ya kudumu katika hilo ni vitu vitatu: Itikadi, itikadi, na itikadi.

Ushauri wangu mdogo kwenu ni kwamba mna changamoto kubwa sana ya kuonyesha umma nini mnaleta ambacho hakiwezi letwa na vyama vingine vilivyopo.

Kwa mtazamo wangu, mnachoshindwa na waliopo ni vitu ambavyo ni vya mpito: wenzenu wana majina/great personalities, wamesha capitalize kwenye mlinganyo wa umaskini kwa walio wengi na ufisadi; wana experience na siasa za uchaguzi; na mwisho, wapo mstari wa mbele katika mchakato wa katiba mpya ambao utakuwa sehemu kubwa sana ya siasa za mwaka 2015. Vinginevyo, hakuna chama hadi sasa chenye uwezo wa kweli wa kubadilisha maisha ya mtanzania kwani itikadi zao zote zina mapungufu, na hili nilishalielezea sana huko nyuma. Itikadi yenu ya uhafidhiana ina lengo zuri kwa maana ya preservation ya masuala mengi katika jamii yetu, in the context of economic development. Lakini hapa kuna conflict of interest kwani pamoja na umuhimu huo, suala la modernity wengi wanaliunganisha na maendeleo. Vile vile uhafidhiana kanuni zake za uchumi hazijali watu wa kada ya chini.

Vinginevyo mje na kitu kama 'african conservatism', ambayo itakuwa more towards the centre of the ideology spectrum, na ikiwezekana, centre left kuelekea social democracy. Mchanganyiko huo - wa kuhifadhi tamaduni zetu na taasisi zake lakini vile vile ujamaa wa kidemokrasia ambao utavumilia uwepo wa ubepari na soko huria, lakini kwa kuwa na sauti juu ya tabia, mwendeno na kasi ya ubepari na soko huria Tanzania, ili vitu hivi viwepo lakini kwa manufaa ya wakulima na wafanyakazi, na sio kuachia ubepari na soko huria uendeshwe kama wanavyotaka WorldBank na IMF, kitu ambacho ni moja ya udhaifu mkubwa wa CCM na Chadema kwa sasa. Suala hili linachangia sana umaskini katika Tanzania ya leo kuliko hata ufisadi. Inawezekana CCM na Chadema hawa challenge madudu haya ya IMF na WorldBank kwasababu wao ndio wanawapatia mlo. Lakini maelezo yenu kwamba hamtakuwa mnategemea ruzuku, kama kweli mtafanikiwa katika hili, basi hiyo itakuwa moja ya silaha yenu kubwa sana ya mafanikio, kwani ina maana hamtanunulika na mafisadi, lakini pia hamtaendeshwa na wahisani kama wanavytaka wao.

Mkiweza fanikisha haya yote, hakina mnaweza kujipatia a unique space katika anga ya siasa za Tanzania. Otherwise hongera sana na karibu sana JamiiForums.
 
Lakini pamoja na yote haya Siasa za Bongo kwa asili yetu ni za makundi na haya matumizi ya Itikadi hayatakiwi kabisa kwa sababu tuneongozwa na mila na desturi za Kiafrika zaidi ya Itikadi za wazungu (vitabuni). Hata hivyo tunaomba uongozi wa chama hiki cha CCK watueleze vizuri kina nani viongozi wao na wameshindwa vipi kujiunga au kuungana na vyama vingine vya Upinzani.

Mkuu Mkandara,

Itikadi haitakiwi kuwa kitu imported, lakini sisi tunafanya hivyo pengine kutokana na kukosa fedha, hivyo kuamua kuiga ya wafadhili ili tupate pesa za kuendesha siasa na vyama vyetu. Vinginevyo hata mababu zetu kabla ya ukoloni walikuwa na itikadi zao. itikadi haizaliwi na chama cha siasa, bali ni zao la jamii, hata ile inayoishi kwa kuokota matunda porini. Vyama vya siasa huwa tu vinachukua itikadi zilizopo katika jamii na kuzi package katika programu ya kisiasa na sera mbalimbali halafu kuanza kushawishi umma kwamba wao kama chama/vyama wapo kwa ajili ya kutetea itikadi zao mbalimbali.

Wewe unaishi Canada, je unataka kuniambia hapo majirani kwenu - wale wahindi wekundu, hata kama hawaishi katika modernity, unataka kuniambia katika jamii zao hawaongozwi na itikadi zozote unique to their surroundings?
 
Mkuu Mkandara labda nikuondowe wasiwasi ili uelewe dhahiri shahiri kwamba CCJ ndio CCK, ili ni genge la wanasiasa wenye uchu wa pesa na madaraka ambao wanaamini hawawezi kupata madaraka endapo watajiunga kwenye vyama vilivyopo, halafu kibaya zaidi chama hiki asilimia kubwa ya wamiliki wake ni wanachama wa CCM, hiki ni chama cha kupigwa vita kama alivyofanikiwa Msajili wa Vyama ndugu Tendwa kukifutilia mbali baada ya kugunduwa ni chama cha wababaishaji.

