RaiaMbishi
JF-Expert Member
- Jan 18, 2012
- 252
- 124
Mkuu, itikadi ya CCK ni nini?
HOTUBA YA UTAMBULISHO WA CHAMA KIPYA CHA SIASA NCHINI CHA CCK
Itikadi yake Itikadi ya CCK ni uhafidhina wa kijamii na kiuchumi. Yaani, socio-economic conservatism. Itikadi hii msingi wake ni historia yetu kama taifa na kama jamii ya watu. Tunaamini kuwa tishio kubwa kabisa katika jamii yetu ni kuvunjwa vunjwa kwa familia ya Kiafrika na vile vile matumizi makubwa ya serikali kwenye mambo mengi ambayo kwa kweli serikali isingestahili kuwa inayafanya.
Hivyo, CCK ni chama ambacho kinataka kutetea na kuyahifadhi mambo ya msingi yanayoifanya jamii yetu kuwa ya Kiafrika katika ulimwengu wa kisasa na hasa kutetea na kulinda familia. Tunaamini kabisa kuwa sera zozote na mipango yoyote ya nchi ambayo haiweki mkazo katika kuipa nafuu na kuboresha maisha ya familia sera hizo ni za kutupwa mbali.
Kwa muda mrefu sasa nchi yetu imejiingiza kwenye sera zenye kutukuza kile kinachoitwa "soko" matokeo yake wakati wenye "soko" wakiendelea kufanya vizuri mamilioni ya familia za Watanzania wanaishi maisha ya wasiwasi wa kudumu. Hivyo, tunataka kupendekeza sera ambazo zitalenga kuinua maisha ya wananchi wetu na hivyo kuinua maisha ya familia.
Katika kutengeneza itikadi hii mpya chama chetu kitachota pasipo haya wala kuomba radhi katika hazina ya hekima ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kujifunza huku tukiboresha nadharia zake nyingi ambazo tunaamini ni msingi wa kujenga taifa la watu walio sawa na wenye kuheshimu utu wa watu wote.
HIvyo, tutapinga ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya Mtanzania mwingine, tutapigania maadili bora ya viongozi na kuhakikisha kuwa misingi iliyiounda taifa letu ikiwemo kupigania umoja wa Afrika, usawa na haki vinasimamiwa tena. Hatutavumilia kauli za kibaguzi zitakapotolewa na kiongozi au taasisi yeyote; kama Mwalimu alivyosema "Tanzania ni ya wote, na Watanzania ni wote"
Kwa kweli ni chama mbadala hasa wa CCM na kinataka kuwarudishia wananchi wa Tanzania fahari yao. Tunataka kurudisha ule moyo wa uzalendo, kuipenda Tanzania na kuona fahari kuwa sisi ni Watanzania.
mzee 6 , mwakyembe na nape watajiunga lini?
assume amejiunga JF kutangaza chama, tatizo liko wapi?
Tunawatakia Kila la kheri, ni matumaini yangu kuwa hakuna mkono wa ccm nyuma yenu kwa ninyi kujua au kutojua.
AKITANDA WEW NI MGENI HAPA AU??UKIPOST KITU KAMA HIKI NI LAZIMA URUDI NA KUJIBU MASWALI SASA WEWE UNAWEKA NA KUKIMBIA KAMA UMEJISAIDIA MAHALI NA KUONDOKA SIO SAWA RUDI HAPA UJIBU MASWALI,MIMI NITAJIUNGA NA CHAMA CHAKO KAMA UTAJIBU KWA UFASAHA HAYA YAFUATAYO
-CCK KINA KATIBA,kama ipo weka hapa kama hamna mna mpango gani
-UCHAGUZI WA CCK ULIFANYIKA LINI-umesema wewe ni mwenyekiti wa CCK taifa,mlichagua lini??
-CCK ina wanachama wangapi kila Mkoa tafadhali
-JE CCK MNA OFISI YA KUDUMU??
-MNAPATA HELA ZENU KUTOKA WAPI??
-MISINGI YENU IKOJE KULE UPANDE WA PILI WA JAMHURI(PEMBA NA UNGUJA)
JIBU HAYO HALAFU NITAULIZA MENGINE BAADA YA MAJIBU YAKO,USISAHAU KUWEKA HAPA FOMU YA KUJIUNGA NA GHARAMA ZENU
Mkuu, itikadi ya CCK ni nini?
