Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,210
- 2,892
Historia ya kuanzishwa kwa vyama vya wafanyakazi ilikuwa ni kuja kuwa sauti ya wafanyakazi dhidi ya mwajiri
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wamekiuka lengo na kuvigeuza kuwa vitegauchumi vya kujichotea hela na kuwatelekeza wanachama wao
Moja ya chama hicho ni Chama cha walimu Tanzania (CWT). Kwa miaka mingi walimu wamelia sana na hiki chama hadi kufikia hatua ya kuanzisha vyama vingine mbadala vinavyohudumia kada hiyo hiyo ya walimu
Mwanzo waliona kama utani, sasa wanachama wengi wanaikimbia CWT na kujiunga na hivyo vyama vipya jambo linalotishia kushuka kwa mapato huko CWT
Baada ya hizo Movements za walimu, Tazama namna CWT walivyoanza kuhaha;
Chama cha walimu nchini (CWT) kimeiomba Serikali kudhibiti uanzishwaji holela wa vyama vya wafanyakazi ili kuzuia mgawanyiko miongoni mwa wafanyakazi na kupunguza ufanisi wa kazi kikidai kuwa baadhi ya vyama hivyo vimekuwa vikieneza propaganda za kuwavuruga wafanyakazi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu nchini (CWT), Magesa Magesa amewasilisha ombi hilo Kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Uhusiano, Dk. Evaline Munisi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uongozi kwa wenyeviti wa mikoa na wilaya wa chama hicho nchini yanayofanyika jijini Mbeya.
Amesema hivi karibuni vimeibuka baadhi ya vyama vya walimu ambavyo vimekuwa vikieneza propaganda na kuwahamasisha walimu kuhusu mambo mbalimbali bila kuwa na mifumo sahihi ya uendeshaji wa shughuli hizo.
Alisema endapo uanzishaji wa vyama hivyo hautadhibitiwa, kuna uwezekano wa kuongezeka migogoro ya wafanyakazi badala ya kupungua na hivyo kudhoofisha utendaji kazi wa wafanyakazi.
“Endapo vyama hivi havitadhibitiwa kuna hatari ya kuongeza migawanyiko miongoni mwa walimu, kupunguza ufanisi katika utekelezaji wa sera za serikali na kuathiri mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji na hivyo kupunguza hata ufaulu wa wanafunzi,” amesema Magesa.
Kaimu Rais wa CWT, Shaban Ambindwile amesema baadhi ya vyama vya wafanyakazi vimeanzishwa na kusajiliwa lakini havina watendaji walioajiriwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya wafanyakazi.
Amesema baadhi ya vyama hivyo havina ofisi na hivyo huwa vinatumia ofisi za mwajiri jambo ambalo ni kinyume na taratibu na linasababisha ufanisi mdogo kwenye utendaji na kutumia muda vibaya.
Imeandikwa| Nebart Msokwa