Ila ningemshauri Mwanakijiji kuendelea kukipigia debe chama hiki ni sawa na kujivunjia heshima na kuwataka watu waanze kumpuuza na kumuona ni mtu wa hovyo tu, maana tusitumie neno Demokrasia kutaka kuwavuruga Watanzania, huu ni uhuni siwezi kukiunga mkono chama hiki kamwe.

Watu wanaowapiga vita Sita, Nape, Mwakyembe kujiunga na CCJ mpaka kuitwa wasaliti wanasahau kwamba, uamuzi wa kamati maalum ya Mzee Mwinyi, Kinana na Msekwa ulikuwa kuwafukuza watu hawa, kilichobakia kilikuwa ni utekelezaji tu wa kuwafukuza. Ni mazingaombwe tu yalitokea wakabakizwa ndani ya CCM. Ni vizuri mkaelewa issue yote ilivyo unfold kabla ya kuwaona hawa wana uchu wa madaraka, wasaliti wa CCM n.k.
 
6. Ushirikiano na vyama vingine vya upinzani Tunapenda ieleweke mapema kabisa kuwa hatuna uadui na chama chochote cha upinzani na hatuna sababu ya kushindana na chama kingine cha upinzani ambacho malengo yake yanakaribiana nay a kwetu. Ugomvi wetu na mgogoro wetu ni Chama cha Mapinduzi na uongozi wake kwa taifa.

Hivyo, tunatangaza uadui wa kudumu na CCM na tutashirikiana na chama chochote kile ambacho kina lengo la kuona CCM inaondolewa madarakani. Hata hivyo, ushirikiano huo utategemea kukubaliana kwa sera mbalimbali siyo kukubaliana kwa kuondoa CCM tu madarakani.

Unataka kuniambia kuwa hapo kwenye rangi ya bluu itakapofika siku za uchaguzi mtatangaza kuwa wapeni kura chama fulani kwa kuwa tuna mlengo mmoja au mtafanya kama yule jamaa aliyekuwa anagombea uraisi mwishoni akajitoa na kusema wapiga kura wake wampe kura zake JK au unamaanisha nini?

Nina wasiwasi sana na hapa kwenye rangi nyekundu, kwa sababu hata baadhi ya vyama vilivyowahi kujifanya vyama vya upinzani kama hiki chako, waliwahi kutoa au kuahidi kama unavyosema hapo kwenye nyekundu lakini mwisho wa siku walikuja kufunga ndoa ambayo hata wewe nadhani unaifahamu vizuri sana tu.

La mwisho, ni kwa nini umebwabwaja sana maneno mengi kuhusu chama chenu ilihali ungetubandikia humu katiba ya chama chenu ingejieleza na nadhani kusingekuwa na mlolongo wa maswali mengi humu kama katiba yenu ingekuwa na kile vyama vya upinzani wameshindwa kukifanya na kufanya tufike hapa tulipo. Tunaomba katiba kwanza, hii ndo inaweza kutufanya tuwaamini au tusiwaamini
 
Watu wanaowapiga vita Sita, Nape, Mwakyembe kujiunga na CCJ mpaka kuitwa wasaliti wanasahau kwamba, uamuzi wa kamati maalum ya Mzee Mwinyi, Kinana na Msekwa ulikuwa kuwafukuza watu hawa, kilichobakia kilikuwa ni utekelezaji tu wa kuwafukuza. Ni mazingaombwe tu yalitokea wakabakizwa ndani ya CCM. Ni vizuri mkaelewa issue yote ilivyo unfold kabla ya kuwaona hawa wana uchu wa madaraka, wasaliti wa CCM n.k.
Kwahiyo unaweza kumshawishi mtu mwenye akili timamu ajiunge na chama ambacho wamiliki wake wamekitegesha kama spea tyre!? kama wao ni wanaume kweli kwa nini wasikatae uwaziri waliohongwa na JK na waje kukijenga chama chao? hawa ni wanafki wakubwa, na kama Mwanakijiji ataendelea na mradi wake wa kukipa promo chama hiki basi atadhalaurika na kupuuzwa miongoni mwa watu wanaofikiri vizuri.
 
Naelewa hoja yako vizuri sana. Lakini naomba tu nawe uelewe nachojaribu kusema ni nini hasa.
 
Ndio tunayaona sasa, yanakwenda kutibiwa makanisani.

Halafu hawana mbinu wala ubunifu, mwenzao kaanzia makanisani na wao wanaona njia ndio hiyo hiyo.

Haya ni matokeo ya Siasa kuwa ajira badala ya wito. Lakini mbaya zaidi, pia tumeona kwa wale waliofanikiwa kimaisha nje ya siasa, roho zao hazitulii mpaka wawe na nguvu za kisiasa kwenye jamii. Hakika Tanzania kazi tunayo.
 
Back
Top Bottom