Naona mmefanyia kazi utabiri wa Shekeh Yahaya. Kimsingi, kuitikia witu wa mtu aliyekuwa akiongozwa na mashetani maana yake ni kuiweka nchi chini ya majini na mashetani. Ni tatizo hili hili ambalo limepelekea nchi yetu kuwa katika hali ngumu ya kiuchumi, kielimu na kisiasa.
Ningependa kuuliza ni nini hasa mlichoona hakikidhi haja zenu katika siasa za upinzani mpaka mfikie maamuzi haya. Chadema katika siku za karibuni wamekuwa wakifanya vizuri sana. Kwa nini msingewaunga mkono ili kuweza kukamilisha ukombozi wa nchi? Je ni nini kitakachonishawishi nisiamini kwamba ninyi mnatumika kisiasa kupunguza kura za upinzani ambao chadema imeujenga? Hivi ninyi magamba mtaendelea kuigawa nchi yetu hata lini?
CCJ= Chukua Chako Jiondoe (ISSUE IMEKAA KI RUZUKU RUZUKU)
Asante sana, sasa hapa umeteguwa kitendawili kwahiyo tunafahamu vyema sasa kwamba upo hapa JF kwa malipo maalum!! ila sidhani kama kuna chama kinachoweza kukulipa ujila wako zaidi ya CCM.Mie mkinilipa ntawafanyia kazi zenu. Bure hamnipati.
soma hapa tafadhali,maana inaonekana watu hamsomi na mnakurupuka kujibu
Mfumo wa siasa hapa nchini Mojawapo ya matatizo makubwa ambayo yanatusumbua sasa hivi nchini na ambayo athari zake zinatoka kizazi kimoja kwenda kingine ni mfumo wetu wa kisiasa nchini. CCK inaamini kuwa mfumo huu wa kisiasa umepitwa na wakati na hauendani kabisa na matamanio ya kujenga taifa la kidemokrasia. Baadhi ya vitu ambavyo tunaamini vimepitwa na wakati na ambavyo vinahitaji kuondolewa mapema zaidi ni suala la ruzuku kwa vyama vya siasa.
Mfumo wa ruzuku uliingizwa kwenye siasa zetu na CCM kwa ajili ya kutafuta njia rahisi ya kupora raslimali zetu na kujinufaisha kwa migongo ya Watanzania. Hakuna sababu wala ulazima wa chama cha siasa kupewa fedha za umma kwa sababu tu ina watu waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali huu ni wizi wa wazi! Sisi kama CCK tunataka na tutapigania hatimaye kuondolewa kwa mfumo huu wa ruzuku kwa vyama vya siasa kwani vinazawadia uzembe na ubadhirifu.
Iweje chama ambacho kimeshindwa kusimamia serikali yake na ufisadi umeshamiri chini yake bado kinapewa kila mwezi mabilioni ya fedha ambayo hayajafungwa na utendaji kazi wa chama hicho?
Yaani, haijalishi CCM inatawalaje lakini bado inalipwa kila mwezi na Watanzania! Hivyo, kinyume na vyama ambavyo vinaweza kudaiwa kuwa vimeundwa kwa ajili ya ruzuku CCK imeundwa huku ikiwa inatambua kuwa mfumo wa ruzuku ni wa hatari kwenye siasa zetu na kwa kweli ndio umechangia sana kuchelewesha kungolewa kwa CCM madarakani!
Hivyo, katika mjadala wa Katiba Mpya sisi kama chama tutapigania na kuhakikisha kuwa ruzuku kwa vyama vya siasa zinafutwa ili kila chama kitegemee wanachama wake na akili zake kujiendesha. Kwani TANU ilipewa ruzuku na serikali ya Mkoloni ili ifanye siasa? Si ilitegemea wanachama wake? Kwanini kama wakati huo iliwezekana leo ishindikane?
Mwanakijiji, ni mwenzenu? Ebu weka katiba ya chama tuipitie kama inafaa.
Mimi ni mfadhili wa Demokrasia natumia resource zangu kuchangia mabadiliko wala bila kuwa na nia ya uongozi wa kisiasa, na mara nyingi tu nimewafadhili wanaCCM mtaani kwangu kwa shughuli zao za kichama ikiwemo hata kutoa gari yangu kuwasaidia misafara yao.Kwa sasa hivi silipwi, umenoa, jaribu tena baadae! Tena nilishawahi kumtumia Nape PM kuwa waanze kunilipa maana mashambulizi nnayopata hapa JF yakiambatana na matusi si kazi ndogo. Kanchunia.
Vipi, Mbowe analipa?
Jitu zima maswali ya kitoto...shame on you!!